Posts

CHADEMA YASITISHA MAANDAMANO YA UKUTA SEPTEMBA MOSI.

Image
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA Mh.Freeman Mbowe, amesitisha shughuli za maandamano zilizokuwa zimepewa jina la (UKUTA) kwa Muda wa mwezi mmoja,kwa kile alichodai baada ya kuombwa na viongozi wa Dini na taasisi Mbalimbali, ambapo maandamano hayo yalitarajiwa kufanyika kesho Septemba Mosi nchi nzima. Mbowe ametoa kauli hiyo ya kuahirisha kwa maandamano hayo mapema leo mchana wakati akizungumza na Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari.Amesema sababu kubwa za kuahirisha maandamano hayo ni busara za viongozi wa dini ambao wameiomba Chadema iwape muda wa kutafuta Suluhu .  Viongozi mbalimbali wa kidini pamoja na Taasisi mbalimbali za kiraia hatimaye wamesaidia kutokomeza UKUTA kwa kuuomba uongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kuahirisha Oparesheni hiyo iliyopangwa kufanyika Septemba mosi nchi nzima.  Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Makao Makuu ya CHADEMA Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa,  Freema...

GERSON MSIGWA ATEULIWA KUWA MKURUGENZI KAMILI WA MAWASILIANO IKULU.

Image
Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Rais, (Director of Presidential Communication - DPC). Bw. Gerson Partinus Msigwa,aliyethibitishwa leo na Rais Dkt John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemthibitisha   Bw. Gerson Partinus Msigwa kuwa Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Rais, (Director of Presidential Communication - DPC). Taarifa iliyotolewa leo Jumatano Agosti 31,2016 na Katibu Mkuu Ikulu Bw. Peter Ilomo imeeleza kuwa Bw. Gerson Partinus Msigwa amethibitishwa kuanzia leo tarehe 31 Agosti, 2016 kushika wadhifa huo. Kabla ya uthibitisho huo,   Bw. Gerson Partinus Msigwa   alikuwa Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Rais, katika Ofisi ya Rais Ikulu kuanzia tarehe 17 Novemba, 2015. Jaffar Haniu Kaimu Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi. Dar es Salaam 31 Agosti, 2016

RC. NDIKILO, ASEMA ULINZI UMEIMARISHWA MKOANI PWANI.

Image
MWENYEKITI wa kamati ya ulinzi na usalama mkoani Pwani,mhandisi Evarist Ndikilo,amesema wanaendelea na mapambano katika eneo la Vikindu na kuimarisha ulinzi wilayani Mkuranga kufuatia kutokea matukio ya uvunjifu wa amani yaliyotokea hivi karibuni. Aidha amevitaka vyama vya  siasa mkoani humo, kuacha kufanya maandamano ikiwemo ya umoja wa kupinga udikteta(UKUTA)na chama kitakachobainika hatua kali zitachukuliwa. Katika hatua nyingine mhandisi Ndikilo ,amewaomba viongozi wa dini wasichoke kuliombea taifa,kumuombea rais John Magufuli na viongozi wote ili waendelee kuwatumikia wananchi kwa maslahi mapana ya taifa. Aliyasema hayo, wakati kamati ya amani ya mkoa wa Pwani,ilipokwenda kutoa pole kwa kamati ya ulinzi na usalama mkoani humo, kutokana na matukio ya kiuhalifu yaliyotokea wiki iliyopita wilayani Mkuranga. Alisema kuwa serikali hiyo, imejipanga kikamilifu kulinda amani ya wananchi na mali zao sambamba na kuimarisha ulinzi wilayani Mkuranga na maeneo meng...

AJALI, SANZALE BAGAMOYO, GARI LA PEPSI LAGONGANA NA ROLI KUBWA LA MIZIGO.

Image
Magari mawili ya mizigo yamegongana mchana huu eneo   la Sanzale kichem   chem kati ya Roli kubwa lenye tera namba T.682 DFF la Kampuni ya   PWANI HAULIERS LTD. (PHL) lililokuwalimebeba mzigo, na Canter ya pepsi   yenye namba T. 912 DCC ambalo   lilikuwa limebeba soda. Kwa mujibu wa dereva Roli lenye Tera, Shomari Shomari aliiambia Bagamoyokwanza kuwa yeye alikuwa anakunja kuingia kiwandani kuingiza mzigo ambapo kutokana na   urefu wa gari alilazimika kuzidi upande wa kulia   ili apate kona ya kukunja kuingia kushoto kwenye Kiwanda. Shomari aliendelea kusema kuwa, mara baada yeye kuzidi upande wa kulia akiwa ameshaakunja kuingia kusho   kiwandani, mwenye gari ya soda amekuja nyuma yake na kupitia kushoto   ambapo gari ya soda ilikwenda kugonga moja kwa moja kwenye mlango Roli kubwa na kusababisha Ajali iliyopelekea Dereva   wa Gari la Soda kuumia na kukimbizwa Hospitali huku   soda zikiwa zimevunjika. Wananchi m...