Katibu Wa Itikadi Na
Uenezi CCM Ndg. Shaka Hamdu Shaka ,Wananchi na Baadhi ya Viongozi wa Chama Cha
Mapinduzi wakipita katika Njia ya Watembea kwa miguu Kukagua maendeleo ya
ujenzi wa daraja jipya la Wami ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 89.02 na
zaidi ya Sh. bilioni 75 zimepangwa kutumika.
..............................................
DARAJA
Jipya la Wami lenye urefu wa mita 513.5 na barabara unganishi ya kilometa 3.8
litaanza kutumika Septemba 30, 2022.
Akizungumza
katika ziara yake leo Septemba 18, 2022 Katibu, wa Itikadi na Uenezi wa Chama
cha Mapinduzi (CCM), Shaka Hamdu Shaka amesema serikali imeridhishwa na ujenzi
wa daraja hilo la Wami ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 89
-
"Daraja
hili lilianza ujenzi mwaka 2018, hadi Rais Samia Suluhu Hassan anaingia
madarakani ujenzi ulikua umefika asilimia 47, lakini ndani ya mwaka mmoja wa
Rais Samia, kasi imeongezeka kwa asilimia 42 na sasa wataalamu wanatuambia
ujenzi umefikia asilimia 89," amesema Shaka na kuongeza
-
“Pongezi
zetu ziwafikie wakandarasi ndani ya kipindi kifupi tuliambiwa daraja hili
lingeanza kazi Septemba 20 tukasema haitawezekana lianze kazi kabla ya chama
kufika hili jambo ni kubwa, ni utekelezaji wa ilani ya CCM ibara 55 (d)
(1)....; "CCM inaridhishwa, na kazi zinazofanywa na serikali” alisema
-
Alisema
daraja hilo limebeba maslahi mapana ya Watanzania kwa kuwa linakwenda
kuunganisha Mikoa yote ya Kaskazini na nchi jirani ikiwemo Kenya hivyo fursa
ambazo zitatokana na daraja hilo ni nyingi hasa kiuchumi.

Katibu wa
Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka
akiwa na viongozi, wana CCM na wataalamu wakipita juu ya Daraja la Wami mkoani
Pwani alipotembelea ujenzi wa daraja hilo.

Katibu wa
Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka
akizungumza na viongozi, wana CCM na wataalamu wakati alipotembelea ujenzi wa
Daraja la Wami mkoani Pwani.