Wednesday, October 30, 2019

TGNP kufanya mapitio ya sera na ilani za vyama vya siasa nchini

TGNP Mtandao imepanga kufanya mapitio ya sera na ilani za vyama vya siasa kwa mrengo wa kijinsia na kushauri kufanya marekebisho mapema kabla ya uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.
Viongozi mbalimbali wa chama cha ACT Wazalendo wakiwa katika picha ya pamoja na wageni wao kutoka TGNP Mtandao, wakionesha Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2019 iliyotengenezwa na TGNP Mtandao kwa kushirikiana na wadau wengine wa haki za wanawake.

Akizungumza wakati wa ziara ya kukabidhi ilani ya madai ya wanawake katika uchaguzi wa serikali za Mitaa wa mwaka 2019 na uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 kwa chama cha ACT wazalendo,  Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao  Lilian Liundi, alisema kwamba baada ya kutembelea vyama kadhaa vya siasa nchini na kusikiliza jinsi wanavyotekeleza masuala ya kijinsia, ameona kuwa kuna haja ya TGNP na Mashirika mengine yanayotetea haki za wanawake na Usawa wa Jinsia, kufanya uchambuzi au mapitio ya sera na ilani za vyama kwa mrengo wa kijinsia na kuangalia mapengo ili kushauri marekebisho.
“Tunapoelekea uchaguzi wa seriali za Mitaa,  na uchaguzi mkuu mwaka ujao 2020, tunahitaji vyama hivi kuzingatia kwa kiasi kikbwa usawa wa kijinsia kwenye uteuzi wa wagombea. Kama chama hakina sera za ndani ambazo zina mrengo wa kijinsia, ni lazima mapendo yataendelea kuwepo. Tunashukuru kwamba vyama  vya siasa vimejitahidi, lakini bado hatujafikia malengo” Alisema.
Kwaupande wake Kaimu Mwenyekiti wa Taifa wa ACT Wazalendo, Doroth Sembu alisema kwamba, pamoja na kwamba chama kinajitahidi kutoa fursa sawa kwa wanawake bado watajitahidi kuendelea kuteua wanawake kushiriki kwenye chaguzi.
“mwaka huu tumejipanga kwenye uchaguzi wa serikali za Mitaa, tutahakikisha kila mahali ambapo wanawake wamejitokeza wanapata nasi, lakini kwa sababu mmetuletea hii Ilani yenu, tutahakikisha tunaitumia  ili wagombea watakao shinda wakatekeleze ilani husika” alisema Semu
Ilani ya Madai ya wanawake kwa  uchaguzi wa serikali za Mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu 2020 iliyoandaliwa na TGNP Mtandao kwa kushirikiana na Mtandao wa wanawake na Katiba, imewashirikia na kukusanya maoni ya wanawake kutoka katika makundi yote nchini hasa vijijini. Asasi za kiraia zinazotetea haki na usawa wa Kijinsia zaidi ya 60 zimeshiriki.

Dkt. Bashiru Ally: wanawake ni walinzi wa rasilimali wakipewa nafasi za uongozi

Mwanyekiti wa Bodi ya TGNP Mtandao, Aseny Muro akimkabidhi Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally, Nakala ya Ilani ya madai ya wanawake katika uchaguzi  wa serikali za Mita 2019 na uchaguzi Mkuu 2020 leo katika Ofisi ndogo ya CCM Lumumba Dar es salaam, Anayefuatia ni Mkurugenzi Mtenaji wa TGNP, Lilian Liundi.

Na Deogratius Temba.
Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt Bashiru Ally, ameyataka mashirika yanayotetea haki za wanawake na usawa wa Kijinsia kutoa elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa ushiriki wa wanawake katika nafasi za maamuzi ngazi ya jamii  ili kulinda rasilimali za umma na kuhakikisha  zinawanuafaisha wananchi wote.
Akizungumza wakati wa kikao kifupi cha TGNP na CCM makao makuu kilichokuwa na lengo la kukabidhi Ilani ya madai ya wanawake katika Uchaguzi wa serikali za Mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020, Dkt bashiru alisema kwamba, TGNP Mtandao imefanya kazi kubwa ya kuhakikisha jamii inapata uelewa wa kudumu juu ya haki zao na uwajibikaji wa wananchi katika kulinda, kutunza na kuendeleza rasilimali zao.
“ Ninajua jinsi ambavyo TGNP Mtandao, imejikita katika kujenga uelewa kwa wananchi, mifumo na mbinu mnazotumia kufikia wananchi ni mizuri, ninajiuliza tu, nchi hii ni kubwa ni namna gani mtaweza kufikia watu wengi zaidi? Je mnazo rasilimali za kufika kila mahali? Mbinu zinazotumika kutoa mafunzo zinaweza kuwafikia wote? Au tubadilishe mbinu? “   alisema Dkt Bashiru
Alisema kwamba TGNP na asasi zingine za kiraia ni muhimu kuendelea kuweka nguvu katika kuelemisha jamii, kujenga uwezo kwa wananwake kuwa viongozi wazuri, kufikia mifumo yote ya kijamii na kiseirkali ili kuhakikisha tunakuwa na taifa linalojali na kuheshimu masuala ya usawa wa kijinsia katika Nyanja zote.
Alisisitiza kuwa. “TGNP na wengine, jengeni uwezo kwa kamati muhimu ambazo wanaawake wanaziongoza, mifumo mizuri inayowagusa watu ni ile iliyoko chini kabisa kwenye jamii, mfano, kamati ya maji, ardhi, mazingira… waelimisheni vizuri na kama kuna wanawake wameshika nafasi humo waoneshe mabadiliko ya haraka, jamii inaheshimu na kuona kwamba  kuna  umuhimu wa wanawake kushika nafasi za maamuzi”
Naye Mwenyekiti wa TGNP Mtandao, Aseny Muro, alimshukuru  katibu Mkuu kwa kazi nzuri na kumshukuru Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt. John Magufuli kwa kuendelea kulinda na kutetea rasilimali za taifa ambazo nyingi zinawanufaisha wanawake na watoto ikiwepo kuboresha huduma za jamii.
Ilani ya madai ya wanawake katika uchaguzi wa serikali za Mitaa 2019 na uchaguzi Mkuu 2020, imeandaliwa na Mtandao  wa Wanawake na Katiba na uongozi na Mfuko wa Wanawake Tanzania (WFT).

Tuesday, October 29, 2019

KIKWETE AONGOZA MAZISHI YA WATU 11 WALIOKUFA KWA MAJI.

 
MBUNGE wa jimbo la chalinze wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, Ridhiwani Kikwete, (kushoto) akizungumza jambo na Mkuu wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe.
............................................
Na shushu Joel

MBUNGE wa jimbo la chalinze wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, Ridhiwani Kikwete, amewaongoza viongozi wa serikali na wananchi mbalimbali katika mazishi ya watu 11 katika kata ya Msata.

Watu hao wamekufa kutokana na ajali mbaya walioipata walipokuwa wakisafiri kuelekea Tanga na gari lao aina ya noah kutumbukia darajani na wote kupoteza maisha.

Alisema kuwa ajali hiyo imetokea maeneo ya mpakani mwa jimbo la chalinze na handeni ambapo gari yao ilianguka mara baada ya daraja dogo kutumbikiwa mtoni.

Aliongeza kuwa kuna familia moja ya watu sita na mtumishi mmoja wa halmashauri ya chalinze aliyefariki na familia yake ya mama na watoto 3.

Aidha alisema kuwa vifo hivi ni pigo kwa taifa na masikitiko ya hali ya juu.

"Nimesononeshwa sana na tukio hili jana tu nimezika ndùgu zangu 6 wa familia moja Leo tena nazika mtumishi wa halmashauri yangu ya chalinze ambaye alikuwa ni afisa uchaguzi , mke wake na watoto wake 3 inasikitisha sana" alisema Kikwete.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya handeni Godwin Gondwe ambaye tukio hilo limefanyika kwenye eneo lake amewataka wananchi kuendelea kuwa na imani na serikali yao kwani ipo pamoja kwa kila jambo.

Aidha amempongeza mbunge wa chalinze kwa kushiriki katika tukio hilo kuanzia mwanzo mpaka mwisho.

Naye mwakilishi wa mkuu wa mkoa wa pwani ambaye ni mkuu wa wilaya ya kisarawe Jokate Mwegelo amewapa pole wafiwa na kuwahakikishia serikali ipo nao kwa kila jambo.

Aliongeza kuwa ameushukuru uongozi wa wilaya ya handeni kwa ushirikiano mkubwa waliouonyesha katika kuwasaka na kuokoa miili ya wananchi wenzao.

Kwa upande wake msemaji wa familia Abdullah Semiono ameipongeza serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli kwa kusimamia na kuhudumia msiba wa ndugu zake.

Aliongeza kuwa kuna waliotangaza vibaya juu ya tukio hili kuhusu serikali naomba wabezwe kwani serikali imetusimamia na kutuhudumia kwa kila kitu kwenye msiba wetu.

"Niaze kwa kumshukuru mbunge wetu Ridhiwani Kikwete,mkuu wa wilaya ya Handeni Godwin Gongwe na kisarawe Joketi Mwigelo kwa ushirika wa dhati katika tukio hili" Alisema
 
 MBUNGE wa jimbo la chalinze wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, Ridhiwani Kikwete (kulia) akisalimiana na Kaimu Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, ambae ni Mkuu wa wialaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo ambaye katika mazishi hayo alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Pwani.

 Majeneza yaliyobeba miili ya marehemu hao

MBUNGE KAWAMBWA AGAWA MILIONI 31 KWA VIKUNDI BAGAMOYO.

Mbunge wa jimbo la Bagamoyo, Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa, akikabidhi hundi kwa Kudura Selemani kutoka kikundi cha Ushirika.
........................................
 Mbunge wa jimbo la Bagamoyo, Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa, amegawa fedha zaidi ya milioni 31 kwa vikundi na taasisi katika jimbo hilo.

 
Akizungumza mara baada ya kukabidhi fedha hizo Dkt. Kawambwa alisema kuwa, fedha ni zile za mfuko wa jimbo ambazo zipo kisheria na zinatolewa na serikali kwaajili ya kusaidia mambo mbalimbali katika jimbo husika.


Alisema fedha hizo alizogawa ni jumla ya 31, 801,000 ni kwaajili ya kuchochea maendeleo kwa vikundi vya wajasriamali na taasisi ambazo hazipaswi kurudishwa.
Aidha, alitoa wito kwa wananchi wa jimbo la Bagamoyo, kujiunga katika vikundi ili weweze kuwa na sifa ya kupata fedha za mfuko wa jimbo na zile asilimia kumi zinazotolewa na Halmashauri.


Alisema serikali imetenga fedha kwaajili ya kuwezesha wananchi katika maeneo mbalimbali ambapo ili uweze kupata fedha hizo ni lazima muwe katika kikundi.


Alifafanua kuwa, serikali haiwezi kugawa fedha kwa mtu mmoja mmoja ispokuwa fedha zitatolewa kwa vikundi ili iwe manufaa kwa watu wengi zaidi.


Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bagamoyo, Ally Ally Issa amewataka wanavikundi na taasisi zilizopata fedha hizo kuzitumia katika malengo yaliyokusudiwa  ili zilete tija kwenye jamii.


Alisema ni kweli fedha hizo hazitarudishwa lakini vikundi vitapitiwa kukaguliwa ili kujiridhisha kuhusu matumizi ya fedha hizo.


Kwa upande wao wanavikundi waliopata fedha hizo wamemshukuru Mbunge Dkt. Kawambwa kwa kupatia kiasi hicho ambacho kitasaidia katika kusukuma maendeleo kwenye maeneo yao.


Walisema serikali ya awamu ya tano imekuwa ikijali watu wa aina zote na ndioamana fedha hizo zimewafikia jambo ambalo hawakulitarajia.
 
Mbunge wa jimbo la Bagamoyo, Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa, akikabidhi hundi kwa Golden Mwenda Magagula kutoka kikundi cha Unjacha.
 
Mbunge wa jimbo la Bagamoyo, Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa, akizungumza na wana vikundi katika ukumbi wa Halmashauri ya Bagamoyo, kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bagamoyo, Ally Ally Issa, na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya hiyo, Fatuma Omari Latu.


 Kutoka kulia ni Diwani wa viti maalum, Hapsa Kilingo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bagamoyo, Ally Ally Issa, Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bagamoyo, Fatuma Omari Latu, Katibu wa CCM wilaya ya Bagamoyo, Salum Mtelela, na Amina Ramadhani.

Diwani wa kata ya Zinga, Mohamedi Mwinyigogo (kulia) akiwa na Diwani wa viti Maalu, Shumina Rashidi, wakimsikiliza katibu wa Mbunge, Magreth Joseph aliyesimama.