Monday, November 28, 2016

MBUNGE WA CHALINZE RIDHIWANI AKABIDHI VISIMA VITATU VYENYE THAMANI YA SH.MILLION 84.5

Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete, wa kushoto akiwa na Afisa Mtendaji  wa Shirika lisilo la kiserikali toka Nchini Omani linaloitwa  TUELEKEZANE PEPONI  Bw.Nasr Al Jahdhamy  wakati wa kukabidhi visima vitatu kwa wananchi wa jimbo hilo.
 
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete, wa pili kutoka kushoto anayemfatia ni Afisa Mtendaji  Bw.Nasr Al Jahdhamy mwakilishi kutoka Oman na Katibu wa Mbunge Bwana Iddi Swala na Mzee Maokola wakati wa kukabidhi visima vitatu kwa wananchi wa jimbo hilo.
 
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete, akiongea na wananchi wa jimbo hilo  akiwa na Afisa Mtendaji  wa Shirika lisilo la kiserikali toka Nchini Omani linaloitwa  TUELEKEZANE PEPONI  Bw.Nasr Al Jahdhamy  wakati wa kukabidhi visima vitatu kwa wananchi wa jimbo hilo.
.................................
 
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete amekabidhiwa visima Vitatu vyenye thamani ya  Shilingi Milioni 48.5 toka kwa Shirika lisilo la kiserikali toka Nchini Omani linaitwa kwa  TUELEKEZANE PEPONI  chini ya Afisa Mtendaji wake Nasr Al Jahdhamy.

Akizungumza wakati wa kukabidhi visima hivyo  Mbunge huyo alisema kuwa , shida ya maji ndani ya Halmashauri ya chalinze imekuwa kubwa na kueleza kuwa kazi iliyofanyika kufanikisha ujenzi wa visima hivyo ni kubwa ili kusaidia tatizo hilo kwa kipindi hiki wakati wakisubiri kukamilika kwa ujenzi wa mradi wa kutoa maji mto wami. 

“Nimeona nifanye kazi ya kutengeneza visima ili kupunguza ukali wa uhaba wa maji kwani matengenezo ya mradi wa wami bado yanaendelea kuchimbwa kwa visima hivi si ishara kuwa ule mradi wa maji ambao tuliongea kuwa umekufa mradi wa wami utakapokamilika tunataraji utawanufaisha wananchi wengi wa jimbo letu.”alisema Ridhiwani

Aidha  visima hivyo vitatu vimekabidhiwa katika  kijiji cha matipwili , shule ya sekondari ya matipwili na kijiji cha Gongo ambavyo vinaendelea kujengwa na vinataraji kukamilika mapema ndani ya wiki ijayo.

Naye Bwana Naseer aliahidi kuendelea kumsaidia Mbunge kufikia malengo yake ya kusaidia kutatua changamoto zinazokabili nyimbo hilo,na kuongeza kuwa atasaidia  kuchimba visima vingine kumi katika Halmashauri hiyo na kusaidia michezo.

BONANZA LA MICHEZO BAGAMOYO, HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAICHAPA KILUNGULE MABAO 3-0.

Bonanza  la michezo liliofanyika jana Tarehe 27 Novemba, katika uwanja wa Mwanakalenge Bagamoyo mjini, limejumuisha timu 11 kutoka Dar es slaam na  Pwani na kulifanya  liwe kivutio cha aina yake  pale timu za maveterani zilipomenyana vikali katika kuonyeshana  uwezo.

Katika michezo hiyo timu ya Halmashauri ya Bagamoyo iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya timu ya Kilungule, Timu ya  Mapinga ilichuana na Neibour ambapo Neibour ilitoka na ushindi wa bao 1 na Mapinga haikupata kitu.

Aidha katika Mechi nyingine Mapinga ilicheza na Temboni ambapo Temboni  waliichapa Mapinga bao  1-0,  Timu ya Mwenge Veterani imeilaza Timu ya Leaders mabao 2-0, huku Corner ikwa imeichapa Kibamba mabao 2-0, na Kibaoni imeibuka na ushindi wa bao 1 dhidi ya Golan ambayo haikupata kitu.

Kwa upande wake Mratibu wa Bonanza hilo, Deodatus Katambi alisema Bonanza hilo limefanikiwa kwa kiasi kikubwa  kwakuwa   matarajio yalikuwa ni kuwa na timu 6 lakini zimepatikana timu 11 zilizoshiriki katika michezo hiyo.

Alisema watu wanapenda Michezo bila ya  kujali umri wao na kwamba kinachokosekana ni kumpata mtu wa kuwaunganisha  pamoja ili waweze kuonyesha uwezo wao.

Katambi ambae ni katibu wa Temboni Veterani ambao ndio walioandaa Bonanza hilo, alisema timu zote zilionyesha uwezo mzuri na kupelekea ushindani kuwa mkubwa jambo ambalo liliwavutia watazamaji.

Aliongeza kwa kusema kuwa, timu ya Halmashauri ya Bagamoyo ilikuwa vizuri katika mchezo na kutoa wito kwa serikali kuzijengea uwezo timu za Halmashauri ili kupata timu bora itakayoleta burudani katika sherehe  mbalimbali na kuwajengea afya bora kutokana na mazoezi.

Mechi hizo zilizochezwa katika uwanja wa mwanakalenge mjini Bagamoyo zilichezeshwa na waamuzi Raphael Ntasi, Idi  Mpingo, Jafari Shaweji, wengine ni Hamadi  Kidodi, Shabani  Milao na Mohamedi  Toloa. 
Wachezaji wa timu ya Temboni veterani wakiwa katika Picha ya Pamoja kabla ya pambano lao na Mapinga Veterani, katika  Bonanza  la michezo lililofanyika uwanja wa Mwanakalenge Bagamoyo mjini.
Nyama choma, vinywaji na  vyakula vilipatikana katika Bonanza hilo 
 Wachezaji pamoja na watazamaji wakiwa wametulia kufuatilia michezo iliyokuwa ikiendelea
Mratibu m kuu wa Bonanza hilo kutoka Tembeni Veterani, Deodatus Katambi akizungumza na waandishi wa Habari.