Friday, August 18, 2023

RAIS, DKT. SAMIA AFANYA UTEUZI.

 



MAASKOFU KATOLIKI WATOA TAMKO MKATABA WA BANDARI.

 












MAKAMU WA RAIS DKT. MPANGO AONDOKA NCHINI ANGOLA

 


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango leo tarehe 18 Agosti 2023 akiondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa 4 De Fevereiro Jijini Luanda nchini Angola mara baada ya kuhitimishwa kwa Mkutano wa 43 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC). (kushoto ni Mke wa Makamu wa Rais Mama Mbonimpaye Mpango)



QS. OMAR KIPANGA AONGOZA WAUMINI KULIOMBEA TAIFA.

 


MOJA YA NDOTO YANGU KUHAKIKISHA MAFIA INAENDELEA KUWA SEHEMU DAIMA YA UPENDO AMANI NA MSHIKAMANO KWA KUMTANGULIZA MUNGU-QS KIPANGA"

MWANDISHI WETU

Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknologia Mhe Qs Omar Kipanga ameongoza Mamia ya Waumini katika Maombi ya kuliombea taifa pamoja na  viongozi mbalimbali wa Kitaifa katika Kuendelea kuwa na imani na Upendo kwa Jamii.


Akiziungumza wakati wa kongamano la amani na Upendo amesema miongoni mwa matarajio yake ni Kuendelea kuhakikisha kwamba Jimbo la Mafia linaendelea kuwa sehemu ya Upendo amani na mshikamano kwa watu wake Kila siku,


"Nafanya Kazi huku nawaza Kila siku kumuomba Mwenyezi mungu atubariki na kutuongoza katika Shughuli zetu za Kila Siku katika Amani, Upendo mshikamano kama ambavyo viongozi Wetu wanavyofanya kwa taifa letu hasa RAIS Dr Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais Dr Philip Mpango na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa Majaliwa alimalizia Mhe Qs Kipanga"


"Tumebahatika Tanzania kuwa na amani Upendo na Mshikamano basi tuendelee kuwaombea Dua Viongozi Wetu kwa Mwenyezi mungu kutuongoza Daima kwa Misingi ya Kumjua Mwenyezi mungu ili tubarikiwe katika mambo yetu sisi na Vizazi vyetu alisisitiza Mhe Qs Kipanga"




*"Kama unataka kuwa na amani ya Moyo kuwa na utamaduni wa Kusoma kitabu Cha Mwenyezi mungu Kila siku asubuhi na usiku wakati wa kulala utabarikiwa sana na Utakua na moyo wa Upendo kwa ndugu jamaa Zako lakini pia Utakua na Imani Ambayo itakuondosha na chuki na wivu alishauri Mhe Qs Kipanga Kipanga*"

MAGAZETI YA LEO IJUMAA TAREHE 18 AGOSTI 2023.

 














Thursday, August 17, 2023

MAKAMU WA RAIS, AMWAKILISHA RAIS DKT. SAMIA MKUTANO WA 43 WA SADC.

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC) kabla ya kuanza kwa Mkutano wa 43 wa Jumuiya hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Intercontinental Jijini Luanda nchini Angola leo tarehe 17 Agosti 2023.

....................................

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango leo tarehe 17 Agosti 2023 amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Mkutano wa 43 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC) uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Intercontinental, Jijini Luanda nchini Angola.

 

Mkutano huo uliobeba kaulimbiu ya “Umuhimu wa Rasilimali Fedha na Rasilimali Watu katika kuendeleza Viwanda na Uchumi” umehudhuriwa na viongozi Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya hiyo, Mawaziri, Viongozi wa Kisekta pamoja na Wakuu wa Majeshi. Baadhi ya masuala yaliyojadiliwa katika mkutano huo ni pamoja na uendelezaji viwanda kwa kuhakikisha uongezaji thamani wa bidhaa unafanyika ndani ya nchi wanachama ili kuongeza ajira na mapato kwa mataifa husika. Pia, Tanzania imesisitiza umuhimu wa usalama wa chakula pamoja na umuhimu wa kutafuta amani kwa nchi za Msumbiji na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

 

Katika Mkutano huo, Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mheshimiwa Felix Tshisekedi amekabidhi Uenyekiti wa SADC kwa Rais wa Jamhuri ya Angola Mheshimiwa João Lourenço. Pia, Rais wa Namibia Dkt. Hage Geingob amekabidhi Uenyekiti wa Asasi ya Ushirikiano katika Masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC Organ Troika) kwa Rais wa Zambia Mheshimiwa Hakainde Hichilema.

 

Mkutano huo, umetoa zawadi mbalimbali kwa washindi wa shule za sekondari wa shindano la insha la Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC) ambapo Mwanafunzi Hollo Kadala wa shule ya sekondari Msalato kutoka nchini Tanzania ameshinda nafasi ya tatu.

 

Mkutano wa 43 wa Wakuu wa Nchi na Serikali umetanguliwa na mkutano wa Kamati ya Baraza la Mawaziri la Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika tarehe 13–14 Agosti 2023.

 

Imeandaliwa na

Ofisi ya Makamu wa Rais

17 Agosti 2023

Luanda, Angola. 


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwasili katika Ukumbi wa Mikutano wa Intercontinental Jijini Luanda nchini Angola kushiriki Mkutano wa 43 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC) leo tarehe 17 Agosti 2023.





Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisalimiana na viongozi mbalimbali wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC) kabla ya kuanza kwa Mkutano wa 43 wa Jumuiya hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Intercontinental Jijini Luanda nchini Angola leo tarehe 17 Agosti 2023.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC) kabla ya kuanza kwa Mkutano wa 43 wa Jumuiya hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Intercontinental Jijini Luanda nchini Angola leo tarehe 17 Agosti 2023.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akijadiliana jambo na baadhi ya viongozi wa ujumbe wa Tanzania wakati wa Mkutano wa 43 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC) uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Intercontinental Jijini Luanda nchini Angola leo tarehe 17 Agosti 2023. (Kutoka kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Mbarouk, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kikanda Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Balozi Kennedy Gaston pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Zanzibar Jamal Kassim Ali)



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akishiriki Mkutano wa 43 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC) uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Intercontinental Jijini Luanda nchini Angola leo tarehe 17 Agosti 2023.




VIONGOZI WA WIZARA YA UTAMADUNI,SANAA NA MICHEZO WAENDELEA KUPATA UZOEFU WA MAGEUZI YA UTENDAJI

 


Na Shamimu Nyaki


 Viongozi na Wakuu wa Taasisi wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo wameendelea kupokea elimu kupitia Mada mbalimbali zinazotolewa na viongozi na Wataalam mbalimbali katika nyanja tofauti katika Kikao cha Faragha cha siku tatu cha viongozi hao kinachoendelea leo Agosti 17, 2023 mkoani Morogoro.


Viongozi hao chini ya Mwenyekiti, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Saidi Yakubu wamepokea Mada kuhusu Itifaki na Ustaarabu iliyowasilishwa na Bw. Batholomeo Jungu, Mkurugenzi wa Maadhimisho kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Mada kuhusu Rasilimaliwatu kama dhamana ya Taasisi iliyowasilishwa na Bw. David Nchimbi kutoka Taasisi ya Deloitte and Touche.


Maada nyingine ni Mabadiliko ya Kitaasisi kupitia uzoefu wa NSSF iliyowasilishwa na Mhe. Balozi Dkt. Ramadhan Kitwana Dau pamoja na Mada ya Tatizo letu ni nini dhidi ya matarajio yetu iliyowasilishwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Saidi Yakubu.


Aidha, Viongozi hao pia walipokea Mada kuhusu Sifa ya Uongozi katika ulimwengu wa kisiasa iliyowasilishwa na Bw. Kadari Singo kutoka Uongozi Institute ambapo walipata nafasi ya kuzijadili, kuuliza maswali, kutoa maoni, ushauri na kupata ufafanuzi wa maswala mbalimbali.