Sunday, August 6, 2023

USHIRIKIANO NA WADAU UTACHOCHEA MIUNDOMBINU BORA NA IMARA KWA ELIMU BORA-KIKWETE

USHIRIKIANO NA WADAU UTACHOCHEA MIUNDOMBINU BORA NA IMARA KWA ELIMU BORA-KIKWETE


Kiwanda cha kutengeneza Marumaru cha KEDA kilichopo Chalinze kimetoa Boksi 1750 zenye thamani ya Shilingi Milioni 46 ikiwa ni mchango wao kwa shule za sekondari za Jakaya Mrisho Kikwete na Miono High School zilizopo katika halmashauri ya Chalinze.


Akiwashukuru wahisani hao, Mbunge wa Jimbo la Chalinze na Naibu Waziri wa Utumishi na Utawala Bora Ndugu Ridhiwani Kikwete amewahasa Wananchi kutunza Mbinu hiyo ili kudumisha shule hizo.


#KaziInaendelea #Keda #Elimu 










 

BALOZI DKT. DAU ATEULIWA UWENYEKITI BODI YA UTALII.





 

MAGAZETI YA LEO TAREHE 06 AGOSTI 2023

 




















MAPOKEZI YA CDE KAWAIDA OFISI NDOGO ZA MAKAO MAKAO MAKUU YA UVCCM TAIFA

 


UVCCM TAIFA
05 AGOSTI, 2023

📍📍 _Upanga Dar es salaam_

*

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Taifa Ndugu Mohamed Ali kawaida (MCC) amewasili ofisi ndogo za Makao Makuu ya UVCCM Taifa ambapo anaongoza kikao cha Kamati ya Utekelezaji UVCCM Taifa tarehe 05 Agosti, 2023.

Makamu Mwenye wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Rehema Sombi Omary (MNEC) Amewaongoza Wajumbe wa kamati ya Utekezaji pamoja na Watumishi wa Jumuiya katika mapokezi ya Ndugu Kawaida.

Imetolewa Na:

Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Taifa

#SautiYaVijana
#MtumishiWenu
#SautiYenu
#KulindaNaKujengaUjamaa
#SisiNaMamaMleziWaWa





RAIS WA ZANZIBAR MHE.DK.HUSSEIN MWINYI AZUNGUMZA NA WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS MIPANGO NA UWEKEZAJI TANZANIA MHE.PROF. KITILA MKUMBO IKULU


 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi  akimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Tanzania Mhe.Prof. Kitila Mkumbo, alipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha akiwa na Ujumbe wake, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Tanzania Mhe.Prof. Kitila Mkumbo (kulia kwa Rais) akiwa na Ujumbe wake walipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha, na (kushoto kwa Rais) Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa TUZO Maalumu ya Kupongeza “ Kwa kuendelea kuleta mageuzi ya kiuchumi kupitia Uchumi wa Buluu”, akikabidhiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Tanzania Mhe.Prof.Kitila Mkumbo,baada ya kumaliza mazungumzo na kujitambulisha alipofika Ikulu Jijini Zanzibar 


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiagana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Tanzania Mhe.Prof. Kitila Mkumbo, baada ya kumaliza mazungumzo na kujitambulisha alipofika Ikulu Jijini Zanzibar na Ujumbe wake, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar l






Saturday, August 5, 2023

UKAGUZI WA AFCON UMEENDA VYEMA – YAKUBU


 Na Eleuteri Mangi, WUSM, Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw Saidi Yakubu amesema timu ya Wakaguzi kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF) kwa maandalizi ya AFCON 2027 imemaliza ukaguzi wao vyema katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda kupitia kapeni ya EA Pamoja Bid.

Akiongea katika Kipindi cha Jambo kinachorushwa ya Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC) Agosti 5, 2023 jijini Dar es salaam, Katibu Mkuu Bw Yakubu amesema timu hiyo imemaliza kazi yao vizuri hapa ambapo ukaguzi wao ulianzia nchini Kenya, Uganda na Tanzania na kuhitimisha kazi yao kikao cha majumuisho kilichofanyika Zanzibar.


Maeneo mengine waliyokagua ni pamoja na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, HospitaIi ya Taifa Muhimbili, Uwanja wa Amaan Zanzibar, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Hospitali ya Mnazi Moja, Uwanja wa uwanja wa Mao Tse Tung Zanzibar pamoja na hoteli zitakazotumiwa wakati wa mashindano hayo kulingana na viwango vya CAF.


“Baada ya ziara yao hiyo Kenya, Uganda na Tanzania, walifanya mkutano wa majumuisho, Hatupo vibaya, tupo vizuri. Kinachotazamwa na wakaguzi ni pamoja na utayari wa Serikali namna ilivyojipanga katika kuhakikisha tukio hili tumelipokea, ukweli ni kwamba ziara yote hii ilikuwa inaongozwa Katibu Mkuu tayari inaonesha kwamba Serikali ipo tayari” amesema Katibu Mkuu Bw Yakubu.


Vigezo zingine ambavyo wakaguzi hao wa AFCON waliangalia ni mtiririko wa matukio kuelekea AFCON, kwa maana ya miundombinu ni lazima yote ikamilike kabla ya tarehe 31 Desemba 2025, Tanzania inajenga kiwanja kipya cha Arusha ambapo walioneshwa michoro, nyaraka zote muhimu na mapango wa mtiririko wa fedha utakavyokuwa katika kukamilisha ujenzi wa uwanja huo.

RATIBA YA LIGI KUU BARA.

Wakati wadau na mashabiki wa soka nchini wakisubiri kuanza kwa Ligi Kuu msimu wa 2023/24 bodi ya ligi hiyo nchini (TPLB) imesema ratiba ya mashindano hayo wataiachia siku mbili zijazo.

Ligi Kuu inatarajia kuanza Agosti 15, huku ikishuhudiwa baadhi ya timu zilizokuwapo msimu uliopita zikikosekana, huku zikitokea mpya tatu kwa michuano hiyo.

Timu za Mbeya City, Ruvu Shooting na Polisi Tanzania zilizokuwapo msimu huo, hazitakuwapo baada ya kushuka daraja, huku Tabora United, Mashujaa na JKT Tanzania zikichomoza msimu ujao.

Hadi sasa timu, mashabiki na wadau wa soka nchini wanasubiria kujua rariba inatoka lini ili kujua nani anaanza na nani na wapi ili kuanza mipango na mikakati rasmi.

Ofisa Habari wa bodi ya Ligi Kuu chini (TPLB), Karim Boimanda amesema hadi sasa ratiba imeshakamilika na muda wowote kuanzia kesho Jumapili au Jumatatu wataiachia rasmi.

Amesema wamechelewa kuitoa kutokana na shirikisho la soka Afrika (CAF) kuchelewesha kalenda yao huku akibainisha wameboresha na huenda changamoto za kusimamisha au kusogeza mechi zisijitokeze kama ilivyokuwa msimu uliopita. "Kuanzia kesho hadi Jumatatu ratiba itatoka rasmi kujua nani anaanza na nani na wapi, tumechelewa kutokana na kutopata mapema kalenda ya CAF, lakini tumezigatia ratiba ya michuano ya kimataifa hivyo zile changamoto za msimu uliopita hatutarajii kujitokeza"

"Ni ngumu ligi kukosa mapungufu kwa sababu kuna ratiba zinaweza kujitokeza za dharula, lakini sisi tumejitahidi kurekebisha kadri ya uwezo wetu ili kuondokana na hilo" amesema Boimanda.

Ofisa habari wa Tanzania Prisons, Jackson Mwafulango amesema wao wapo tayari kukutana na yeyote na popote kwani kikosi chao kipo fiti kwa ajili ya msimu ujao.

"Sisi hatuna presha wala wasiwasi tumejipanga kuanza na yeyote na popote, iwe nyumbani au ugenini, tupo kambini mazoezi yakiendelea tangu Julai 3," ametamba Mwafulango.

https://www.mwanaspoti.co.tz/ms/soka/ratiba-ligi-kuu-bara-hiyoooo-4327534



 

NAIBU WAZIRI: IJA NI CHUO MUHIMU KWENYE MAMBO YA HAKI.

 

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul amesema kuwa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto(IJA) ni Chuo muhimu katika kuwajenga watu wanaosimamia masuala ya haki hapa nchini.


Naibu Waziri Mhe. Pauline Gekul amesema hayo leo Jumamosi tarehe 05/08/2023 wakati akizungumza na wajumbe wa Menejimenti ya IJA, Halmashauri Tendaji ya Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu, Sayansi, Teknolojia, Habari na Utafiti (RAAWU) tawi la Lushoto pamoja na Watumishi wa Mahakama ya Wilaya ya Lushoto, hapa Chuoni wilayani Lushoto.


Amesema kuwa Chuo cha IJA kinapotoa maarifa kwa watu wa kada mbalimbali, basi kinasaidia katika masuala ya haki, akibainisha kuwa wananchi mbalimbali bado wanakabiliwa na ukosefu wa haki.


"IJA ni Chuo muhimu, nimefurahi kuona kumbe tuna Taasisi nzuri hapa," amesema Naibu Waziri na kuongeza,
"Sisi ambao tuna husika na wananchi moja kwa moja kama wabunge, madiwani na wenyeviti ni mashahidi kwamba wananchi wetu bado wana ukosefu wa haki zao hasa masuala ya kisheria, kwa hiyo nina imani ninyi mkiwapa maarifa watu wanaokuja kusoma hapa mnakuwa mnasaidia kwenye eneo la haki."


Pia Naibu Waziri huyo wa Katiba na Sheria ameongeza kuwa amejifunza masuala mengi ya Chuo cha IJA na kuhusu changamoto za Chuo Cha IJA, amebainisha kuwa atakwenda kuzifanyia kazi pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria na viongozi wengine.


"Mhe. Waziri wa Katiba na Sheria alikuja hapa akapokea changamoto zenu, nami niwaambie tutakwenda kuzifanyia kazi na kazi yetu sisi ni kuwa kiungo ili kuona mnafanya kazi vizuri," amebainisha Mhe. Naibu Waziri.


Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha IJA ambae pia ni Jaji wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Dkt. Paul F.Kihwelo amesema kuwa Chuo ni kitovu cha elimu na Utafiti kwa upande wa Mahakama na kwamba kimeendelea kuzalisha watu muhimu kwenye eneo la usimamizi wa haki.


Pia Mhe. Jaji Kihwelo amesema kuwa Chuo kimefarijika na ujio wa Naibu Waziri hapa Chuoni na kwamba ziara hiyo imekuwa na tija.


Awali katika ziara hiyo, Mhe. Naibu Waziri huyo wa Katiba na Sheria alitembelea maeneo kadhaa ya Chuo, ikiwemo Maktaba, Hosteli ya Wanaume ya Benjamini Mkapa pamoja na viwanja vya michezo vya Chuo.





MAJALIWA: MFUKO WA WATU WENYE ULEMAVU HAUJAUNGANISHWA NA MIFUKO MINGINE

 

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Mfuko wa Taifa kwa Watu wenye Ulemavu haujaunganishwa na mifuko mingine ya makundi maalum kama ambavyo inadaiwa.

“Katika risala yenu mmeomba Mfuko wa Taifa kwa Watu wenye Ulemavu usiunganishwe na mifuko mingine ili uweze kutekeleza majukumu yake yaliyoainishwa kwenye Sheria ya Watu wenye Ulemavu Na. 9 ya mwaka 2010. Nitumie fursa hii kuwafahamisha kuwa mfuko huo haujaunganishwa na mifuko mingine na kama mlivyosikia, mfuko huo umetengewa kiasi cha shilingi bilioni moja kwa ajili ya utekelezaji wa afua mbalimbali kwa watu wenye ulemavu,” amesema.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumamosi, Agosti 5, 2023) wakati akifungua kongamano la siku moja la watu wenye ulemavu Dar es Salaam lililofanyika kwenye ukumbi wa JNICC, jijini humo.

Alikuwa akijibu hoja kuu ya kwenye risala ilisomwa na Mwenyekiti wa SHIVYAWATA, Ernest Kimaya ambaye alitaka wapate majibu ya Serikali kuhusu hatua iliyofikiwa ya uanzishwaji wa Mfuko wa Maendeleo wa Watu wenye Ulemavu kwani wanaona ukiunganishwa na mifuko mingine, utasababisha masuala yao yafunikwe na kundi lao halitanufaika ipasavyo.

Hata hivyo, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuainisha changamoto zitakazowakabili kwenye matumizi ya fedha hizo endapo hawatajipanga kwa vile wana makundi mengi ambayo inabidi yaainishwe ili kila kundi liweze kunufaika na mfuko huo.

“Watu wenye ulemavu mna makundi mengi mno kama walivyo wasanii. Kuna wasanii wa muziki wa bongo fleva, orchestra, muziki laini, wa kufoka foka, bongo movie, wachoraji na wachongaji. Na hapa nimeona huo mchanganyiko. Mwenyekiti inabidi mkae na kuainisha haya makundi ili muweze kunufaika,” amesema.

Akitoa ufafanuzi kuhusu mkwamo wanaoupata watu wenye ulemavu katika maombi ya kazi kupitia utaratibu wa kidijitali wa Sekretarieti ya Ajira, Waziri Mkuu amesema Serikali inatambua uwepo ya changamoto hiyo na tayari imeweka utaratibu maalum kwa ajili ya watu wenye ulemavu.

“Waombaji wanatakiwa wawasilishe maombi kupitia Vyama vya Watu wenye Ulemavu ili wapate usaidizi kwa kuwa ofisi hizo tayari zina miundombinu rafiki kwa ajili ya watu wenye ulemavu. Mkurugenzi wa Idara, Kitengo cha watu wenye ulemavu upo hapa, simamia utaratibu huu ili kila nafasi za kazi zinapotangazwa wapelekee taarifa Vyama vya Watu wenye Ulemavu ili wapate usaidizi kwa wale wenye sifa zinazolingana na nafasi za ajira zilizotangazwa. Wekeni utaratibu mzuri wa kuwafikia ili nao wanufaike na fursa hizo.”

Akifafanua kuhusu ombi lao la kutaka kuharakishwa kwa utaratibu mpya wa kutoa na kurejesha mikopo inayotolewa na Halmashauri, Waziri Mkuu amesema Kamati ya Kitaifa iliyoundwa kuandaa utaratibu mpya wa usimamizi wa mikopo inayotokana na asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri kwa mfumo wa kibenki iko katika hatua za mwisho za maboresho ya taarifa yake. “Niwasihi sana mvute subira na pindi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI atakapotoa miongozo yake basi miongozo hii itagusa namna nzuri ya kurejesha mikopo hii.”

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na washiriki wa kongamano hilo, Naibu Waziri (OWM - Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu), Patrobas Katambi alisema Serikali imeanza kukusanya fedha za kufanya mapitio ya Sera ya Maendeleo na Huduma kwa Watu Wenye Ulemavu ya mwaka 2004.

“Sera hii ni ya mwaka 2004, ni takriban miaka 20 sasa. Tumeanza kutafuta fedha ili kuibadilisha sera hii badala ya kuboresha sheria kwa kutumia sera iliyopo. Ili upate sheria nzuri ni lazima uwe na sera nzuri. Tumedhamiria kwamba kutakuwa na ushirikishwaji wa makundi tofauti kulingana na ulemavu walionao kwa sababu kila kundi lina mahitaji tofauti.”

Alisema Serikali imetoa sh. milioni 35 kugharimia upatikanaji wa hati ya kiwanja katika eneo la Mtumba, jijini Dodoma kwa ajili ya kujenga Ofisi za Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu. Vilevile, Serikali kupitia Ofisi ya Rais - TAMISEMI inaendelea kuratibu upatikanaji wa ofisi za vyama vya watu wenye ulemavu kwenye Mikoa na Halmashauri zote nchini.

Naye Mwenyekiti wa Keysha Empowering Development Foundation (KEDEF) ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum (Walemavu), Khadija Shaban Taya alisema kongamano hilo ni la tatu na kwamba amekwishaandaa makongamano kama hayo kwenye mikoa ya Dodoma na Mwanza.

“Nia ya makongamano haya ni kuwaleta pamoja watu wenye ulemavu ili watoe maoni yao na kuelezea changamoto zinazowakabili. Pia, tutawapa elimu juu ya sheria ya manunuzi ambayo inataka asilimia 30 itengwe na Halmashauri zote ili zitumike kuendeleza shughuli za watu wenye ulemavu.”








MAGAZETI YA LEO AGOSTI 05, 2023.