Saturday, August 5, 2023
Friday, August 4, 2023
TBA YATAKIWA KUHAKIKISHA UBORA WA MAJENGO WANAYOJENGA ILI KUKIDHI MAHITAJI YA SOKO.
Makamu wa Rais amesema hayo mara baada ya kufungua Jengo la Makazi la Kibiashara la Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) lililopo katika eneo la Sekei Jijini Arusha, Jengo lililogharimu shilingi bilioni 6.86.
Amewahimiza TBA kuzingatia tija na viwango katika miradi mingine kama ilivyofanyika katika jengo hilo pamoja na kuwasihi kutekeleza kikamilifu Mpango Mkakati wa Wakala wa Majengo wa mwaka 2021/22 hadi 2025/26 ili kutimiza mahitaji ya makazi bora kwa Watumishi wa Umma na wananchi kwa ujumla. Amesema kukamilika kwa miradi mingi ya nyumba kutawezesha TBA kujiendesha kibiashara badala ya kutegemea ruzuku kutoka serikalini.
Halikadhalika Makamu wa Rais amewaagiza TBA kuhifadhi na kutunza mazingira kwa kupanda miti katika maeneo yote inapotekelezwa miradi ya ujenzi wa nyumba ikiwemo uwekaji wa miundombinu sahihi ya ukusanyaji takangumu ili kuwezesha ukusanyaji na utupaji wake.
Amesema kila inapowezekana TBA ihakikishe inaweka miundombinu ya kuvuna maji ya mvua kwa matumizi mbalimbali ikiwemo umwagiliaji wa miti na maua.
Makamu wa Rais ametoa rai kwa wapangaji wanaotumia nyumba hizo kuzingatia masharti ya mkataba wa upangishaji kwa kulipa kodi kwa wakati ili kuepukana na usumbufu unaoweza kujitokeza kutokana na teknolojia mpya ya uwekaji vitasa janja (Smart locks) ambavyo hujifunga pindi mpangaji anapofanya ulimbikizaji wa kodi. Pia amewasihi wapangaji kutunza nyumba hizo ili zibaki katika hali ya ubora kwa muda mrefu.
Vilevile Makamu wa Rais ametoa wito kwa sekta binafsi kuchangamkia fursa adhimu ya kushirikiana na TBA katika kutekeleza miradi ya ujenzi wa nyumba nchi nzima kwa kuwa Serikali tayari imeiruhusu TBA kushirikiana na Sekta binafsi katika utekelezaji wa miradi mbalimbali kwa ubia. Aidha amewasihi TBA kuendelea na mpango wa kuyaendeleza maeneo yote yaliyorejeshwa Serikalini kwa kujenga majengo ya ghorofa kama ilivyoelekezwa kwenye Ibara ya 55(h)(ii) ya Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya 2020.
Makamu wa Rais amewaasa wananchi wa mkoa wa Arusha kutunza mazingira kwa kuepukana na tabia ya kutupa taka ovyo kwani jambo hilo litaleta athari katika masuala ya utalii mkoani humo.
Amewaagiza viongozi wa mkoa huo kusimamia suala hilo kwa kuhakikisha usafi unafanyika katika maeneo yote na kudhibiti utupaji taka ovyo hususani chupa za maji.
Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa ameishukuru serikali kwa kuendelea kuiamini Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi inayotekeleza miradi mbalimbali ikiwemo miradi ya ujenzi wa nyumba na majengo ya serikali katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Prof Mbarawa amesema kukamilika kwa ujenzi wa mradi huo kutasaidia upatikanaji wa makazi ya uhakika kwa wakazi wa jiji la Arusha. Ameongeza kwamba mradi huo umesaidia wataalamu wazawa wa fani za ujenzi kujengewa uwezo wa taaluma kwa vitendo pamoja na kusaidia kuendelea kukua kwa kasi kwa jiji la Arusha, kuongezeka kwa mapato ya serikali pamoja na huduma za kijamii katika jiji hilo.
Awali akitoa taarifa kuhusu mradi huo Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Arch. Daud Kondoro amesema Chimbuko la mradi huo ni katika kuiwezesha Wakala kuwa na uwezo wa kujiendesha kupitia vyanzo vyake vya mapato na kupunguza utegemezi kwa Serikali. Ameongeza kwamba mapato yatakayopatikana kwenye miradi kama hiyo yatatumika kujenga nyumba nyingine za watumishi wa umma.
Arch. Kondoro ameongeza kwamba pamoja na mradi huo, Wakala wa Majengo Tanzania unaendelea kutekeleza miradi mingine kwa fedha za ndani ikiwemo Ujenzi wa Majengo ya Makazi eneo la Canadian Village, Masaki, Dar es Salaam ambapo jengo moja lenye uwezo wa kuchukua familia 12 limekamilika na majengo mengine mawili utekelezaji wake umefika asimilia 35. Wakala pia umeanza ujenzi wa Jengo la Makazi eneo la Ghana Kota jijini Mwanza ambalo utekelezaji wake umefikia asilimia 12.
Ujenzi wa Jengo hilo lenye uwezo wa kuhudumia familia 22 umeleta faida mbalimbali ikiwemo kutoa ajira kwa wataalam wa ujenzi, mafundi, vibarua, baba na mama lishe ambapo ajira zipatazo 171 zilipatikana hadi kukamilika kwa mradi huo. Mradhi huo unatarajia Kuongeza mapato ya ndani kwa Wakala kupitia kodi ya pango itakayokusanywa kwa makadirio ya Shilingi milioni mia mbili na kumi (210,000,000.00) kwa mwaka.
IMETOLEWA NA
OFISI YA MAKAMU WA RAIS
04 AGOSTI 2023
Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akikata utepe kuashiria Ufunguzi wa Jengo la Makazi la Kibiashara la Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) lililopo katika eneo la Sekei Jijini Arusha leo tarehe 04 Agosti 2023.
Wengine katika picha ni Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof Makame Mbarawa, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula, Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela, Mtendaji Mkuu wa TBA Arch. Daud Kondoro pamoja na wawakilishi wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof Makame Mbarawa pamoja Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula katika sebule ya moja ya nyumba iliopo katika Jengo la Makazi la Kibiashara la Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) lililopo katika eneo la Sekei Jijini Arusha mara baada ya kufungua jengo hilo leo tarehe 04 Agosti 2023.
SITA WAKAMATWA KWA HLKUHIFADHI WAHALIFU SAME
Watu Sita wanashikiliwa na Polisi wakituhumiwa kuwaficha kwa kuwahifadhi wahalifu walioingia kinyemela na kujihusisha na uchimbaji wa madini eneo ambalo ni chanzo tegemeo cha Maji kwa wakazi zaidi ya 22,000 wa kata nne za Vudee,Mwembe,Mhezi na Mbangalala Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro.
Kukamatwa kwa watuhumiwa hao Sita ni matokeo ya Oparesheni ya kamati ya Usalama Wilaya ya Same iliyo ongozwa na mwenyekiti wake ambae ni mkuu wa Wilaya Kasilda Mgeni, waliolazimika kufanya msako kwa kushtukiza baada ya kupata taarifa za kuwepo watu zaidi ya 70 wanaoendesha shughuli za uchimbaji madini Aina ya Dhahabu bila vibali.
Kwa mujibu wa mkuu wa Wilaya ya Same taarifa zilizo mfikia ni kwamba mbali na wachimbaji hao kufanya shughuli zao kinyemela, pia wameharibu miundombinu ya Maji na kuhatarisha Usalama wa watumiaji kwakua wanasafisha madini moja Kwa moja kwenye Bwawa wakitumia Mercury ambayo ni hatari kwa binadamu.
“Kuingia huku kinyemela na kuharibu miundombinu ya Maji NI hujuma, hatutavumilia vitendo kama hivi, niwatake Jeshi la Polisi kuweka kambi kwenye eneo hili kuimarisha ulinzi kuhakikisha shughuli za uchimbaji zinakoma na waliohusika kuihujumu Serikali lazima watafute popote na wachukuliwe hatua”.Alisema Kasilda Mgeni mkuu wa wilaya ya Same.
Awali kaimu Afisa Mtendaji wa kijiji cha Mteke Felix Ngeti amesema kwa sasa asilimia kubwa ya watu wamelazimika kuacha kutumia Maji hayo kwakua Uharibifu ni mkubwa na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi kulazimika kutafuta huduma ya majinsafi maeneo ya mbali.
"Hapa mnapoona kuna wachimbaji zaidi ya sabini na viongozi wa kijiji walikuja baada ya kupata malalamiko kwa wananchi juu ya uchaguzi unaofanyika lakini wachimbaji hao kwakua waliokua wengi waliwafukuza viongozi”.Alisema Ngeti.
Baadhi yao wakazi wanaoishi jirani na eneo hilo kulikofanyika Uharibifu wamepongeza hatua za haraka zilizochukuliwa na kamati ya Usalama, wakisema Hali ilizidi kuwa mbaya kwakua kumekua na ongezeko la idadi ya watu wanaotoka maeneo mbalimbali na kuingia kinyemela katika eneo hilo la chanzo cha Maji na kuanza uchimbaji wa madini.
SAHANI YA MLO UNAOFAA.
Sahani ya Mlo Unaofaa.
Sahani ya Mlo unaofaa, ambayo imebuniwa na wataalamu wa lishe kutoka Chuo Kikuu cha Afya ya Jamii, Harvard na kuhaririwa na wataalamu kutoka Harvard, ni muongozo wa mlo kamili unaofaa kwa afya-ikiwa utatumiwa kwenye sahani ya mlo ama kama chakula cha kufunga kwenye box. Bandika nakala kwenye fridge au kabati ili ikukumbushe kuandaa mlo kamili wenye afya!
- Sehemu kubwa ya mlo wako uwe mbogamboga na matunda – ½ ya sahani
Hakikisha unaweka aina mbalimbali zenye rangi tofauti. Viazi mbatata havihesabiwi kama mbogamboga katika Sahani ya Mlo unaofaaa kwa sababu ya madhara yake kwenye kiwango cha sukari mwilini.
- Tumia vyakula vya nafaka isiyokobolewa – ¼ ya sahani
Vyakula vinavyotokana na nafaka isiyokobolewa kama vile ulezi, mtama, mchele wa brown vinaathari kidogo katika kiwango cha sukari mwilini na utengenezaji wa insulini kuliko vyakula vinavyotokana na nafaka iliyokobolewa.
- Nguvu itokanayo na protini – ¼ ya sahani
Samaki, Kuku, maharagwe, njugu, vyote ni vyakula vinavyoleta afya kutokana na protini-vinaweza kuchanganywa na kachumbari, na pia kwenye Sahani ya Mlo Unaofaa vinafaa kuchanganywa na mbogamboga. Punguza matumizi ya nyama nyekundu and epuka nyama za kusindikwa kama beconi na soseji.
- Mafuta yatokanayo na mimea kwa kiasi
Chagua mafuta yanayofaa ambayo yanatokana na mimea kama vile mizeituni, soya, mahindi, alizeti, karanga na mengineyo na epuka kutumia mafuta ambayo yameganda. Kumbuka kuwa alama ya “low-fat” kwenye makopo ya mafuta haimaanishi “mafuta yafaayo kwa afya”
- Kunywa maji, kahawa au chai
Epuka vinywaji vyenye sukari, punguza matumizi ya maziwa na vyakula vitokanavyo na maziwa mpaka mara moja au mbili kwa siku, punguza matumizi ya juisi mpaka glass ndogo moja kwa siku.
- Shughulisha mwili
Picha nyekundu ya mtu anayekimbia kwenye Sahani ya Mlo Unaofaa inakumbusha kuwa, kuweka mwili katika hali ya mazoezi ni muhimu pia katika kupunguza uzito.
Ujumbe muhimu wa Sahani ya Mlo Unaofaa ni kusisitiza kuhusu Aina ya Mlo unaofaa
- Aina ya wanga kwenye mlo ni muhimu zaidi kuliko kiwango cha wanga kwenye mlo, kwa sababu baadhi ya vyakula vya wanga mfano mbogamboga, matunda, nafaka zisizokobolewa na maharagwe vina manufaa kiafya kuliko zingine.
- Sahani ya Mlo unaofaa pia inashauri watumiaji kuepuka vinywaji vyenye sukari, ambavyo ni chanzo kikubwa cha kalori kwenye mwili, wakati vikiwa na faida ndogo kiafya.
- Sahani ya Mlo unaofaa inasisitiza utumiaji wa mafuta ya kupikia yatokanayo na mimea na haijamuwekea mtu kiwango cha juu cha asilimia ya kalori kutoka kwenye mafuta yanayofaa.
Thursday, August 3, 2023
WAZIRI KIJAJI:ATAKAYEUZA SUKARI ZAIDI YA 3200 ACHUKULIWE HATUA
Waziri Kijaji ameyasema hayo alipotembelea Kiwanda cha kuzalisha Sukari cha TPC Mkoani Kilimanjaro kujionea shughuli za uzalishaji na kisikiliza changamoto walizonazo.
Dkt. Kijaji amesema ni jukumu la Maafisa Biashara kutambua mfanyabiashara yeyote atakayeuza sukari juu ya bei kati ya 2800 na 3200 kumchukulia hatua.
Dkt. Kijaji amesisitiza kiwa ni jukumu la Serikali kulinda bidhaa yoyote inayotengenezwa nchini na kufanya Juhudi za kila namna ili kuweza kuwasaidia wawekezaji na wafanyabiashara kuwa na mazingira bora na wezeshi ili kukuza biashara zao na kiwa na tija.
Aidha, amesema bidhaa zinazotengenezwa nchinj zinatakiwa kuwanufaisha wawekezaji na wafanyabiashara wa ndani na biashara yoyotee inayofanyika nje ya nchi inatakiwa kuwa rasmi.
Vilevile amekipongeza Kiwanda cha kuzalisha Sukari cha TPC kwa kutoa ajira zaidi ya elfu 3200 na jinsi kinavojihusisha na utoaji wa huduma kwa jamii inayokizunguka
Naye Kaimu Afisa Mtendaji Utawala wa Kiwanda cha TPC, David Shiltu amesihi watanzania kuwa na Amani kwa kuwa sukari ipo sokoni ya kutosha na hakuna uhaba na uzalishaji unaendelea.
QS KIPANGA AONGOZA FALSAFA YA RAIS SAMIA KATIKA KUSIMAMIA WAWEKEZAJI NA UWEKEZAJI WENYE TIJA NA TAIFA
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknologia Mhe Qs Omar Kipanga ameongoza watalaamu mbalimbali kutoka Tanzania katika Mkutano maalumu wa uwekezaji na uwezeshaji uliofanyika Kigali Rwanda Leo 03.08.2023.
Akiziungumza mara baada ya kikao hicho kilichohudhuriwa na wawakilisho wa Tasisi mbalimbali nchini Rwanda kutoka nchi za afrika Mashariki,Ulaya na Asia,
Aidha katika kikao hicho Mhe Qs Omar Kipanga alisema amepokea ujumba maluum kutoka kwa Mhe Rais Samia kuhusu Mazingira Mazuri na salama yenye kuwarahisishia wawekezaji ambao wapo Tayari kuwekeza Tanzania,
*"Serikali ya Awamu ya Sita Rais Dkt Samia na Chama chetu Cha Mapinduzi CCM kimeweka Mazingira rafiki kwa mtu,tasisi ama shirika lolote linalotaka kuwekeza Tanzania basi mje maana tuna Kila kitu ambacho mnakihitaji kwa ajili ya faida ya Taifa alimalizia Mhe Qs Kipanga*"
*"Kwa sasa Tanzania imeamua kuwekeza zaidi kwa faida ya Watanzania wa kizazi Cha Sasa na Baadae Hivyo kwa makusu tumeamua kuwafata na kuwambia kuwa tumeweka Mazingira salama kwa Kila mwekezaji nyanja yoyote Ile muhimu inufaishe taifa na iwe kwa maslah ya taifa alisisitiza Mhe Qs Kipanga*"
*"Tunategea Kutoa fursa za uwezeshaji wenye tija kwa yoyote katika Elimu Sayansi na Teknologia, Utalii, Biashara,Kilimo kikubwa, Uvuvi,Uvumbuzi na Utafiti,Nk Muhimu Kila mmoja anaetaka awe anajua Wazi anakuja Kutoa faida kwa taifa bila ya kuleta matatizo muhimu ajipange alisisitiza Mhe Qs Kipanga"*
Mkutano huo umejumuisha wawekezaji kutoka mataifa ya Israel, Romania, Smart Afrika,na Bank ya Dunia.
DKT. BITEKO ATETA NA KAMPUNI YA SOTTA MINING DODOMA
Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko leo Agosti 3, 2023 jijini Dodoma amekutana na Uongozi wa Juu wa Kampuni ya Sotta Minerals Corporation Limited ambayo ni ya ubia Kati ya Serikali na kampuni ya Orecorp Tanzania limited ya Australia inayosimamia Mradi wa uchimbaji madini ya dhahabu uliopo wilayani Sengerema Mkoani Mwanza.
Kupitia Mkutano huo, kampuni ya Sotta imeeleza maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo ambao unatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwaka 2025.
Aidha, Dkt. Biteko ameelezwa kuwa, hivi sasa kampuni iko kwenye hatua za mwisho za kuweza kuwalipa fidia wananchi walio ndani ya eneo la mradi ili kuwezesha mradi huo kuanza.
CHANGAMKIENI FURSA ZA UFUGAJI WA MAJONGOO BAHARI.
Na Nurdin Ndimbe, Morogoro.
Wananchi wameshauriwa kuchangamkia fursa zilipo katika Halmashauri ya Wilaya
Bagamoyo katika ufugaji wa majongoo Bahari ili kujiongezea kipato pamoja na
kupunguza changomoto za ajira.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkuu wa Sehemu ya Uvuvi katika Divesheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo Bw Kiboko Kiondo Godson, wakati akizungumza na wananchi waliotembelea banda la Halmashauri ya Bagamoyo katika maonesho ya Wakulima Nanenane yanayoendelea Manispaa ya Morogoro, leo tarehe 3 Agosti, 2023.
Aliwafahamisha wananchi hawo kuwa, kilimo cha majongoo bahari hufanyika
kwa kutengeneza vizimba baharini vyenye ukubwa mita za mraba kuannzia 40 na
kuendelea ambapo majongoo hufugwa na kuanza kuvunwa kuanzia miezi sita na
kuendelea.
Kilimo hiki kwa sasa kina faida kubwa sana kwani mahitaji ni makubwa kuliko uzalishaji, mathalani kilo moja ya majongoo yaliyokaushwa kwa bei ya soko ni
si chini Ths 180,000/-. “Tuna mahitaji makubwa sana kuliko uwezo wetu hivyo
nawasihii wananchi kuchanagamkia fursa za ufugaji wa majongoo na viumbe bahari
, na soko kubwa lipo hasa Asia hasa wenzetu kule China”. Alisistiza Bw Kiondo.
Aidha alieleza mikakati ya Halmashauri ya Bagamoyo katika kuwawezesha
wananchi kuanza ufuguaji wa majongo bahari ni pamoja na kuwaelimisha wananchi namna bora ya ufugaji wa majongoo pampja na kuwahamasiha kuunda vikundi vya ufugaji wa majongoo bahari kwani kwa sasa kuna vikundi vitatu tu
vinavyojishughulisha na ufugaji huu.
Kasi ya kuunda vikundi bado ni ndogo.
tunawashauri waanzishe fursa zipo na kubwa kwani ufugaji wa majongoo hauna
gharama kubwa unaweza kufuga wakati ukiendelea na sguhuli zingine”. Alisisitiza.
Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo ni moja ya Halmashauri inayozalisha majongoo bahari kama zao la biashara na kwa Mwaka wa fedha 2022/2023 zaidi ya tani 1,200 ziliuzwa nje ya Nchi hasa Uchina.
Kauli mbiu ya Maonesho wa Wakulima Nanenane 2023 ni “ Vijana na Wanawake ni msingi imara wa mifumo endelevu ya chakula.

















































