Sunday, November 17, 2019

ADC YAGOMA KUFUATA MKUMBO...YASEMA WATASHIRIKI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2019

Katibu Mkuu wa Chama cha ADC  Doyo Hassan Doyo akizungumza na waandishi wa habari katika makao mkuu ya chama hicho Buguruni jijini Dar es salaam wakati alipotangaza msimamo wa chama hicho kushiriki uchaguzi wa serikali ya mtaa, amesema chama hicho kitashiriki uchaguzi, Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa ADC Bi. Queen Sendiga.


Chama cha Alliance For Democratic Change’ (ADC) kimetangaza kushuriki katika uchaguzi wa serikali wa mitaa wakisisitiza kuwa hawaoni sababu ya kutoshiriki huku kuna wagombea wao ambao wamepitishwa katika uchaguzi huo.
Akizungumza na Waandishi wa Katibu Mkuu wa chama hicho, Doyo Hassan Doyo amesema Chama chao kitashiriki uchaguzi huo licha ya ‘figisu figisu’ zilizojitokeza zilizosababisha baadhi ya wagombea wake kukosa kuenguliwa huku akikiri kuwa baadhi yao ‘walijichanganya’ katika mchakato wa ujazaji fomu za uteuzi.
Tunao wagombea wetu ambao wamepitishwakugombeamaeneo mbalimbali, kujitoa katika uchaguzi huu ni kuwanyima haki ya wananchi ya kuchagua viongozi wanaowataka, lakini pia kuwanyima wanachama wetu haki ya kugombea. Ndiyo maana tunagombea.

SERIKALI YASISITIZA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA 2019 UKO PALEPALE


Katibu Mkuu wa Wizara ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Joseph Nyamuhanga akizungumza na waandishi wa habari leo wakati walipotangaza msimamo wa serikali kuhusu uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vitongoji na Vijiji ambapo Kampeni zinatarajiwa kuwanza kesho.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Joseph Nyamuhanga alipokuwa akizungumza nao leo ofisini kwake jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu wa Chama cha Alliance For Democratic Change ADC Bw. Doyo Hassan Doyo akizungumza na waandishi wa habari katika makao mkuu ya chama hicho Buguruni jijini Dar es salaam wakati alipotangaza msimamo wa chama hicho kushiriki uchaguzi huo amesema chama hicho kinashiriki kikamilifu, Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa ADC Bi. Queen Sendiga.
Katibu Mkuu wa Chama cha Alliance For Democratic Change ADC Bw. Doyo Hassan Doyo Naibu Katibu Mkuu wa ADC Bi. Queen Sendiga wakiwa katika picha ya pamoja na wagombea wao wanaoshiriki katika nyazifa mbalimbali za uchaguzi huo.
Naibu Katibu Mkuu wa ADC Bi. Queen Sendiga akizungumza na kusisitiza jambo katika mkutano huo.
Baadhi ya wagombea wa chama cha Chama cha ‘Alliance For Africa Farmers Party’ (AAFP) wameenguliwa katika uchagzui huo kwa makosa mbalimbali ya kikanuni na kisheria..
Katibu Mkuu wa AAFP Rashid Rai akizungumzzia kuhusu makosa mbaimbali ambayo wagombe wa chama chake walifanya na kisha kuengeuliwa kikanuni na wasimamizi wa uchaguzi.
Katibu Mkuu wa AAFP Rashid Rai akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu yao yaliyopo Tandika wilayani Temeke jijini Dar es salaam.
……………………………………………………….
SERIKALI imeweka wazi kwamba uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajia kufanyika Novemba 24 mwaka 2019 uko pale pale huku ikitangaza kuanza rasmi kwa kampeni za uchaguzi huo zikitarajiwa kuanza kesho. 
Hivyo vyama vyote ambavyo vitashiriki uchaguzi huo zimetakiwa kupeleka ratiba ya mikutano yao ya kampeni kwa wakuu wa Polisi wa Wilaya kwa lengo la kupatiwa ulinzi kuhakikisha kampeni hizo zinakuwa salama na wagombea kupata fursa ya kujinadi kwa wapiga kura.
Wakati Serikali ikitoa msimamo huo baadhi ya  vyama kadhaa vya upinzani kikiwemo Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) Chama cha Wananchi(CUF) ,Chama cha ACT Wazalendo , Chama cha Chauma na NCCR Mageuzi wao walishatangaza kujitokea ,huku Chama Cha Mapinduzi(CCM) na vyama kadhaa vya upinzani vimetangaza kutoshiriki.
Akizungumza leo Novemba 16,mwaka 2019 Katibu Mkuu  wa Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Joseph Nyamuhanga amesisitiza uchaguzi huo utafanyika kama ambavyo imepangwa na kampeni itaanza kesho nchini na kila kitu kiko sawa.
Amefafanua kuwa kwamba Watanzania waajiandae kusikiliza mikutano ya kampeni ya vyama vya siasa na kisha Novemba 24 wakachague viongozi wao .Tunaomba vyama ambavyo vitashiriki kujiandaa na kampeni ambazo zinaanza kesho( leo) , ushauri wetu kwa vyama hivyo ni kupeleka ratiba ya mikutano yao ya kampeni za uchaguzi huu kwa wakuu wa polisi wa wilaya ili wapatiwe ulinzi,”alisema.
Kuhusu kampeni za uchagzi huo, ameeleza kuwa baada ya kuanza kesho,zitahitimishwa Novemba 23 mwaka huu ambayo itakuwa siku moja kabla ya upigaji wa kura kwa vyama vyote ambavyo vimebakia katika uchaguzi huo.Amesisitiza hakuna sababu ya uchaguzi huo kuusogeza mbele wala kuuahirisha.
Ameongeza kuwa kampeni  za uchaguzi huo zinazoanza kesho zitafanyika katika maeneo yenye wagombea pekee na kuyaacha maeneo ambayo wagombea wake wamejitoa au kupita bila kupingwa jambo ambalo pia limevifanya vituo vya uchaguzi kupungua kwa kiwango fulani kutoka vituo 1,10000.
Nyamuhanga amesema  kwa ujumla wagombea waliopita bila kupingwa katika mchakato wa uchaguzi huo nchi nzima ni 1,2319 sawa na asilimia 55 ya wagombea wote waliokuwa wamejitokeza kuomba kuteuliwa huku akitoa msisitizo kwa vyama vyote kufanya kampeni za kistaarabu.
Amesisitiza kuwa Wasimamizi wa uchaguzi, askari Polisi, mgambo wote wanapaswa kuwa katika sare kipindi chote cha kampeni  hadi uchaguzi utakapofanyika ili kuondoa mkanganyiko wowote unaoweza kujitokeza huku akitoa onyo kwa vyama hivyo  na kuvitaka kuacha kutumia vikundi vya sungusungu na vinginevyo na kwamba sheria itachukua mkondo wake pale ambapo agizo hilo utekelezaji wake utakiukwa.
Katibu Mkuu Nyamuhanga amesema maandalizi ya uchaguzi huo yameshakamilika ikiwemo wino maalumu utakapakwa kidoleni mara baada ya kupiga kura pamoja na rakiri itakayotumika kufungia masanduku mara baada ya kuhitimishwa kwa zoezi la kupiga kura.
 Wakati Serikali ikisisitiza kufanya uchaguzi huo, vyama vya ‘Alliance For Democratic Change’ (ADC) pamoja na Chama cha ‘Alliance For Africa Farmers Party’ (AAFP) vimetangaza kushiriki uchaguzi huo kwa kudai havioni sababu yoyote ya wao kujitoa.
Hatua hiyo imekuja siku moja baada ya Vyama vya Tanzania Labour Party(TLP) na chama cha National Reconstruction Party (NRA) kutangaza kushiriki mchakato wa uchaguzi huo kama ilivyopangwa vikidai kuwa kufanya hivyo ni kuitendea haki demokrasia iliyopo nchini.
Kwa upande wa Katibu Mkuu wa ADC, Doyo Hassan Doyo amesema Chama chao kitashiriki uchaguzi huo licha ya ‘figisu figisu’ zilizojitokeza zilizosababisha baadhi ya wagombea wake kukosa kuenguliwa huku akikiri kuwa baadhi yao ‘walijichanganya’ katika mchakato wa ujazaji fomu za uteuzi.
Amesema ni kweli wapo waliofanya makosa ya aina mbalimbali katika ujazaji fomu hatua iliyosababisha kukiuka kanuni,  kilichosababisha hayo kutokea hatuwezi kukilaumu kwa kuwa mengine yalitokana na uzembe wao kwa  kutowapa elimu wagombea wao kabla ya kuzijaza fomu hizo.
 Wakati  Katibu Mkuu wa AAFP Rashid Rai, pamoja na kusisitiza kushiriki katika uchaguzi huo, amesema  changamoto iliyojitokeza katika chama chake na kusababisha wagombea wake kuenguliwa ni kukiuka kanuni katika ujazaji fomu.
Hata hivyo amesema licha ya kujitokeza kwa changamoto mbalimbali wao bado watashiriki katika uchaguzi huo kwa kuwa bado wanao wagombea katika baadhi ya maeneo nchini.’Kwetu  hata tukipata mtaa mmoja ni ushindi wa zaidi ya asilimia hamsini, haijarishi wenzetu wameshinda viti vingapi,”ameongeza.
Uchaguzi huo wa Serikali za Mitaa ulioanza Oktoba mwaka huu  kwa mchakato wa uandikishaji wapiga kura na baadae uchukuaji fomu, urejeshaji wa fomu, ukataji rufaa na sasa.kuanza kwa kampeni ambazo zitahimitishwa kwa kufanyika uchaguzi huo Novemba 24 kwa wananchi kupiga kura kuwachagua viongozi wanaowataka.

Friday, November 15, 2019

WANANCHI KISARAWE WAFURAHIA ELIMU YA KODI TOKA TRA.

Na Shushu Joel.

WANANCHI wa wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani wamefurahishwa na huduma ya elimu kwa mlipa kodi inayotolewa na mamlaka ya mapato nchini (TRA).

Wakizungumza mara baada ya kutembelewa na wahudumu kutoka TRA walisema kuwa elimu imekuwa kubwa na yenye mashiko kwa wafanyabiashara.

James Joackim ni mmoja wa wafanyabiashara wa muda mrefu katika wilaya hiyo anasema kuwa tangu aanze biashara kipindi hiki amefurahishwa na huduma zinazotolewa na mamlaka hiyo kwa jinsi wanavyojitoa kuwaelimisha wafanyabiasha.

"Miaka ya nyuma ilikuwa ukiwaona watu kutoka TRA unakuwa kama umewaona polisi hata ilifikia hatua ya kuwaona watu wa mapato unafunga duka lakini kipindi hiki ni raha sana"Alisema Joackim.

Aidha aliongeza kuwa elimu hii iendelee kutolewa mara kwa mara ili wafanyabiasha waweze kupata elimu zaidi.

Kwa upande wake Bi' Mariam Mbaga ameishukuru mamlaka ya mapato kwa kuelimisha juu ya utoaji wa risiti kwa wateja.

Pia amesema kuwa amewataka wafanyabiashara kujitokeza kwa wingi katika zoezi linalofanywa na mamlaka ya mapato kwani elimu ni nzuri sana hivyo ukikosa elimu hii utajutia sana.

Naye Mkurugenzi wa huduma ya elimu kwa walipa kodi Richard Kayombo alisema kuwa mamalaka ya mapato nchini imeamua kuwafuata wananchi katika mkoa wa Pwani na Morogoro kwa madhumuni ya kuwaelimisha na kuwasaidia kutatua changamoto zao.

"Kampeni hii ya kuwaelimisha wananchi juu ya ulipaji wa kodi kwa hiyari ni endelevu na litafika kila mkoa kwa lengo la kuwasaidia wafanyabiashara na wananchi juu ya malipo ya kodi" Alisema Kayombo.

Aliongeza kuwa sio kila mtu anatakiwa alipe kodi hivyo ni muhimu sana kuwasikiliza watoa huduma kutoka TRA ili waweze kukuelimisha juu ya nani anastahili kulipa au kutokulipa.

Aidha Kayombo aliongeza kuwa dhamira ya mamlaka ni kuwaelimisha wananchi juu ya upataji wa namba ya utambulisho kwa mlipa kodi (TIN) na uchukuaji wa risiti kwa wanunuzi ni jambo la muhimu sana.

Akitoa ufafanuzi juu ya faida za kulipa kodi mkurugenzi huyo wa huduma ya elimu kwa walipa kodi alisema kuwa miradi yote inayotekelezwa kwa pesa za ndani ni matokeo ya ulipaji kodi.

Amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika zoezi la ulipaji kodi za majengo, biashara na kodi zjngine ili kuisaidia serikali katika ufanikishaji wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa wingi.

ASILIMIA 80 YA FAMILIA LINDI ZAHUDUMIWA NA WANAWAKE.

 Ofisa mradi wa Taasisi ya ukuwaji kwa usawa wa maendeleo Tanzania EQUALLY FOR GRWTH (EFG) kupitia mpango wa sauti ya mwanamke Sokoni Suzan Sitta Kulia akimkabidhi mstahiki meya wa Manispaa ya Lindi Mohamedi Lihumbo Lidume kushoto taarifa ya mradi wao walipofanya zihara ya Mafunzo katika Manispaa hiyo jana

PICHA NA HADIJA HASSAN.
......................................................


Na Hadija Hassan, Lindi.

Imeelezwa kuwa Zaidi ya asilimia 80 ya Familia za Manispaa ya Lindi Mkoani humo zinaendeshwa kwa kipato cha akina Mama huku akina baba wakiishia vijiwe vya kahawa na bao.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Jomary Satura alipokuwa anazungumza na viongozi mbali mbali wa Mradi wa mwanamke sokoni (EQUALLY FOR GRWTH) walipofanya ziara ya mafunzo katika Manispaa hiyo.

Alisema asilimia 80% ya majukumu na malezi ya familia kwa Wanandoa wa Mkoa wa Lindi hufanywa na kina mama huku kina baba hufanya kwa asilimia 20% pekee.

Jomari alisema ni jambo la kawaida kwa kina baba wa ukanda huo kwenda kukaa katika vibanda vya kahawa ama kucheza bao huku kina mama ndio wakibaki na majukumu ya kutafuta riziki na baadae kuendesha familia za nyumba zao.

Nae ofisa maendeleo wa Manispaa hiyo Judica Sumary amekili kuwepo kwa changamoto hiyo huku akieleza kuwa hali ya kina mama hao kuwa ndio waendeshaji wa familia huchangia kwa kiasi kikubwa kushindwa kurejesha kwa wakati kwa mikopo inayotolewa na Halmashauri.


"Hali hii inatokana na uchache wa watu katika Manispaa hii ambapo hufanya mzunguuko wa biashara kuwa mdogo hivyo kulingana na majukumu ya kifamilia mam huyo hujikuta kiasi kidogo alichonacho hutumia katika majukumu ya kifamilia na baadae kushindwa kufanya marejesho ya Mkopo aliochukuwa".

Awali akitoa taarifa ya mradi wa Sauti ya mwanamke Sokoni ofisa mradi wa (EQUALLY FOR GROWTH) Suzan Sitta alisema kuwa Lengo kubwa la kufika katika Manspaa hiyo ni kuwahamasisha wanawake wafanya biashara kujiunga na Umoja wa wanawake sokoni wa kimataifa.

Alisema lengo lingine la mpango huo ni kumkomboa mwanamke mfanya biashara kwa kumjengea uwezo wa kutambua yeye ni nani na nafasi yake kama raia huru katika kuendesha biashara na shughuli za soko.

Hata hivyo alieleza kuwa katika mpango wa mradi huo zaidi ya wanawake Wafanya biashara 1,000 katika masoko watanufaika na mradi katika maswala ya kukuza biashara, VICOBA, haki za wanawake , ushiriki wa wanawake katika uongozi pamoja na kujiunga katika umoja wa wanawake sokoni.

JESHI LA POLISI LAWATAKA WAGOMBEA SERIKALI ZA MITAA KUZINGATIA SHERIA.