Wednesday, October 9, 2019

MAREKANI YASAINI MKATABA WA DOLA MILIONI 10 NA AMANA BANK TANZANIA

 Msimamizi Msaidizi wa USAID kwa Ofisi ya Afrika, Dkt. Diana B. Putman (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Amana Bank, Dkt. Muhsin Salim Masoud, wakitabasamu pamoja na kupeana mikono baada ya kusaini makubaliano mapya ya Mamlaka ya Mkopo wa Maendeleo (DCA) jijini Dar es salaam Oktoba 7, 2019.

Serikali ya Marekani, kupitia Wakala wa Maendeleo ya Kimataifa (USAID), imesaini Mkataba wa Dhamana ya Dola milioni 10 na Amana Bank.

Lengo la DCA ni kuimarisha uwezo wa benki kutoa fedha kwa biashara zinazohusiana na ndogondogo, kilimo na biashara za kati na wanawake, pamoja na biashara zinazomilikiwa na vijana nchini Tanzania. (Picha na USAID).

Msimamizi Msaidizi wa USAID kwa Ofisi ya Afrika, Dkt. Diana B. Putman (wa pili kutoka kulia waliokaa) na Mkurugenzi Mtendaji wa Amana Bank, Dkt. Muhsin Salim Masoud (wa pili kutoka kulia waliokaa) wakisaini makubaliano mapya ya Mamlaka ya Mkopo wa Maendeleo (DCA) na Benki ya Amana jijini Dar es salaam Okotoba 07, 2019.


Serikali ya Marekani, kupitia Wakala wa Maendeleo ya Kimataifa (USAID), imesaini Mkataba wa Dhamana ya Dola milioni 10 na Amana Bank.

Lengo la DCA ni kuimarisha uwezo wa benki kutoa fedha kwa biashara zinazohusiana na ndogondogo, kilimo na biashara za kati na wanawake, pamoja na biashara zinazomilikiwa na vijana nchini Tanzania. (Picha na USAID).
Mkurugenzi wa Misheni ya USAID / Tanzania Andrew Karas (2 kutoka kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Amana, Dkt. Muhsin Salim Masoud (3 kutoka kulia) akizungumza na waandishi wa habari baada ya hafla ya utiaji saini wa makubaliano ya Mamlaka ya Mikopo ya Maendeleo (DCA) jijini Dar es salaam Oktoba 07, 2019.


Serikali ya Marekani, kupitia Wakala wa Maendeleo ya Kimataifa (USAID), imesaini Mkataba wa Dhamana ya Dola milioni 10 na Amana Bank.

Lengo la DCA ni kuimarisha uwezo wa benki kutoa fedha kwa biashara zinazohusiana na ndogondogo, kilimo na biashara za kati na wanawake, pamoja na biashara zinazomilikiwa na vijana nchini Tanzania. (Picha na USAID).
 

 

UTABIRI WA HALI YA HEWA WA SIKU TANO NA ATHARI ZAKE

MAGAZETI YA LEO OKTOBA 09, 2019.

ZAIDI YA WAKAZI MIL.1.9 ARUSHA KUJIANDIKISHA DAFTARI LA KUPIGA KURA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA.

Mkuu wa mkoa wa Arusha akipata maelezo namna ga kujiandikisha kwenye daftari la kupiga kura jana Oktoba 09, 2019, ambapo yeye ni mkazi wa eneo hilo.

Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akipata maelekezo namna ya kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura katika kata ya Murieti ambapo yeye ni mkazi wa eneo hilo.
....................................


Na Vero Ignatus,Arusha.

Zaidi ya wakazi milioni 1.9 mkoa wa Arusha wanatarajia kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura la uchaguzi mdogo wa serikali za mitaa ili kuweza kutimiza haki yao ya msingi ya kikatiba ya kuchagua viongozi wanaowataka kwa ajili ya kujiletea maendeleo katika Nyanja zote.


Richard Kwitega ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha amesema kuwa wananchi hao watapiga kura watakuwa na sifa ya umri wa miaka 18 na kuendelea huku wakiwa na sifa za kuwa wakazi wa eneo husika wanakojiandikishia na kupiga kura .


Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amefika na kujiandikisha katika daftari la kupiga kura, katika kata ya Muriet ambako ni mwenyeji wa eneo hilo, amesema kuwa serikali imeweka mazingira rafiki kwa watu wote kujiandikisha bila kujali itikadi za vyama vyao wote wanapaswa kushiriki katika zoezi hilo la kujiandikisha.


Msena Bina ni msimamizi wa Uchaguzi jiji la Arusha amesema kuwa vituo vimefunguliwa 154 kwa ajili ya wananchi kujiandikisha hivyo amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi.


Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Jonathan Shana amesema kuwa jeshi hilo litaimarisha hali ya ulinzi na usalama, na kufanya kazi bila kupendelea chama chochote, kama walivyotoa maelekezo kwa Askari kufanya kazi kwa uadilifu na uzalendo.

MWENGE WA UHURU KUKAGUA MIRADI YA BILIONI 12 LINDI.

Na Hadija Hassan, Lindi.

Mwenge wa uhuru umewasili Mkoani Lindi ukitokea Mkoani Mtwara ambapo jumla ya miradi ya Maendeleo 28 yenye Thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 12, inatarajiwa kupitiwa.

Mwenge huo wa uhuru umewasili jana Mkoani Lindi na kufanyika makabidhiano katika Kijiji cha Madangwa Halmashauri ya wilaya ya Lindi Mkoani humo na unatarajiwa kukimbizwa katika Halmashauri sita za Mkoa huo.

Akitoa taarifa ya mapokezi ya mbio za Mwenge wa Uhuru, Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi, baada ya makabiziano hayo, alisema kati ya miradi hiyo 28 miradi 9 itawekwa mawe ya msingi ,8 itazinduliwa, 8 itakaguliwa na 3 itafunguliwa.

Aidha Zambi alisema kuwa Mwenge huo wa uhuru unatarajiwa kukimbizwa Umbali wa Km.950.7 katika Wilaya za Lindi, Ruangwa, Nachingwea, Liwale, Kilwa na Mansipaa ya Lindi Mkoani humo.

Nae mkimbiza mwenge kitaifa Mzee Mkongea Ally aliwataka wataalamu wanaohusika na miradi kuwepo kwenye miradi yao wakati wote ambao mwenge utafika katika maeneo yao