Wednesday, September 18, 2019

TIF KWA KUSHRIKIANA NA SHARJAH CHARITY WAFANIKISHA MATIBABU YA MOYO.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akipokea ngao kutoka kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya The Islamic Foundation yenye makao yake makuu mkoani Morogoro, Areef Nahdi, baada ya kukamilisha kambi ya matibabu ya moyo yaliyofadhiliwa na

shirika la Sharjah Charity Group kutoka nchi za Falme za Kiarabu chini ya The Islamic Foundation ya hapa nchini.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimpa ngao Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) iliyotolewa na taasisi ya The Islamic Foundation ya hapa nchini, ikiwa ni kumpongeza kwa jitihada anazozifanya katika kuboresha huduma za matibabu ya moyo katika taasisi hiyo wakati wa kuhitimisha kambi maalum ya matibabu ya moyo inayofanywa na madaktari wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao kutoka Shirika la Sharjah Charity Group leo Jijini Dar es Salaam, anaeshuhudia kushoto ni Mwenyekiti wa The Islamic Foundation, Areef Mbarak Nahdi.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimpa zawadi daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto kutoka Shirika la Sharjah Charity Group kuwapongeza kwa jitihada wanazozifanya kuokoa maisha ya watoto wenye magonjwa ya moyo wakati wa kuhitimisha kambi maalum ya matibabu ya moyo inayofanywa na madaktari wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao kutoka Shirika la Sharjah Charity Group leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Balozi wa Falme za Kiarabu Mhe. Abdulrahman Mohamed Marzooqi.
 

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimpa ngao Kiongozi kutoka shirika la Sharjah Charity Group Ali Mohamed Alrasholi kuthamini mchango unaotolewa na shirika hilo kuokoa maisha ya watoto wenye magonjwa ya moyo wakati wa kuhitimisha kambi maalum ya matibabu ya moyo inayofanywa na madaktari wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao kutoka Shirika la Sharjah Charity Group leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Balozi wa Falme za Kiarabu Mhe. Abdulrahman Mohamed Marzooqi.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katika picha ya pamoja na wataalamu wa afya, viongozi mbalimbali na watoto wenye magonjwa ya moyo wanaopata matibabu katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa kuhitimisha kambi maalum ya matibabu ya moyo inayofanywa na madaktari wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao kutoka Shirika la Sharjah Charity Group leo Jijini Dar es Salaam. Kulia kwa waziri ni Balozi wa Falme za Kiarabu Mhe. Abdulrahman Mohamed Marzooqi

SIMBACHAWENE AAGIZA TAASISI ZIANDAE MAZOEZI YA UPANDAJI MITI ZINAPOFANYA HAFLA MBALIMBALI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. George Simbachawene ambaye pia ni Mbunge wa Kibakwe akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Pwagu wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma katika mkujtano wa hadhara ulioambatana na maombi maalumu alipofanya ziara ya kikazi.
..................................

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. George Simbachawene ameagiza taasisi ziwe zinaandaa utaratibu wa upandaji miti wakati wa matukio au sherehe mbalimbali hatua itakayohakikisha utunzaji wa mazingira unafanyika kwa ufanisi.

Pia amezitaka taasisi za umma, binafsi na za dini kuhakikisha zinaandaa vitalu vya miche ya miti na kugawa kwa wananchi waende kupanda akisema kuwa utaratibu huo utasaidia katika kuhakikisha kunakuwa na ongezeko la miti nchini.

Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Pwaga wakati wa ziara yake ya kikazi Wilayani Mpwapwa katika Jimbo la Kibakwe Mkoani Dodoma, Mhe. Simbachawene alisema wastani wa ukataji miti kwa mwaka ni 496,000 ambao unatokana na shughuli za kibinadamu, hali inayochangia uharibifu wa mazingira na kwa hali hiyo jukumu la kupanda miti ni la kila mtu.

“Nitafurahi kuona kiongozi yeyote anapofanya ziara mahali popote anaandaliwa utaratibu wa kupanda miti halafu ndio ahutubie mkutano na kwa kufanya hivyo tutaweza kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi zinazotokana na kukosekana kwa miti na hapa Sheria ya Mazingira ya Mwaka 2004 inasema kila mtu ni taasisi ya mazingira hivyo ni lazima apande mti,” alisisitiza Waziri.

Kwa hali hiyo Mhe. Simbachawene ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kibakwe alitahadharisha kuwa matumizi ya mkaa kwa kiasi kikubwa yanachangia upotevu wa misitu yetu kwani unahusisha ukataji wa miti ya asili ambayo huleta mvua na uaoto wa asili.

Aidha, katika ziara hiyo Kijijini hapo pamoja na mambo mengine mara baada ya kuwasili Waziri huyo aliongoza zoezi la upandaji miti kwenye eneo la Kituo kipya cha Afya cha Pwaga kwa pamoja na viongozi mbalimbali Wilayani humo akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Paul Sweya.

Waziri huyo amebainisha kuwa shughuli za kibinadamu ni nyingi na harakati za kutafuta maisha zinazosababisha akate miti kwa wingi zimeongezeka na hivyo kumfanya aharibu mazingira kwa kukata miti hivyo ni lazima sasa tulinde misitu yetu kwani ndio uhai wetu.
Kutokana na hilo aliwataka wananchi kuacha mara moja kuvichezea vyanzo vya maji huku na kutaka uwekwe msukumo zaidi kwa wananchi kuhusu suala zima la utunzaji mazingira na kuwa elimu itolewe kuanza ngazi ya shule za msingi ili wanafunzi wapate uelewa.

“Miti ni muhimu sana kwani kusaidia kupunguza mabadiliko ya tabianchi tena wataalamu wanasema ni vizuri kupanda miti ya asili kwani ina uwezo mkubwa wa kunyonya hewa ya kaboni ambayo ikiungana inatengeneza gesi joto ambayo inasababisha tabaka la ozone linalosababisha joto kubwa duniani,” aliasa Mhe.Waziri.

 

BALOZI WA FALME ZA KIARABU ATOA MSAADA KWA WANAFUNZI DAR.

 Mwanafunzi wa shule ya sekondari ya jangwani wa kidato cha tano, akipokea Msaada wa fedha kutoka Kwa Balozi wa nchi za falme za kiarabu Khalifa abdulrahman, pembeni ni mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Paul Makonda.
 
Balozi wa nchi za falme za kiarabu Khalifa abdulrahman, akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kugawa misaada hiyo, kulia ni mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Paul Makonda.
 
Balozi wa nchi za falme za kiarabu Khalifa Abdulrahman, akikabidhi msaada wa fedha kwa wanafunzi mbalimbali wa kidato cha tano Mkoa wa Dar es Salaam pembeni ni mkuu wa Mkoa huo, Paul Makonda.
 
Balozi wa nchi za falme za kiarabu Khalifa Abdulrahman, na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi mbalimbali.