Wednesday, September 18, 2019

SERIKALI KUSHUGHULIKIA CHANGAMOTO SOKO LA NYAMA NJE YA NCHI

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (kulia) akibadilishana mawazo na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti mara baada ya kuwasili ofisini kwake kuanza ziara ya kanda ya ziwa.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (kulia) akipewa maelezo ya ranchi za Mabale, Kagoma na Kikulula zilizopo Wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera na Kaimu Meneja Mkuu wa NARCO Prof. Phillemon Wambura.
..............................


Serikali imesema itahakikisha katika kipindi cha miezi mitatu ijayo changamoto mbalimbali zinazoikabili nchi kwenye soko la nyama nje ya nchi zinatatuliwa ili kuhakikisha wafugaji wananufaika kupitia mifugo yao kwenye soko la nje ya nchi.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amesema hayo katika Ranchi ya Kikulula iliyopo Wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera wakati akizungumza na wawekezaji waliopatiwa vitalu katika ranchi hiyo, ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani humo, ambapo amesema baadhi ya masoko nje ya nchi hushindwa kununua nyama kutoka Tanzania kwa madai yasiyo sahihi kuwa mifugo iliyopo nchini ina maradhi.

Akizungumza na wawekezaji takriban 33 waliopewa vitalu katika ranchi ya Kikulula iliyopo Wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera, Naibu Waziri Ulega amesema katika kipindi cha miezi mitatu ijayo ni lazima vikwazo vilivyopo katika soko la nyama nje ya nchi viwe vimetatuliwa kwa wawekezaji kwenye vitalu kuwa na mipango maalum ya ufugaji ili wakaguzi kutoka nje ya nchi wakija kukagua ubora wa mifugo nchini wapate taarifa sahihi itakayowezesha mifugo na nyama itokanayo na mifugo hiyo ipate soko nje ya nchi kwa kuwa na afya bora.

Aidha Waziri Ulega amesema Ranchi ya Kikulula lazima iendelezwe na kuwa ya mfano kwa kuwekewa mikakati mbalimbali ili iweze kuwa na tija kwa mfugaji na taifa kwa ujumla pamoja na kuwataka wawekezaji kuendeleza vitalu vyao kwa kuweka miundombinu imara bila kuwa na hofu ya uwepo wa mkataba wa muda mfupi wa mwaka mmoja.

Nao baadhi ya wawekezaji katika Ranchi ya Kikukula wameiomba serikali kutatua changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo ikiwemo ya ufinyu wa maeneo ya mifugo yao huku wakiipongeza kwa namna inavyoboresha sekta ya mifugo nchini.

Kwa upande wake Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni ya Ranchi ya Taifa (NARCO) Prof. Phillemon Wambura akijibu hoja hizo amewataka wawekezaji kuhakikisha wanapata vitalu kwa misingi ya kisheria.

Awali Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega mara baada ya kuwasili mjini Bukoba alipata nafasi ya kukutana na mkuu wa mkoa huo brigedia jenerali Marco Gaguti ambapo ameiomba Wizara ya Mifugo na Uvuvi kufanya utafiti namna wafanyabiashara wanavyoweza kunufaika na mabaki ya samaki yakiwemo mabondo.

Naibu Waziri Ulega yupo Mkoani Kagera kwa ziara ya kikazi ya siku tatu ambapo katika siku ya kwanza ametembelea ranchi za Kikulula na Mabale pamoja na kuzungumza na wawekezaji katika ranchi hizo na kufanya mkutano wa hadhara katika kijiji cha Katanda kilichopo Kata ya Kihanga, Wilayani Karagwe.



Tuesday, September 17, 2019

NYANKUMBU KUNUFAIKA NA UMEME WA ELFU 27.

Image may contain: 8 people, people standing
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani, akikata utepe kuashiria uwashaji rasmi wa umeme katika Shule ya Msingi ya Kabeho, iliyopo wilayani Chato, Septemba 16, 2019.
................................
Na Veronica Simba - Geita

Serikali imewaagiza watendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA), kuwaunganishia umeme wananchi wa vijiji vyote 11 vya Kata ya Nyankumbu iliyopo Geita mjini, kwa gharama ya shilingi 27,000 tu kuanzia sasa.

Agizo hilo lilitolewa jana, Septemba 16 mwaka huu na Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, wakati akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Uwanja, Kata ya Nyankumbu, akiwa katika ziara ya kazi.

Waziri alisema, awali, Kata hiyo haikuwa katika mpango wa umeme vijijini, ambao wanufaika wake ndiyo huunganishiwa umeme kwa gharama hiyo lakini baada ya serikali kujiridhisha kuwa eneo hilo halina tofauti na maeneo mengi ya vijijini, imeamua nao wapatiwe huduma hiyo kwa gharama inayotozwa vijijini.

Aidha, Waziri aliwaagiza viongozi wa taasisi husika kwa kushirikiana na mkandarasi anayetekeleza mradi wa umeme vijijini, awamu ya tatu, wilayani humo, kuweka magenge 10 katika Kata hiyo na waanze kuunganishia wananchi umeme mara moja.

Hata hivyo, Waziri Kalemani alibainisha kuwa, watakaounganishiwa umeme kwa gharama ya shilingi 27,000 katika eneo hilo, ni wale tu wateja wapya na kwamba wale ambao walikwishaunganishiwa awali kwa gharama tofauti, hawatahusika na hawatarejeshewa fedha.

Katika hatua nyingine, Waziri aliendelea kusisitiza agizo lililotolewa na serikali kuwa wananchi vijijini hawapaswi kulipia nguzo wala kifaa kingine chochote isipokuwa gharama za kutandaza mfumo wa nyaya kwenye majengo yao (wiring), ambazo ni makubaliano yao binafsi na wakandarasi watakaowafanyia kazi hiyo.

Alitoa onyo kali kwa yeyote atakayebainika kumwambia mwananchi kulipia nguzo au kumtoza gharama nyingine yoyote zaidi ya shilingi 27,000 tu ambayo ndiyo bei halali iliyotangazwa na serikali kwa ajili ya kuunganishia umeme wananchi wa vijijini.

Katika ziara hiyo, Waziri pia alitembelea kijiji cha Kabeho kilichopo wilayani Chato mkoani humo, ambapo aliwasha rasmi umeme katika Shule ya Msingi ya kijiji hicho.

Aliwataka wanafunzi kuutumia umeme huo kwa ajili ya kuongeza kiwango cha ufaulu shuleni hapo.
Image may contain: 5 people, people smiling, people standing and outdoor

Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (kulia), akimkabidhi kifaa cha Umeme Tayari (UMETA), mmoja wa wanakijiji wa Kabeho wilayani Chato, wakati wa hafla ya uwashaji rasmi umeme katika kijiji hicho, Septemba 16, 2019.
Image may contain: 7 people, people smiling, crowd and outdoor 

WAKULIMA KIJIJI CHA VISAKAZI WAIOMBA SERIKALI KUTATUA MIGOGORO INAYOHUSU MIFUGO.

Na Omary Mngindo, Ubena.

WAKULIMA katika Kijiji cha Visakazi, Kata ya Ubena halmashauri ya Chalinze wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, wameitaka Serikali kuwatafutia suluhu ya migogoro inayohusiana na mifugo kijijini hapo.

Wakizungumza na Waandishi wa habari kijijini hapo, wakazi Daud Selemani, Selemani Mtonga wakiwemo wezee maarufu John Lumoto na Mwinjuma Malano kwa niaba ya wenzao walisema kuwa hali kijijini hapo ni mbaya kutokana na wingi wa mifugo.


"Mimi na familia yangu tuko katika hali ngumu ya kiuchumi kutokana na kuwepo kwa wafugaji kwenye maeneo yetu ambayo ni kwa ajili ya kilimo, kama mnavyojionea mazao yangu yote yameliwa, mihogo imeng'olewa pamoja na miche ya minanasi," alisema Mtonga.

Kwa upande wake Daud amewaonesha waandishi wa habari miche ya mikorosho na migomba ambayo imeliwa na mifugo hali iliyomfanya mkulima huyo kuangusha kilio kutokana na uharibifu huo.

"Serikali inatutaka vijana tujikite kwenye kilimo, tunalima lakini mwisho wa siku mifugo inaingizwa kwenye mashamba tunapokwenda kulalamika kwenye ofisi za serikali hakuna hatua zinazochukuliwa, hii hali isipoangaliwa inaweza kusababisha hali mbaya," alisema Daud.

Mkazi Lumoto aliwataka viongozi waliochaguliwa kutimiza majukumu yao na si kila kitu aingilie Rais John Magufuli na kuongeza kwamba hatua ya rais kuingilia migogoro inayopaswa kutatuliwa na wateule wake ni udhaifu kwa wateule hao.

Akizungumzia migogoro ya mifugo, Ofisa wa kitengo hicho kijijini hapo Malilo Daniel alisema kwamba, hali ni tete kutokana na mifugo kuwa mingi aliyofikia elfu hamsini, huku eneo la kufugia likiwa eka 499 tu, wakati eka elfu nane zikiwa kwenye hifadhi ya Wami Mbiki.

"Wastani ng'ombe mmoja kwa mwaka anakula eka moja, hivyo kutokana na wingi huo mifugo kijijini hapa, kwa kipindi hiki kuna kesi za mifugo zipatazo 156, hii inadhihirisha kwamba hali si ya kuridhisha," alisema Daniel.

RAIS. DKT. MAGUFULI AMTENGUA DC WA MALINYI NA MKURUGENZI WAKE.

Image may contain: text