Saturday, June 29, 2019

RUVUMA YAFANIKIWA KUTOA CHANJO KWA WATOTO WACHANGA KWA ASILIMIA 102

Dk.Jair Khanga Mganga mkuu Ruvuma
  Joyce Joliga  Songea.
Wazazi wameshauliwa kuacha  utoro wa kuwapeleka watoto wao Kliniki ili waweze kupata chanjo za kuwakinga na Ulemavu au vifo  vinavyotokana na maradhi mbalimbali .
  Hata hivyokwa mujibu wa  takwimu za mwaka 2017 za  Shirika la afya duniani (WHO)zinaonyesha kuwa upatikanaji wa chajo umeongezeka ambapo watoto 85% wanachanjwa  ambapo zaidi ya watoto 16 walipata chanjo muhimu tatu za kuwakinga dhidi ya magonjwa ya kuambukiza ambayo wakati mwingine usababisha ulemavu.
Tayari  Mkoa wa Ruvuma imefanikiwa kutoa chanjo  ya Matone Polio,kifua kikuu kwa watoto weny e umri chini ya miaka mitano kwa 102% katika kipindi cha January-Machi 2019 .
 Mganga mkuu mkoa wa Ruvuma Dkt.Jair Khanga anasema hali ya utoaji chanjo kwa watoto chini ya miaka mitano inazidi kuhimarika ambapo  kwa mwaka 2018  asilimia 93 walipata chanjo hizo na kutokana na mikakati mbalimbali waliyojiwekea  idadi ya watoto waliopata kinga imepanda  na wanatarajia kufikia 130% hadi kufikia Desemba 2019.

Anasema, Chanjo hukinga maradhi, ulemavu na vifo vitokanavyo na magonjwa yanayozuilika kwa chanjo ikiwa ni pamoja na surua, homa ya ini (hepatitisi B), dondakoo, kifaduro, nimonia, polio, kuhara kunakosababishwa na virusi vya rota, rubela na pepopunda.
Dkt.Khanga anasema, Watoto waliopata chanjo huwa wamekingwa dhidi ya magonjwa haya hatari, ambayo kwa kawaida huweza kusababisha ulemavu au kifo.

Anasema ,elimu iliyotolewa kwenye  kampeni maalum iliyoanzishwa ya kuwaelimisha wazazi umuhimu wa chanjo kwa watoto imesaidia wazazi na walezi kupata uelewa  na kuwapeleka watoto kupata chanjo  hali ambayo imesaidia kuongezeka kwa  idadi ya waliopata chanjo hivyo kuwanusuru na magonjwa bali mbali ikiwemo  upofu, ulemavu pamoja na vifo.

Dkt.Khanga anaeleza kuwa elimu inaendelewa kutolewa kwa jamii huduma za mkoba pia chanjo  zinapatikana kuanzia ngazi ya zahanati, vituo vya afya , hospitalini  pia commitment ya wahudumu ni kubwa wanahakikisha  kila mtoto anafikiwa.
Aidha, ameongeza kuwa ni asilimia ya wanawake 82.2% pekee ndio wanajifungulia hospitalini , kwenye vituo vya afya na Zahanati  na asilimia 17.8%  wanajifungulia  majumbani na kwa wakunga wa jadi  hivyo hakuna  chanjo wanazopata na amewashauri kujifungulia  Hospitali ili watoto wao waweze kupata chanjo  hizo muhimu  .
Amewashauri wazazi na walezi wa watoto wenye umri kuanzia  0- 5 miaka kuhakikisha wanawapeleka watoto wao kliniki na kufata maelekezo yote wanayopewa na wataalam wa afya ili kuweza kuwa na jamii yenye afya bora  na salama .
 kwa upande wake Mariam  Ally Mkazi  Kijiji cha Lyangweni amekiri kuwepo kwa uzembe wa baadhi ya wazazi kutowapeleka watoto wao  kliniki ambapo amesema wapo ambao wanaamini madawa ya kienyeji  kuwa yanawakinga watoto wao na wapo ambao wanapuuza tu  na hawana sababu ya msingi.
“kiukweli hata mimi sikujua kama kuna umuhimu wa watoto wetu kupelekwa  Kliniki , kutokana na kubanwa na kazi nyingi za kilimo  nimekuwa mzembe naahidi kuanzia sasa nitampeleka mwanangu  Husein kliniki ili niweze kumnusuru na magonjwa mbalimbali,”alisema

KINA MAMA WAJAWAZITO 18 WAFANYIWA UPASUAJI KILWA.


 Chumba cha upasuaji katika kituo cha Afya Kilwa Msoko, wilayani Kilwa mkoa wa Lindi.

 
Jengo la kituo cha Afya Kilwa Msoko, wilayani Kilwa mkoa wa Lindi, Picha zote Na Hadija Hassan.
..................................

 NA HADIJA HASSAN, LINDI…


Jumla ya kina Mama wajawazito 18 kutoka katika kata ya masoko na maeneo jirani wamefanyiwa upasuaji mkubwa katika kituo cha afya cha kilwa masoko kilichopo katika Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi baada ya kukosa Huduma hiyo kwa miaka mingi.


Hayo yameelezwa na Mganga Mfawidhi wa kituo hicho cha Afya Dkt, Daud Selema jana alipokuwa akizungumza na BAGAMOYO KWANZA BLOG ilipotembelea kituoni hapo.


Dkt. Selema Alisema upasuaji huo ni wa miezi Saba kuanzia September 2018 mpaka April 2019.
Alisema kuwa kituo hicho cha Afya Masoko ni miongoni mwa vituo 44 vya Afya Nchini vilivyofanyiwa ukarabati na Serikali lengo likiwa kuzingatia majengo ya Muhimu katika utoaji wa huduma za Mama, Baba na Mtoto.


Aliongeza kuwa, kufuatia ukarabati huo kituo hicho cha Afya kimeshaanza kutoa huduma za upasuaji ambao ndio lengo kuu la vituo vinavyokarabatiwa ili kuweza kutoa huduma za dharula kwa kina Mama wajawazito wanaopata changamoto wakati wa kujifungua.


Alisema kabla ya kufanyiwa ukarabati huo walikuwa wanalazimika kumuhamisha Mama Mjamzito ambae ameshindwa kujifungua kwa njia ya kawaida na kumpeleka katika Hospital ya Wilaya ambayo ipo umbali wa kilometa 30 kutoka kituo hicho cha Afya kilipo.


“hali hii ilikuwa ni hatari kwa usalama wa uhai kwa Mama Mjamzito mwenyewe na hata kwa Mtoto atakae zaliwa kwani kutokana na muongozo wetu ni lazima mama huyo awe amefikia hatua Fulani ya uchungu na tuthibitishe kwamba kweli atashindwa kujifungua kwa kawaida ndipo tunaweza kuamua Mama huyo afanyiwe Upasuaji ambapo hata hivyo Huduma hiyo haikuwepo” Alifafanua Dkt, Selema.


Hata hivyo DKT, Selema aliwataka kinamama wajawazito kuwahi kituo cha Afya mapema pindi wanapojisikia dalili za uchungu ili watakapoanza kupata matatizo madogo madogo wakati wa kujifungua waweze kupatiwa huduma ya upasuaji mapema ili kumuokoa mama na mtoto atakae zaliwa.


Wakizungumza kwa nyakati tofauti Baadhi ya kina Mama waliokuja kupatiwa Huduma za Matibabu Katika Kituo hicho cha Afya akiwemo Asha Kiambi Mkazi wa Mtaa wa Mifugo kilwa Masoko na Kibibi Duka Mkazi wa Kilwa Masoko Walisema kuwa kutolewa kwa huduma za upasuaji Katika Kituo hicho Cha Afya kumewasaidia kupungunza gharama za Usafiri pindi Mama mjamzito anapotakiwa kupewa Rufaa kwenda Hospital ya Wilaya.


"Hapo zamani Kama Mgonjwa wako atapewa Rufaa kwenda Katika Hospital ya Wilaya tulikuwa tunalazimika kuchangia Mafuta kwa ajili ya Gari ya kumbeba Mama huyo Mjamzito lakini kwa sasa tunaishukuru Serikali kwa kutuletea huduma za Upasuaji Katika Kituo Chetu ambapo gharama hizo sasa tutaondokana nazo"alieleza kiambi.


 "Uwepo wa Huduma hii pia umeturahisishia kupata muda wa ziada wa kuendelea Kufanya majukumu mengine kwa wakati Mfano Kama utapewa Rufaa ya kwenda kwenye Hospital ya Wilaya lazima itakubidi ukae huko mpaka mgonjwa wako atakapopata nafuu na kurudi nyumbani lakini Hapa kwa kuwa pamekuwa Karibu na nyumbani unaweza ukamuhudumia mgonjwa na Ukafanya na mambo Mengine kulingana na Hali ya Mgonjwa wako" aliongeza Duka

MAGAZETI YA LEO JUNI 29, 2019.

KILWA WAFANYA UPASUAJI WA MABUSHA BURE.

Madaktari katika kituo cha Afya Kilwa Masoko wilayani Kilwa Mkoa wa Lindi, wakifanya upasuaji kwa wagonjwa wa Mabusha (Ngiri maji) upasuaji huo umeanza Juni 24 na kuendelea hadi Julai 03 mwaka huu 2019.

 
Baadhi ya wakazi wa Kilwa walipata huduma ya kufanyiwa upasuaji wa mabusha (Ngiri maji) kama walivyokutwa na mpiga picha wetu katika kituo cha Afya Kilwa Masoko wilayani Kilwa Mkoa wa Lindi,
upasuaji huo umeanza Juni 24 na kuendelea hadi Julai 03 mwaka huu 2019. Picha zote Na Hadija Hassan.
 ...................................


NA HADIJA HASSAN, LINDI.

Wagonjwa 250 wenye Mabusha (ngili maji) wa wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji mkubwa katika kituo cha Afya Cha Kilwa masoko Wilayani humo.


Hayo yameelezwa na Mganga Mfawidi wa kituo hicho cha Afya Masoko Dkt, Daud selema alipokuwa anazungumza na BAGAMOYO KWANZA BLOG Jana ofisini kwake.


Dkt, Selema alisema kuwa upasuaji huo utafanyika kwa siku kumi mfululizo kuanzia june 24 mwaka huu mpaka julai 3 mwaka huu 2019 ambapo watu wenye matatizo hayo watafanyiwa upasuaji bure.


Aidha, Dkt, Selema aliongezakuwa,  zoezi hilo la upasuaji mabusha linafanyika kwa kushirikiana na wizara ya Afya, madaktari bingwa kutoka muhimbili pamoja na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Matibabu (NIMR).


Aidha Dkt, Selema alisema kuwa tokea zoezi hilo limeanza tayari wameshafanya upasuaji kwa wagonjwa zaidi ya 70 waliofika Hospitalini hapo.


Nao baadhi ya wagonjwa ambao tayari wameshafanyiwa upasuaji huo akiwemo Bakari saidi mkazi wa masoko Mtaa wa Mnazo mmoja, Abdallah Magonga mkazi wa kijiji cha Kiwawa Kilwa na Ahamedi Saidi, kwa pamoja walisema wanaishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kuendesha zoenzi hilo bure.


Nae Bakari Saidi alisema tatizo hilo la Ngili maji kwake liligundulika miaka minane iliyopita ambapo anasema kuwa kutokana na gharama za upasuaji kuwa kubwa alishindwa kwenda hospitali ili kufanyiwa upasuaji huo hivyo mpango huo umeweza kumuondolea maradhi yaliyokuwa yakimsumbua kwa muda mrefu.


Kwa upande wake Abdallah Mganga alisema kuwa changamoto aliyokuwa anakabiliana nayo kabla hajafanyiwa upasuaji huo ni kuwa na homa za mara kwa mara, maumivu maeneo ya nyonga pamoja na kukosa hamu ya tendo la ndoa Huku ahmedi Saidi akiwashauri wanaume walio na matatizo kama yake kujitokeza kwa wingi ili kuweza kufanyiwa upasuaji kwani ni Bure na huduma zinazotolewa zinaridhisha.


“mimi nawashauri vijana wenzangu, wazee wote walio na matatizo kama haya waje wafanye upasuaji maana hivi vizigo havina faida bora ufuge kuku nyumbani utakula nyama au utamuuza utapata pesa sasa mizigo hii itatusaidia nini? Aalimalizia kwa kuhoji.