Monday, June 24, 2019

DED-BAGAMOYO ATAKA WATUMISHI KUFANYA KAZI KWA KUZINGATIA SHERIA.

Image may contain: 3 people, people sitting
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Bi. Fatuma Latu amewaasa watumishi wa Halmashauri hiyo kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria, Taratibu na Kanuni (STK) za utumishi wa Umma ili kuleta matokeo chanya kwenye utumishi.


Bi. Fatuma Latu, ameyasema hayo mapema wakati alipokuwa akifungua mkutano maalum wa watumishi takribani 200 wa Halmashauri hiyo, uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri, katika kilele cha maadhimisho ya juma la utumishi wa Umma.


“Kila mtumishi ahakikishe anafanya kazi kwa kuzingatia Sheria, taratibu na kanuni za utumishi wa Umma, hizi ziwe dira wakati tukitimiza majukumu yetu ya kila siku ili kuleta matokeo chanya ya utekelezaji wa shughuli za Serikali katika Halmashauri yetu” Alisema Bi. Fatuma Latu.


Bi. Fatuma Latu pia ametumia fursa hiyo kuwaasa Watumishi kuhakikisha wanajiepusha na vitendo vya rushwa, matumizi ya lugha chafu, na kuhimiza ushirikiano baina ya watumishi katika ngazi zote, huku akitanabaisha kwamba hatamvumilia mtumishi yeyote ambaye atapatikana na makosa ya kuomba ama kupokea rushwa.


Akaongeza, Suala la kutunza siri pia ni muhimu sana wakati wa utekelezaji wa Shughuli za Serikali kila mmoja katika nafasi yake, utunzaji wa Siri unatufanya kufanya kazi kwa kuaminiana na kwa usalama wakati wote hivyo kuongeza ari ya kutumikia Wananchi.


Vilevile, Mkurugenzi Mtendaji, Bi. Fatuma Latu, amewakumbusha watumishi kuhakikisha wanapata chakula bora na kujipa muda wa kupumzika baada ya kumaliza kutimiza majukumu yao ya kila siku ili mwili uwe na Afya wakati wote na kuongeza uwezo wa kufanya kazi.


Nae, Mkuu wa Idara ya Utumishi na Utawala Ndg. George Mwalukasa akizungumza na watumishi katika Mkutano huo amewahimiza watumishi kuwa makini pale wanapotakiwa kuhuisha taarifa zao za kiutumishi, kwani wengi wao wamekuwa na hulka ya kupuuzia maagizo ya usafishaji taarifa za kiutumishi yanapotolewa, kwani kupuuzia usafishaji wa taarifa za mtumishi kunaweza kupelekea mtumishi kuondolewa katika orodha ya malipo ya mshahara.


Aliongeza kwa kusema  “Mtumishi ambaye hatajaza fomu za OPRAS kuaniza tarehe 01 Julai, 2019, ambapo OPRAS zitaanza kujazwa kwa njia ya kielektroniki, hatapata mshahara hadi hapo atakapokuwa amejaza fomu hiyo ya upimaji wa utendaji kazi wa Mtumishi, yaani OPRAS”.


Wakati huo huo, watumishi wamepata darasa maalum la madhara ya kujihususha na vitendo vya rushwa ambapo Afisa TAKUKURU – Elimu kwa Umma, Bi. Jane Mgaya amezungumzia mada maalum ya madhara ya vitendo vya Rushwa katika utendaji kazi wa kila mtumishi anapokuwa akitekeleza majukumu yake ya kila siku.


“Tuepuke mambo yanayopelekea uwepo wa mazingira ya vitendo vya rushwa kutengenezwa, tunapokuwa tukitekeleza majukumu yetu ya kila siku, mambo hayo ni pamoja na ukosekanaji wa uwazi katika uwajibikaji, urasimu katika utoaji huduma na tamaa ya kujipatia mafanikio kwa haraka” Alisema Bi. Jane Mgaya


Aliongeza, athari za rushwa ni kubwa kwani rushwa huondoa utu na thamani ya mtu, hudhoofisha utoaji huduma bora, kukosekana kwa uwazi na uwajibikaji katika utumishi wa umma na hupelekea mtumishi kufanya maamuzi yenye upendeleo, hivyo akasisitiza kila mmoja kushiriki katika vita dhidi ya rushwa ili kuiletea jamii yetu maendeleo kwani vita dhidi ya rushwa si ya TAKUKURU peke yake bali ni ya jamii nzima ili kuiletea jamii yetu maendeleo.


Wiki ya utumishi wa umma huadhimishwa mara moja kila Mwaka kila ifikapo Mwezi Juni, ambapo shughuli mbalimbali za kiutumishi huambatana na maadhimisho hayo, ikiwa na pamoja kusikiliza kero na malalamiko toka kwa Watumishi na kuzipatia ufumbuzi,


Aidha, katika maadhimisho hayo kunakuwa na semina mbalimbali zinazohamasisha weledi na utawala bora katika utumishi wa umma, pamoja na mkutano maalum wa watumishi ambao hufanyika siku ya kilele cha Wiki ya Utumishi wa Umma ambao huhudhuriwa pia na wadau mbali mbali toka sekta binafsi zikiwemo taasisi za kifedha na mashirika binafsi Wilayani hapa.
Image may contain: 2 people, people sitting, table and indoor

Tuesday, June 18, 2019

WANANCHI LINDI WAHAMASISHWA KUCHANGIA DAMU.

Mkazi wa anispaa ya Lindi Juma Bakari akichangia damu katika moja ya vituo vya kutolea damu mjini humo.

NA HADIJA HASSAN, LINDI

Kundi la akinamama wajawazito na watoto wachanga limetajwa kuwa ndio kundi kubwa lenye mahitaji ya Damu salama katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Lindi sokoine.

Hayo yamebainishwa na mtaalamu wa Maabara wa Hospitali  ya Rufa ya Lindi, Diana Ngowi katika maojiano maalumu yaliyofanywa na BAGAMOYO KWANZA BLOG ambayo ilitaka kujua hali ya ukusanyaji wa Damu pamoja na matumizi yake katika Hospitali hiyo.

Ngowi alisema kwa kipindi cha miezi mitatu January-machi 2019 Hospitali hiyo ilikusanya jumla ya Lita 372 za damu huku akitaja matumizi ya Damu kwa mwezi lita 110.

Alisema 55% ya Damu inayotumika katika hospitali hiyo ni kwa ajili ya akinamama wajawazito 20% kwa ajili ya wagonjwa wa upasuaji, 10% watoto wachanga na asilimia 15 makundi mengine.

Ngowi alitaja sababu kubwa ya kundi hilo kuwa na mahitaji ya damu ni matatizo wakati wa kujifungua ambayo hupelekea upasuaji , kutokwa na damu nyingi wakati wa kujifungua, mahudhurio hafifu ya Kliniki, kutotumia vidonge vya kuongeza damu vinavyotolewa katika Kliniki.

Nae Merina Bwago Mtaalamu wa Maabara wa Manispaa ya Lindi alisema kuwa licha ya kufanya uhamasishaji kupitia radio za kijamii zilizopo mkoani hapo pamoja na matangazo mbali mbali lakini bado jamii kubwa ya wananchi wanaoishi katika manispaa hiyo wamekuwa na tabia ya kuchangia damu kwa matukio mfano wakati wa kampeni au wanapokuwa na mgonjwa aliekuwa na mahitaji ya damu.

wambo alisema kuwa hali hiyo ya uchangiaji wa Damu inawafanya wakusanye kiasi kidogo cha damu inayotakiwa kutumika kama dharula kulingana na mahitaji ya damu yaliyopo katika hospital hiyo Mbwambo aliongeza kuwa watu wengi hawapendi kuchangia damu kwa kuhofia kupimwa magonjwa mbali mbali kama vile ukimwi, kaswende, manjano na magonjwa mengine ya zinaha

“lakini pia kuna baadhi ya vitu wanaviogopa Damu yako mpaka ije itumike imeshafanyiwa vipimo visivyopungua vinne , ugonjwa wa presha, kaswende, ugonjwa wa manjano ukimwi pamoja na wingi wa damu , sasa hivi vinne kidogo ni changamoto.

Watu wengi wanaona nikienda pale si nitagundulika nina ukimwi,si nitagundulika nina manjano bila kujua ukichangia damu kunafaida ya kujua hivyo vitu, na kuchangia damu hulipii hela yoyote lakini ukichangia unapimwa hivyo vipimo na ukibainika unaugojwa unapatiwa matibabu” alisema Bwambo.

Ugo amandusi na bakari juma ni miongoni mwa vijana wachache katika manispaa ya lindi ambao wamejiwekea utaratibu wa kuchangia Damu kila baada ya Miezi mitatu walisema kuwa kuchangia kwao damu kumekuwa kukiwasaidia pindi wanapokuwa na wagonjwa katika hospitali mbali mbali hapa nchini wanapokuwa na mahitaji ya damu hutumia kadi zao za uchangiaji na kuwawekea ndugu zao.

Ugo alisema ameamua kuchangia Damu ili kuwasaidi watu wenyemahitaji ya huduma hiyo huku akisema kuwa kutoa kwake damu ni sawa na sadaka kubwa kwa mwenyezimungu.

Nae Bakari Juma alitumia fursa hiyo kuwaasa wakazi wa Manispaa hiyo kujenga tabia ya kuchangia damu ili kuwasaidia watu wenye mahitaji ya Damu ikiwa ni  pamoja na kundi la akina mama wajawazito na watoto wadogo

MAGAZETI YA LEO JUNI 18, 2019.

Monday, June 17, 2019

NMB LINDI YATAKA WAKULIMA WA KOROSHO KUCHUKUA MIKOPO.


NA HADIJA HASSAN, LINDI

BANK ya National microfinance Bank ( NMB) Tawi la Lindi imewaaasa wakulima wa zao la Korosho Mkoani Humo kuchangamkia fulsa ya Mikopo ya Pembejeo pamoja na vifaa mbali mbali vya kilimo vinavyotolewa na Bank hiyo ili kuongeza tija ya uzalishaji wa Mazao yao.

Hayo yameelezwa na Meneja wa NMB- Shaabani kasali katika mafunzo ya utumiaji ya viuwatilifu Vya zao la korosho yaliyofanyika katika Halmashauri ya Manispaa ya Lindi Mkoani humo yaliyotolewa na Bodi ya Korosho Tanzania ambayo yaliwakutanisha Wakulima wa zao hilo wapuliziaji wa viuwatilifu pamoja na maafisa ugani lengo likiwa ni kuhamasisha matumizi sahii ya viuwatilifu.

Kasali alisema katika kushiriki kusaidia matumizi bora ya viwatilifu benki yao inawasaidia wakulima wa zao hilo kuwawezesha kuwapatia mikopo itakayoweza kununua pembejeo pamoja na zana mbali mbali za kilimo.

Alisema katika Msimu uliopita Bank hiyo iliweza kutoa Mikopo kwa wakulima wa zao hilo zaidi ya shilingi billion 30 kwa wakulima wa ukanda wa kusini kwa ajili ya kuwawezesha kutumia viuwatilifu ili kuhakikisha mazao hayo yanapatikana.

Aidha kasali aliongeza kuwa licha ya mikopo hiyo ya pembejeo na viuwatilifu alitaja mikopo mingine inayotolewa kwa wakulima hao ni vifaa mbali mbali vya kilimo kama vile matrekta pamoja na mashine za upuliziaji.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga akizungumza na washiriki wa mafunzo hayo alisema kuwa ili kuweza kufikiwa na fulsa hiyo ya Mikopo ni vyema kwa wakulima hao wakajisajili katika Dafutari la kudumu la wakulima itakayomuwezesha kufahamika kwa urahisi katika taarifa zao