Tuesday, June 18, 2019

WANANCHI LINDI WAHAMASISHWA KUCHANGIA DAMU.

Mkazi wa anispaa ya Lindi Juma Bakari akichangia damu katika moja ya vituo vya kutolea damu mjini humo.

NA HADIJA HASSAN, LINDI

Kundi la akinamama wajawazito na watoto wachanga limetajwa kuwa ndio kundi kubwa lenye mahitaji ya Damu salama katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Lindi sokoine.

Hayo yamebainishwa na mtaalamu wa Maabara wa Hospitali  ya Rufa ya Lindi, Diana Ngowi katika maojiano maalumu yaliyofanywa na BAGAMOYO KWANZA BLOG ambayo ilitaka kujua hali ya ukusanyaji wa Damu pamoja na matumizi yake katika Hospitali hiyo.

Ngowi alisema kwa kipindi cha miezi mitatu January-machi 2019 Hospitali hiyo ilikusanya jumla ya Lita 372 za damu huku akitaja matumizi ya Damu kwa mwezi lita 110.

Alisema 55% ya Damu inayotumika katika hospitali hiyo ni kwa ajili ya akinamama wajawazito 20% kwa ajili ya wagonjwa wa upasuaji, 10% watoto wachanga na asilimia 15 makundi mengine.

Ngowi alitaja sababu kubwa ya kundi hilo kuwa na mahitaji ya damu ni matatizo wakati wa kujifungua ambayo hupelekea upasuaji , kutokwa na damu nyingi wakati wa kujifungua, mahudhurio hafifu ya Kliniki, kutotumia vidonge vya kuongeza damu vinavyotolewa katika Kliniki.

Nae Merina Bwago Mtaalamu wa Maabara wa Manispaa ya Lindi alisema kuwa licha ya kufanya uhamasishaji kupitia radio za kijamii zilizopo mkoani hapo pamoja na matangazo mbali mbali lakini bado jamii kubwa ya wananchi wanaoishi katika manispaa hiyo wamekuwa na tabia ya kuchangia damu kwa matukio mfano wakati wa kampeni au wanapokuwa na mgonjwa aliekuwa na mahitaji ya damu.

wambo alisema kuwa hali hiyo ya uchangiaji wa Damu inawafanya wakusanye kiasi kidogo cha damu inayotakiwa kutumika kama dharula kulingana na mahitaji ya damu yaliyopo katika hospital hiyo Mbwambo aliongeza kuwa watu wengi hawapendi kuchangia damu kwa kuhofia kupimwa magonjwa mbali mbali kama vile ukimwi, kaswende, manjano na magonjwa mengine ya zinaha

“lakini pia kuna baadhi ya vitu wanaviogopa Damu yako mpaka ije itumike imeshafanyiwa vipimo visivyopungua vinne , ugonjwa wa presha, kaswende, ugonjwa wa manjano ukimwi pamoja na wingi wa damu , sasa hivi vinne kidogo ni changamoto.

Watu wengi wanaona nikienda pale si nitagundulika nina ukimwi,si nitagundulika nina manjano bila kujua ukichangia damu kunafaida ya kujua hivyo vitu, na kuchangia damu hulipii hela yoyote lakini ukichangia unapimwa hivyo vipimo na ukibainika unaugojwa unapatiwa matibabu” alisema Bwambo.

Ugo amandusi na bakari juma ni miongoni mwa vijana wachache katika manispaa ya lindi ambao wamejiwekea utaratibu wa kuchangia Damu kila baada ya Miezi mitatu walisema kuwa kuchangia kwao damu kumekuwa kukiwasaidia pindi wanapokuwa na wagonjwa katika hospitali mbali mbali hapa nchini wanapokuwa na mahitaji ya damu hutumia kadi zao za uchangiaji na kuwawekea ndugu zao.

Ugo alisema ameamua kuchangia Damu ili kuwasaidi watu wenyemahitaji ya huduma hiyo huku akisema kuwa kutoa kwake damu ni sawa na sadaka kubwa kwa mwenyezimungu.

Nae Bakari Juma alitumia fursa hiyo kuwaasa wakazi wa Manispaa hiyo kujenga tabia ya kuchangia damu ili kuwasaidia watu wenye mahitaji ya Damu ikiwa ni  pamoja na kundi la akina mama wajawazito na watoto wadogo

MAGAZETI YA LEO JUNI 18, 2019.

Monday, June 17, 2019

NMB LINDI YATAKA WAKULIMA WA KOROSHO KUCHUKUA MIKOPO.


NA HADIJA HASSAN, LINDI

BANK ya National microfinance Bank ( NMB) Tawi la Lindi imewaaasa wakulima wa zao la Korosho Mkoani Humo kuchangamkia fulsa ya Mikopo ya Pembejeo pamoja na vifaa mbali mbali vya kilimo vinavyotolewa na Bank hiyo ili kuongeza tija ya uzalishaji wa Mazao yao.

Hayo yameelezwa na Meneja wa NMB- Shaabani kasali katika mafunzo ya utumiaji ya viuwatilifu Vya zao la korosho yaliyofanyika katika Halmashauri ya Manispaa ya Lindi Mkoani humo yaliyotolewa na Bodi ya Korosho Tanzania ambayo yaliwakutanisha Wakulima wa zao hilo wapuliziaji wa viuwatilifu pamoja na maafisa ugani lengo likiwa ni kuhamasisha matumizi sahii ya viuwatilifu.

Kasali alisema katika kushiriki kusaidia matumizi bora ya viwatilifu benki yao inawasaidia wakulima wa zao hilo kuwawezesha kuwapatia mikopo itakayoweza kununua pembejeo pamoja na zana mbali mbali za kilimo.

Alisema katika Msimu uliopita Bank hiyo iliweza kutoa Mikopo kwa wakulima wa zao hilo zaidi ya shilingi billion 30 kwa wakulima wa ukanda wa kusini kwa ajili ya kuwawezesha kutumia viuwatilifu ili kuhakikisha mazao hayo yanapatikana.

Aidha kasali aliongeza kuwa licha ya mikopo hiyo ya pembejeo na viuwatilifu alitaja mikopo mingine inayotolewa kwa wakulima hao ni vifaa mbali mbali vya kilimo kama vile matrekta pamoja na mashine za upuliziaji.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga akizungumza na washiriki wa mafunzo hayo alisema kuwa ili kuweza kufikiwa na fulsa hiyo ya Mikopo ni vyema kwa wakulima hao wakajisajili katika Dafutari la kudumu la wakulima itakayomuwezesha kufahamika kwa urahisi katika taarifa zao

DKT. ABBASI AIPONGEZA PSSSF.

 Msemaji Mkuu wa serikali ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo, Dkt. Hassan Abbasi, (kushoto), akipeana mikono na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSSSF bw. Abdul Njaidi.
 
Dkt. Abassi (kulia), akijadiliana jambo na Bi. Eunice Chiume, (katikati), na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSSSF, Bw. Abdul Njaidi ,mara baada ya mazungumzo yao.

 ............................................

MSEMAJI Mkuu wa serikali, Dkt. Hassan Abbasi ameupongeza Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa watumishi wa Umma (PSSSF) kwa kuanza vizuri kutekeleza majukumu yake katika kipindi kifupi tangu kuunganishwa kwa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.


Dkt. Abbasi ameyasema hayo leo Jumamosi Juni 15, 2019 ofisini kwake jijini Dar es Salaam wakati alipotembelewa na Meneja Kiongozi Uhusiano na Elimu kwa Umma wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, (PSSSF), Bi. Eunice Chiume, aliyefuatana na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo Bw. Abdul Njaidi.


Kwa takriban wiki nzima, Meneja huyo amekuwa kwenye ziara ya kuvitembelea vyombo vya habari ikiwemo mitandao ya kijamii ili kujenga mahusiano ikiwa ni pamoja na kueleza malengo ya Mfuko huo ambao ni mpya baada ya serikali kuunganisha Mifuko minne ya Hifadhi ya Jamii ya PSPF, LAPF, PPF na GEPF kwa lengo la kuboresha utoaji huduma.


“Tunaposikia kuwa watu wameanza kupata mafao yao tena kwa wakati kwakweli ni jambo la faraja kwa serikali kwa hiyo mpeleke salamu zangu kwa watendaji wote, akiwemo mtendaji mkuu wa Mfuko, tunafarijika sana tunapoona kwamba yale malengo ya serikali kuu kuunganisha hii mifuko ili kutoa huduma bora yametimia.” Alisema.


Dkt, Abbasi ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Malezeo, pia amempongeza Meneja huyo kwa uamuzi wa kuvitembelea vyombo vya habari kwa lengo la kuelimisha umma na kueleza shughuli za Mfuko kwani hii itasaidia wanachama kujua kinachoendelea kwenye Mfuko wao.



“Huu ni Mfuko mpya, yako maswali mengi yanayozua tashtiti na tashwishwi ambavyo kwa pamoja vinafanya kitu kinaitwa jakamoyo ambayo ni vile mtu anaumia moyoni kumbe anakuwa tu hana taarifa sahihi, hili nalo niwapongeze baada ya kukamilisha zile taratibu za ndani na kuhakikisha wale wastaafu wanapata kile kilicho chao sasa kazi kubwa ni kutoa elimu.” Amefafanua Dkt, Abassi


Aidha Dkt. Abbasi alitoa wito kwa wastaafu na wale wastaafu watarajiwa kutambua kuwa msingi wa pensheni ni kumuhudumia mfanyakazi anapokosa nguvu ya kufanya kazi, ama uzeeni au kutokana na kupata madhara mengine ambayo yatafanya akose nguvu ya kufanya kazi.


“Niwakumbushe watanzia kuwa tuweke pesa benki zile tunazohitaji kutumia leo, kesho au katika kipindi kifupi, lakini mafao ni kwa ajili ya kukusaidia katika maisha ya baadaye, si vema umetumikia nchi, jamii halafu baada ya kustaafu ukaishi maisha ya mashaka.” Aliasa.


Awali Meneja Kiongozi Uhusiano na Elimu kwa Umma wa PSSSF, Bi. Eunice Chiume alimweleza Dkt. Abassi kuwa amepata fursa ya kutembelea vyombo vya habari ili kujenga na kuendeleza mahusiano ikiwa ni pamoja na kuutambulisha Mfuko huo mpya kwa wadau wa sekta ya habari.


Alisema Mfuko ulianza kutekelez amajukumu yake Agosti 1, 2018 na ndani ya miezi 6 tangu Mfuko uanze kutekeleza majukumu hayo umeweza kulipa malimbikizo ya pensheni ya mkupuo na ile ya kila mwezi kiasi cha shilingi bilioni 880, lakini pia Mfuko unaendelea na zoezi la kuhakiki taarifa za wanachama (wastaafu) ambapo kati ya wastaafu 120,000, elfu 10,000 bado hawajahakikiwa.


“Kwa hiyo tumeeleza kuwa Mfuko umefungua ofisi nchi nzima bara na visiwani na kwa kila mstaafu ambaye bado hajahakiki taarifa zake afike kwenye ofisi ya PSSSF iliyo karibu naye ili atekeleze wajibu huo wa kisheria.” Alifafanua Bi. Chiume.


Msemaji Mkuu wa serikali ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo, Dkt. Hassan Abbasi, (kushoto), akipeana mikono na Meneja Kiongozi Uhusiano na Elimu kwa Umma, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, (PSSSF), Bi. Eunice Chiume baada ya mazungumzo yao ofisini kwa Dkt. Abassi jijini Dar es Salaam Bi. Chiume ambaye alikuwa katika ziara ya kuvitembelea vyombo vya habari ikiwemo mitandao ya kijamii jijini Dar es Salaam, amehitimisha ziara hiyo kwa kufanya mazungumzo na Dkt. Abassi.