Monday, April 1, 2019

MAGAZETI YA LEO TAREHE 01 APRILI 2019.

Dkt Kikwete: Watoto wenye usonji wanastahili kupendwa, kuthaminiwa kama wengine msiwafiche ndani










Na Selemani Magali
Rais  mstafu wa awamu ya nne, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amewataka jamii, walezi na wadau kuwapenda, kuwajali na kuwathamini watoto wenye ugonjwa wa usonji, akisisitiza kuwa kufanya hivyo kutasaidia kuwapa furaha.

Dkt Kikwete amesema watoto wenye matatizo ya usonji (Autism) wapo sawa na watoto wengine kinahitajika ni malezi yenye upendo kutoka kwa jamii ili nao wajihisi wako sawa na watoto wengine hapa Nchini.

Dkt Kikwete ametoakauli hiyo mapema hii leo wakati akizungumza katika viwanja vya shule ya AL-MUNTAZIR baada ya matembezi kwa ajili ya kueneza uelewa kwa jamii kuhusu umuhimu wa kuwapenda watoto wenye ugonjwa wa usonji kwani nao ni watu kama wengine ambao wanaweza pewa fursa ya  kushiriki kwenye shughuli mbalimbali za kijamii.

Watoto wenye hali ya usonji wana shida katika kuwasiliana na tabia zao ni kurudia rudia mambo anayofanya mara kwa mara na pia watuwengi wenye ugonjwa huu wananamna yao ya kujifunza, kusikiliza na kuitika.

“Mfano wa hali hii ni kwamba katika hali ya kawaida, mtoto wa mwaka mmoja hutabasamu au kuwa na furaha kila wakati, huiga mambo mbalimbali anayoona na kufuatilia vitu anavyoviona vikisogea, lakini mtoto mwenye ugonjwa huu hafanyi vitu hivi.

 Wadau wanasema Kukosa uelewa wa hali hii ya watoto wenye mahitaji huwafanya walimu na wazazi kudhani watoto ni watundu, wavivu au wanakera na wakati mwingine huadhibiwa kwa sababu hiyo wakati kwamba watoto hawa wanahitaji uangalizi wa karibu, kupendwa na kupata msaada kutoka kwa walimu na wenzao.

Sunday, March 31, 2019

KAZI YA KUREJESHA UMEME MLANDIZI PWANI YAENDA VIZURI.

Image may contain: 4 people, people standing, shoes and outdoor
Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga ameeleza kuridhishwa kwake na kazi kubwa iliyofanywa na TANESCO ya kuhakikisha kuwa maeneo yote yaliyokosa umeme kutokana na kuungua kwa transfoma ya Mlandizi yanapatiwa Umeme katika kipindi kifupi.


Hayo yalibainika wakati alipofanya ziara ya kukagua Kituo cha kupoza umeme cha Mlandizi mkoani Pwani kilichopata hitilafu tarehe 30/3/2019, majira ya Saa 1:50 asubuhi baada ya Transfoma katika kituo hicho kuungua na moto.


Akitoa maelezo kwa Kamishna, Naibu Mkurugenzi Mtendaji anayesimamia mifumo ya Usafirishaji umeme kutoka TANESCO, Mhandisi Isaack Chanji, alieleza kuwa, maeneo yaliyoathirika na tukio hilo ni pamoja na Mlandizi yote, baadhi ya maeneo ya Chalinze, Kibaha, Kibamba, Mbezi kwa Msuguri na Kimara. 


Hata hivyo, maeneo yote hayo yalipatiwa Umeme kupitia vituo vya Ubungo, Chalinze na Mlandizi chenyewe baada ya kukamilisha matengenezo ya dharura.


Kamishna Luoga aliwataka Wataalam kufanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha kazi ya ukarabati wa Transformer ya akiba yenye uwezo wa MVA 10 iliyopo katika Kituo hicho ifikapo tarehe 2/4/2019 ili kuhakikisha umeme wa uhakika unapatikana katika viwanda vilivyopo Kibaha pamoja na Mitambo ya maji ya Ruvu Chini na Ruvu Juu.


Aidha, aliitaka TANESCO kushirikiana na Kikosi cha Zimamoto cha Mkoa wa Pwani ili kufanya uchunguzi wa chanzo cha moto huo pamoja na kuweka mikakati ya kuhakikisha tatizo hilo halitokei tena.


Katika ziara hiyo, Mhandisi Luoga alikagua Kituo pamoja na kuongea na Wataalam wanaofanya kazi ya matengenezo katika kituo hicho akiwemo Mhandisi Mkuu wa Mkoa wa Pwani.

WASICHANA 4,000 MKOA WA LINDI KUFIKIWA NA MRADI WA LISHE KWA WATOTO WA KIKE.

NA HADIJA HASSAN-LINDI

JUMLA ya Wasichana elfu 4000 kutoka Halmashauri ya manispaa ya Lindi na Nachingwea Mkoani Lindi wanatarajiwa kufikiwa na Mradi wa lishe kwa watoto wa kike (GIRLS POWERD NUTRITION) unaoendeshwa na  World Association of girls guide and girl scouts 


Hayo yameelezwa na Meneja wa Mradi huo  David Mbimila  leo Machi 31, 2019 wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kuwajewajengea uwezo wa usimamizi wa Mradi huo kwa Viongozi wa Girl Guide wa Manispaa ya Lindi


Mbumila alisema Mradi huo wa Lishe kwa watoto wa kike Duniani unafanyika kwa majaribio  katika Nchi tano ikiwemo Tanzania, Bagladesh, Sirilanka, Filipino na Madagaska


"kwa Tanzania Mradi huu unatekelezwa katika Mikoa sita ikiwemo Mkoa wa Dar-es-salaam, Tanga , Arusha, Lindi , Dodoma pamoja  na Mkoa wa Mara ambapo kwa Mkoa wa Lindi kwa kuanzia tutaanza na Halmashauri ya Manispaa ya Lindi pamoja na Wilaya ya Nachingwea ambapo matarajio yetu ni kuwafikia wasichana elfu nne mpaka ifikapo 2020" alifafanua Mbimila


Mbimila aliyataja malengo makuu ya Mpango huo kuwa ni kutoa Elimu ya Lishe kwa watoto wa kike ili waweze kula vizuri, kukua vizuri, kuongeza nguvu kazi ya kitaifa


Alitaja malengo mengine ni kutaka kuishahuri Serikali kuweka Mada ya Lishe kwa Watoto wa kike katika vikao na mikutano yao wanayoifanya mara kwa mara , pamoja na kulipa kipaumbele swala la lishe kwa  Mtoto wa kike katika Sera na Sheria Mbali mbali ambazo wanazitengeneza


Nae kamishina wa Girls Guide Mkoa wa Lindi Grecy Chipanda alisema kuwa kati ya wasichana hao elfu 4000 watakaonufaika na Mradi  huo wasichana 2700 watatoka Halmashauri ya Manispaa ya Lindi huku 1500 watatoka Wilayani Nachingwea


"unaweza ukajiuliza ni kwanini Wasichana wengi wametoka Manispaa hii ni kwa sababu Viongozi wengi wa Mkoa tuko hapa , kwa hivyo bira shaka kwa kushirikiana kwa pamoja na viongozi wa Wilaya tunaweza kuunganisha nguvu zetu na kufanikisha mpango huu kufanyika vizuri" alisema Chipanda


Nae Mwenyekiti wa Girls Guide Mkoa wa Lindi Mwalimu mstaafu Zuhura Mohamedi alisema kuwa Baada ya mradi  huo wa Lishe kwa watoto wa kike  wa majaribio kumalizika mwaka 2020 matarajio yake ni kuona wasichana Wanashiriki kikamilifu katika masomo yao pasipokukosa kuhudhuria Darasani 


Alisema matarajio yao mara baada ya kumaliza kwa warsha hiyo walimu pamoja na viongozi wa girls guide walioshiriki mafunzo hayo wataenda kuwaelimisha wanafunzi pamoja na jamii kwa ujumla umuhimu wa kula chakula chenye lishe bora ili kumaliza changamoto zinazowakuta wasichana hasa wa umri kuanzia miaka 6 hadi 19 


Awali akifungua warsha  hiyo ya siku nne katibu tawala , utawala na rasilimali watu wa Mkoa wa Lindi  DKT Bora Haule alisema kuwa kama Mkoa wamefarijika kuona Mkoa wao ni miongoni mwa Mikoa sita inayotekeleza mradi huo, huku akieleza kwamba Mradi huo utakuwa unaunga mkono jitihada zinazofanywa na mkoa huo za kuongeza ufaulu kwa Watoto wakike sambamba na kutokomeza  mimba za utotoni kupitia kampeni ya "TUMSAIDIE AKUE, ASOME, MIMBA BAADAE"


Pamoja na mambo mengine Dkt Bora pia aliwataka washiriki wa Mafunzo hayo kwenda kuwajibika kikamilifu katika maeneo yao sambamba na kuwataka Wananchi wa Manispaa ya Lindi na wa Wilaya ya Nachingwea kuupokea mradi huo pamoja na kuwapa ushirikiano wa kutosha waratibu wakati wa kutekuleza Mradi huo