Sunday, January 20, 2019

CHRISTAFARI WATOA UJUMBE SOBER HOUSE BAGAMOYO.

 Mkurugenzi wa kituo cha Life and Hope ''Sober House Bagamoyo'' Al-karim Sadrudin Bhanji,(kushoto) akifafanua jambo mara baada ya kuwapokea wageni wake ambao ni kundi la CHRISTAFARI kutoka Mareknai
 ....................................

Waimbaji wa nyimbo za injili kundi la CHRISTAFARI kutoka Mareknai wametembelea Kituo cha Life and Hope ''Sober House Bagamoyo'' kilichopo Bagamoyo Mkoa wa Pwani nchini Tanzania ili kubadilidhsna mawazo na vijana wanaopata malezi katika kituo hicho.


Wakiwa katika kituo hicho wameweza kutuo ushuhuda wao jinsi madawa ya kulevya yanavyomuathiri mtumiaji kiasi cha kupoteza utu wake, heshima mbele ya jamii, na wakati mwingine kupoteza maisha.
Wamesema dawa za kulevya zinastahili kupigwa vita kote duniani ili kunusuru kundi la kubwa la vijana ambalo limetumbukia kwenye matumizi ya dawa hizo.


Msafara huo wa vijana kutoka nchi mbalimbali ambao kwa pamoja wanatumia nyimbo kufikisha ujumbe kwenye jamii wamesema kila binadamu ni mwenye kufanya makosa lakini ni vizuri unapogundua kuwa umekosea ukajirekebisha na kuacha lile kosa ambalo umeligundua.


Kijana Makes kutoka nchini Marekani amesimulia kisa chake cha kutumia dawa za kulevya na kusema kuwa alianza kidogo kidogo kwa kushawishiwa na rafiki yake mpaka akazoea.


Alisema katika matumizi yake ya dawa za kulevya alijikuta amepoteza ubinadamu kiasi cha kujihisi kama amekaribia kupoteza uhai wake.
Anasimulia kuwa kuanzia hapo alipata ujasiri wa kuacha matumizi ya dawa za kulevya na hatimae kujiunga na kundi la CHRISTAFARI ili kufikisha ujumbe wake 


Akiendelea kutoa nasaha kwa vijana wa Kituo cha Life and Hope ''Sober House Bagamoyo'' Makes alisema njia pekee ambayo vijana kote duniani itawasaidia ni kumrudia Mungu wao ili waishi katika maadili mema ya kumjua muumba wao sambamba na kusikiliza ushauri wa wazazi.


Alisema ukiamua kurudi kwa Mungu wako basi Mungu atakusaidia kufikia lengo kwani kupoteza nguvu kazi ya vijana ni hasara kwa familia na taifa kwa ujumla.


Kwa upande wao vijana wanaopata malezi katika kituo cha Life and Hope ''Sober House Bagamoyo'' wamesema wanaamini nia waliyonayo itapokelewa na Mungu na hatimae nao watakauwa miongoni mwa watanzania wenye kutoa mchango kwa taifa lao.


Walisema hakuna aliyetaraji kufika hapo walipofika bali nguvu za shetani zilichukua nafasi yake kiasi kujiona wao wajanja hali ya kuwa wanapotea.


Wametoa wito kwa jamii kutumia busara na hekina katika kuwarekebisha vijana walioathirika na dawa za kulevya huku wakiwataka vijana kujitafakari katika yale wanayofanya ili wasije kujuta hali yakuwa wamepoteza nguvu na baadhi ya viungo.


Awali akiwakaribisha wageni hao Mkurugenzi wa kituo cha Life and Hope ''Sober House Bagamoyo'' Al-karim Sadrudin Bhanji, alisema kituo hicho kinatoa huduma kwa vijana walioathirika na aina zote za dawa za kulevya ili kuijenga jamii iwe na watu wenye nguvu za kufanya kazi.


Alisema licha ya changamoto wanazokumbana nazo kama kituo wameweza kufanikiwa kutoa vijana wengi ambao kwa sasa wameungana nafamilia zao wakiwa watu wema wenye kufanya kazi.


Aliongeza kwa kuwataka wadau mbalimbali ndani na nje ya nchi kujitokeza kusaidia kituo hicho ili kiweze kutoa huduma kwa ufanisi zaidi.


Alisema wapo vijana ambao tayari wametengwa na ndugu zao na wanakimbilia katika kituo hicho kuomba msaada hali inayowalazimu kuwapokea bila ya kujali gharama za kuwahudumia.
 
 Makes kutoka nchini Marekani, akielezea madhara ya dawa za kulevya walipotembelea katika cha Life and Hope ''Sober House Bagamoyo'' hivi karibuni.

   
 Mkurugenzi wa kituo cha Life and Hope ''Sober House Bagamoyo'' Al-karim Sadrudin Bhanji, akiwa katika picha ya pamoja na kundi la CHRISTAFARI kutoka Mareknai

Saturday, January 19, 2019

WAZIRI MKUU KUWAPOKEA WATALII 300 KUTOKA CHINA

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Kampuni  ya Touchroad Group ya China, Bw. He Liehui, ofisini kwa Waziri Mkuu, jijini Dodoma, Januari 19, 2019.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza  na Mwenyekiti wa Kampuni  ya Touchroad Group ya China, Bw. He Liehui, ofisini kwa Waziri Mkuu, jijini Dodoma, Januari 19, 2019.

Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
.........................................


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameahidi kupokea kundi la watalii wasiopungua 300 ambao wanatarajiwa kuwasili nchini Machi, mwaka huu.


Watalii hao ni kundi la kwanza miongoni mwa watalii 10,000 wanaotarajiwa kuwasili nchini katika mwaka 2019 chini ya mpango unaosimamiwa baina ya Wizara ya Maliasili na Utalii, Bodi ya Utalii Tanzania na kampuni ya TouchRoad International Holding Group ya China.


Ametoa ahadi hiyo leo (Jumamosi, Januari 19, 2019) alipokutana na Mwenyekiti wa Touchroad Group, Bw. Liehui He na Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii, Jaji Thomas Mihayo ofisini kwake Mlimwa, jijini Dodoma.


Waziri Mkuu amefikia uamuzi huo baada ya kuelezwa na Bw. He huyo kwamba kundi hilo la watalii likiwa Djibouti litapokelewa na Waziri Mkuu wa nchi hiyo na likienda Zimbabwe, litapokelewa na Rais wa nchi hiyo.


“Tanzania imeamua kuweka mkakati wa kuongeza idadi ya watalii nchini kwa kuboresha miundombinu ya usafiri na kukuza utalii kupitia vivutio vya vyakula vya asili, mavazi ya asili, wanyama, fukwe za bahari na milima. Kwa hiyo, ujio wa kundi hili kubwa, unatoa fursa mpya ya kutangaza vivutio vya nchi yetu,” amesema.


“Nitoe wito kwa Watanzania wanaoishi maeneo ya jirani na vivutio vyetu, wachangamkie fursa ya ujio wa watalii hawa katika maeneo mbalimbali. Wakifika Dar es Salaam, wanaweza kwenda Kigoma kuona Ziwa Tanganyika, mbuga zilizoko Nyanda za Juu Kusini, Arusha au vivutio vya Zanzibar. Tujiandae, tuwe tayari kuwauzia bidhaa mbalimbali,” amesema.


Pia amesema amefurahishwa na wazo lao la kuifanya Dar es Salaam iwe kitovu cha utalii (tourist hub) kwa makundi ya watalii ambayo yatakuja Tanzania na baadaye kutoka Tanzania kwenda Lusaka, Harare, Johannesburg na Djibouti.


Mwenyekiti huyo ambaye aliwasili nchini juzi, ameambatana na ujumbe wa watu 31 ambao unajumuisha waandishi wa habari, wasanii, wanamuziki na watu mashuhuri.


Akiwa Beijing, China, wakati akishiriki mkutano wa Jukwaa la Biashara baina ya Tanzania na China lililofanyika Septemba mwaka jana, Waziri Mkuu alikutana na uongozi wa kampuni ya TouchRoad ambayo ilionesha nia ya kutangaza fursa za utalii zilizopo hapa nchini.


Ziara ya Bw. He ni sehemu ya utekelezaji wa makubaliano yaliyoingiwa kati ya kampuni ya TouchRoad na Bodi ya Utalii ya Tanzania, Novemba 2018.


Mapema, Bw. He alimweleza Waziri Mkuu nia ya kampuni hiyo kutekeleza makubaliano yao ya kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania katika soko la China ili kuvutia watalii wapatao 10,000 waitembelee Tanzania katika mwaka 2019.


“Tumepanga kuleta watalii 10,000 kwa mwaka huu wa 2019 na tumeweka lengo la kuongeza idadi hiyo kwa asilimia 20 kila mwaka kwa muda wa miaka mitano. Pia tuna lengo la kuitumia ndege ya ATCL ili ilete watalii moja kwa moja kutoka Shanghai, China,” alisema.


Akielezea ujio wa kundi la kwanza la watalii, Bw. He alisema kundi hilo litakaa Djibouti kwa siku moja, Tanzania siku nne (tatu za kulala) na Zimbabwe siku tatu (mbili za kulala) na kisha kurejea China.


Alisema wanapanga kila mwezi wawe na kundi kubwa la watalii ambao watakuwa wanafikia Tanzania na kupelekwa nchi nyingine kwa sababu Wachina wengi hupenda kufanya utalii kwa siku walau 10, lakini wapelekwe maeneo matatu au manne tofauti kuona vivutio vya aina nyingine badala ya kukaa sehemu moja kwa kipindi chote hicho.


“Watalii hawa wakija kwa siku tatu au nne, wana uhakika wa kutumia dola za Marekani zaidi 2,000, wakienda eneo jingine watatumia fedha pia, namna hiyo tuna uhakika wa kuongeza pato la Taifa, lakini pia tuna uhakika wa kutengeneza ajira kwa Watanzania,” alisema.