Friday, November 2, 2018

MAJALIWA ATEMBELEA VIWANDA JIJINI TANGA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kuhusu uzalishaji wa saruji  kutoka kwa Bw. Pradeep Punlana  (katikati) ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha saruji cha  Rhino kilichopo eneo la Maweni jijini Tanga  wakati alipotembelea kiwanda hicho  Novemba 1, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Soni wilayani  Lushoto akiwa katika ziara ya mkoa wa Tanga, Novemba 1, 2018

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kuhusu uzalishaji wa saruji  kutoka kwa Bw. Pradeep Punlana  (katikati) ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha saruji cha  Rhino kilichopo eneo la Maweni jijini Tanga  wakati alipotembelea kiwanda hicho  Novemba 1, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama usindikaji wa maziwa wakati alipotembelea kwanda cha Maziwa cha Tanga Fresh cha jijini Tanga, Novemba 1, 2018.  Kushoto ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, watatu kushoto ni Meneja Ufundi wa kiwanda hicho, Adam Gamba na wanne kukhoto ni Meneja Mkuu wa kiwanda, Michael Karata. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

DC KIBAHA ATOLEA UFAFANUZI MAKAMU WA RAIS KUKATAA KUZINDUA STENDI YA MAILI MOJA.

MKUU wa wilaya ya Kibaha  ,Assumpter Mshama akizungumza na waandishi wa habari , wakati akitolea ufafanuzi masuala mawili ambayo makamu wa Rais Samia Suluhu aliyagusia kwenye ziara yake aliyoifanya wilayani humo,mwishoni mwa wiki iliyopita.
.................................................

NA MWAMVUA MWINYI, PWANI

MKUU wa wilaya ya Kibaha  ,Assumpter Mshama, atolea ufafanuzi juu ya hatua ya makamu wa Rais ,Samia Suluhu ,kukataa kuzindua stendi mpya ya Mailmoja ambapo amesema yeye alishaweka hofu kuupokea mradi huo tangu kipindi cha nyuma “;na mhandisi wa halmashauri ya Mji wa Kibaha ndio aliyewafikisha hapo.

Aidha amemuagiza mkurugenzi wa halmashauri ya Kibaha Vijijini ,kumsimamisha cheo ofisa manunuzi na ugavi, Peter Mboje kwa madai ya kutumia vibaya ofisi yake kujipatia fedha kinyume na utaratibu.

Aliyasema hayo kwa waandishi wa habari , wakati akitolea ufafanuzi masuala ambayo Samia aliyagusia kwenye ziara yake aliyoifanya wilayani humo,mwishoni mwa wiki iliyopita.

Assumpter alisema yeye anaungana na makamu wa Rais kujiridhisha kwanza na uchunguzi.

Alisema alishakataa utekelezaji wa mradi huo na kuomba usipitiwe kuzinduliwa kwakuwa una baadhi ya kasoro na hauendani na thamani ya bilioni 3.2

Assumpter alibainisha,kutokana na hofu hiyo na malalamiko kutoka kwa wananchi alihitaji apatiwe ripoti ya gharama za ujenzi ambayo mhandisi wa mji huo alikaidi na hajampatia hadi sasa .


“Nilimwambia alikaidi, sina mamlaka ya kumfanya chochote  ,acha tuone uchunguzi unaleta majibu yapi ili kujiridhisha na kuondoa minong’ono kwa wananchi ” 

“Serikali hii ni sikivu ,ukiona wananchi wanasema sema inabidi kufanyia kazi suala wanalolalamikia ,tusipuuzie minong’ono ya watu kikubwa tuwe tunaifanyia kazi “alisema Assumpter.

Alitoa wito kwa wakurugenzi wa halmashauri zote hizo mbili, wakipewa ushauri wausikilize na wafanye nae kazi kama timu moja.

Akizungumzia sakata la ofisa manunuzi ,alisema , anaviachia vyombo vyake vya ulinzi na usalama kuchunguza juu ya tuhuma zinazomkabili mtumishi huyo ndani ya siku 14 kuanzia sasa.

Assumpter alieleza ,ofisi yake imefuatilia na kupata ushahidi wa watu watano wa awali ndipo ameamua kuchukua maamuzi hayo.

Alielezea ,Mboje anadaiwa kutumia nafasi yake kuomba fedha kwa wakandarasi wa ujenzi wa mradi wa upanuzi wa kituo cha afya Mlandizi ,akiwadanganya ametumwa fedha na mkurugenzi wa halmashauri ,hali inayosababisha kusuasua kwa mradi.

“Hakuna haja ya kumsubiri Samia ,nimefuatilia na kubaini ametumia madaraka yake vibaya ,” Mfano tumepata taarifa zake anasumbua mjenzi wa jengo la OPD na fundi wa jengo la upasuaji”alifafanua Assumpter .

Assumpter alisema ,uchunguzi ukikamilika na kubaini ametenda kosa hilo ,sheria itachukua mkondo wake.

WAZIRI KALEMANI ATAKA MKOA WA PWANI KUAINISHA MAENEO YA UWEKEZAJI WA VIWANDA ILI KUBORESHA MIUNDOMBINU YA NISHATI.

WAZIRI wa Nishati Dkt Medard Kaleman

Na Grace Semfuko-MAELEZO

WAZIRI wa Nishati Dkt Medard Kaleman, ameuagiza uongozi wa Serikali ya Mkoa wa Pwani kuainisha maeneo yote kwa uwekezaji wa viwanda ili kuharakisha miundo mbinu ya nishati ya umeme utakaosaidia kuhamasisha wawekezaji na hivyo kusaidia kukuza uwekezaji wa viwanda.

Dkt. Kalemani ameyasema hayo alipotembelea maonesho ya bidhaa za viwandani katika Viwanja vya Sabasaba vilivyopo Picha ya Ndege, Wilaya ya Kibaha Mkoani  Pwani, akasisitiza kuwa wakati Serikali ya awamu ya tano inaweka mikakati ya kuhakikisha kunakuwa na viwanda vya kutosha kuinua uchumi wa Taifa watendaji wa Serikali hiyo hawana budi kuimarisha miundombinu yake na kupanua fursa.

“Mkoa wenu huu wa Pwani ni Mkubwa na wenye ardhi na rasilimali za kutosha kabisa, ainisheni maeneo ya uwekezaji na mtuambie tuje kuweka miundombinu ya nishati, sisi tutafanya kazi hiyo haraka, kwani tunataka uwekezaji uwe mkubwa ili Nchi yetu iweze kupata manufaa makubwa kiuchumi” alisema Dkt. Kalemani.

Pia Waziri Dkt Kalemani amewataka wawekezaji nchini kuongeza bidii katika kujenga viwanda vya uzalishaji wa bidhaa mbalimbali ili kuwawezesha Watanzania kupata ajira pamoja na kuiingizia Serikali pato kutokana na kodi mbalimbali za uuzwaji wa bidhaa hizo.

Waziri huyo pia ametoa wito kwa viongozi wa mikoa mbalimbali nchini kutenga maeneo ya uwekezaji ili kuwawezesha wawekezaji kutoka katika mataifa mengine kuja kuwekeza bila kuwa na vikwazo vya kiuchumi.

Pia Waziri Kalemani  amesema katika kukabilina na changamoto za miundo mbinu ya nguzo za miti kwa ajili ya Umeme kuharibika hususani katika maeneo yenye maji mengi amewataka wadau wanaotengeneza nguzo za umeme za zege kuboresha bidhaa hiyo ili ziweze kuingia katika ushindani na hatumaye ziweze  kupata masoko zaidi.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo amesema Mkoa wake unafanya kila jituhada za kuhakikisha miundombinu rahizi inafikika kwenye maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya viwanda na kuwaagiza watendaji katika Halmashauri zote kutenga maeneo ya uwekezaji.

“ Sisi Mkoa wa Pwani tunayo maeneo ya kutosha kabisa katika uwekezaji, na tunafanya kila jitihada za kuhakikisha miundombinu rahisi ikiwepo ya Barabara,Maji na Umeme inafikika ili viwanda vijengwe na vianze uzalishaji wa bidhaa mara moja” alisema Mhandisi Ndikilo.

Nae Meneja  wa kiwanda kinachotengeenza nguzo za umeme za zege cha  East Africa Infrastructure Engineering Limited, JohnsPeter Majura amesema wameanza kuzalisha nguzo za umeme ili kuimarisha miundombinu ya umeme kwenye maeneo mbalimbali nchini.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Asumpta Mshama amesema Wilaya yake tayari imeanza kuvutia wawekezaji kwa kutenga maeneo ya uwekezaji ambayo tayari yameanza kupata wawekezaji kutoka katika mataifa mbalimbali duniani.

Maonesho ya bidhaa za viwandani katika Mkoa wa Pwani yalifunguliwa tare 29  ili kutangaza bidhaa mbalimbali za uwekezaji katika mkoa huo na yatafungwa Nov. 3, mwaka huu.

MAGAZETI YA LEO NOVEMBA 02, 2018