Sunday, October 28, 2018

MAMA SALMA AFURAHISHWA NA WAHITIMU WA SHULE YA MANDERA

 Mama Salma Kikwete akizungumza katika mahafali ya Shule ya Sekondari Mandera, kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya shule hiyo, Ramadhani Kabelwa na kushoto ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Rose Umila.
............................................

Na Omary Mngindo, Chalinze.

MKE wa Rais Mstaafu wa Serikali ya awamu ya Nne Mama Salma Kikwete, amefurahishwa na wanafunzi wasichana 49 waliomaliza elimu ya kidato cha nne katika shule sekondari ya Mandera, Kata ya Mandera, Halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo Mkoani  Pwani.

Alisema amefurahishwa na wasichana hao ambao wanamaliza sfari yao ya masomo bila ya kuwa na mimba hata mmoja.

Furaha ya Mama Salma ameitoa kwenye Mahafali ya saba shuleni hapo, ambapo alipoongozana na Mbunge mwenzake Hawa Ghasia wakiwa na mwenyeji wao Mwalimu Mkuu Rose Umila, huku akichukizwa na baadhi ya wazazi kutowalipia michango ya chakula watoto wao.

Alisema kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli alipotangaza elimu bure, alimaanisha hakutokuwepo na ada, na sio kwa huduma za mavazi na chakula awapo shuleni, na kwamba masuala hayo yanamhusu mzazi na mlezi mwenyewe.

Katika Mahafali hayo Mama Salma ambaye pia ni mlezi, amesimamia harambee iliyokusanya kiasi cha shilingi milioni 1,510,000, mwenyewe akichangia shilingi laki tano wakati Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akituma laki moja kupitia Mohamed Mzimba, ambapo Mama Salma aliwaomba wazazi kuhakikisha wanasimamia elimu kwa mtoto wa kike.

"Nimesikitishwa na taarifa ya Mwalimu Mkuu inayoeleza kuchelewa kwa baadhi ya wanafunzi baada ya likizo, sababu zikielezwa kipato kidogo cha wazazi, hali hii inakwamisha jihudi za mwalimu katika kufundisha, huku mwanafunzi kukosa kile alicholikikusudia," alisema Mama Salma.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo Ramadhani Kabelwa aliwataka wazazi na walezi kila mmoja aone umuhimu wa elimu kwa mtoto wa kike, huku akiongeza kwamba kumsomesha mtoto wa kike ni sawa na kuielimisha jamii.

Taarifa ya Mwalimu Mkuu Umila ameeleza kuwa shule hiyo inakabiliwa na changamoto kadhaa, ikiwemo ya uchakavu wa miundombinu shuleni hapo, sanjali na ukosefu wa mabweni pamoja na bwalo la chakula.

"Tunaishukuru halmashauri ya Chalinze kwa kutujengea tenki la maji, limesaidia kupunguza adha hiyo, pia Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu kwa mataulo ya vijana wetu, sanjali na kikosi cha Jeshi Kiangaiko kinasaidia mambo kadhaa," ilieleza sehemu ya taarifa ya Umila.

 Mama Salma Kikwete akizungumza katika mahafali ya Shule ya Sekondari Mandera, kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya shule hiyo, Ramadhani Kabelwa na kushoto ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Rose Umila.

 Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Rose Umila akisoma taarifa mbele ya mgeni Rasmi, Mama Salma Kikwete.

 
Mama Salma Kikwete akipokea Taarifa kutoka kwa Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Rose Umila
 
Mama Salma Kikweteakimkabidhi saa Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Rose Umila.
  
Diwani wa kata ya Mandera Madaraka Mbode wa kwanza kushoto.

MAMA SAMIA SULUHU AIPONGEZA CHALINZE KWA MIRADI YA AFYA

MAKAMU wa Rais Mama Samia Hasan Suluhu akizungumza katika Halmashauri ya Chalinze wakati wa ziara yake wilayani Bagamoyo, Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete.
........................................................ 
Na Shushu Joel,Chalinze.

MAKAMU wa Rais Mama Samia Hasan Suluhu ameipongeza halmashauri ya wilaya ya chalinze iliyoko wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani  kwa utekelezaji wake wa miradi bora ya Afya yenye lengo la kumaliza changamoto za hupataji wa huduma za kiafya kwa wakazi wa maeneo hayo.

Akizungumza na wananchi wa kata ya Lugoba mara baada ya kutembelea kituo cha afya cha lugoba kinachojengwa na serikali ya awamu ya tano,Mama Samia alisema kuwa chalinze ni mfano wa kuigwa kutokana na kile ambacho serikali imekuwa ikisisitiza kufanyika kwa wananchi wake basi chalinze kinafanyika kwa mifano na huu ndiyo utekelezaji wa ilani tulioubiri mimi na Raisi Magufuli wakati tunaomba kuungwa mkono.

“Nimejionea mwenyewe jinsi chalinze inavyotekeleza na kusimamia fedha za serikali kwa makusudi yale iliyokuwa ikiyahitaji yafanyike kwa wananchi wake inavyotekelezeka kwa vitendo kwenye halmashauri hiyo”Alisema Mama Samia Suluhu.

Aliongeza kuwa usimamizi unaofanywa na wasaidizi wa serikali kupitia mwakilishi wa wananchi mbunge wa jimbo hilo Ridhiwani Kikwete umekuwa ni wa tija katika kutambua thamani ya wananchi wao katika kuwafanikishia maendeleo.

Aidha Mama Samia Suluhu ametumia mkutano huo kuwataka wananchi wa chalinze na hasa kinamama kujijengea tabia ya kuwahi mapema katika vituo vya afya pindi wanapokuwa wajawazito ili kuweza kupata ushauri nasaha kutoka kwa wataalamu na kuacha tabia za kutumia miti shamba ambayoinaweza sababisha matatizo makubwa kwa wakina mama wakati wa kujifungua.

Pamoja na wito huo, Makamu wa Raisi aliwakumbusha Wananchi wa Halmashauri ya Chalinze kujiunga na mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa, kwani faida ya Mfuko huo ni kubwa sana. Mfuko wa Bima ya Afya utawawezesha wananchi kutibiwa hadi Hospitali kubwa za Rufaa, Jiungeni na fursa hii ili kulinda na kuhifadhi afya zetu.

Kwa upande wake mbunge wa jimbo hilo Ridhiwani Kikwete amempongeza Raisi Dr.John Pombe Magufuli na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu  kwa kutambua jitihada zinazofanywa na viongozi wa chalinze katika ufanikishaji wa miradi ya maendeleo hasa katika sekta ya afya,elimu,maendeleo ya jamii na maeneo mengine ya ustwi wa jamii.

Mheshimwa Kikwete, Alisema kuwa mpaka sasa jimbo la chalinze limejipanga kuhakikisha linawakamilishia maendeleo wananchi wake ili kuondoa changamoto zote zilizokuwa zikiwakabili kwani serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli imekuwa ikifanya mambo yake kwa vitendo na wakati.

“Mheshiwa Makamu Wa Raisi, halmashauri yetu inajenga zahanati zaidi ya 12 ambazo ziko katika hatua za mwisho zikielekea kukamilika. Mheshimiwa Kikwete, alizitaja baadhi ya Zahanati hizokuwa ni  Chahua,Visakazi,Ubenazomozi,Pingo,Lulenge, Magulumatale,Msigi, Mindukene,Mwetemo,Bago,Mandela na Dihozile” Alisema Kikwete.

Aidha mbunge huyo aliongeza kuwa kuna vituo vya Afya ambavyo pia vinaendelea kujengwa na serikali na vimekamilika kwa asilimia 90 mahususi kwa sababu ya kusaidia masuala ya Wanawake na Watoto na zimepewa na uwezo wa upasuaji ambavyo ni Kibindu, Miono, Lugoba, Chalinze na Msoga.Malengo yakiwa ni kuondoa kabisa vifo vinavyotokana na kutopatikana kwa huduma bora za Afya hasa kwa Wakina mama na Watoto katika jimbo la chalinze.

Mbunge huyo alitumia nafasi huyo kuwataka wananchi wa jimbo lake kutumia fursa walizozipata za kuwa na wingi wa vituo vya afya kuhakikisha wanakwenda kupatiwa matibabu katika sehemu zinazostahili na si kubaki majumbani na kupeana tiba za kienyeji.

Naye mkuu wa mkoa Eng Evarist Ndikilo   amemuhakikishia Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu kuwa halmashauri ya chalinze imekuwa kinara wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo kutokana na umoja wa viongozi wa eneo hilo.

Hivyo amempongeza mbunge wa jimbo hilo kwa jinsi anavyopambana na ufanikishaji wa miradi ya maendeleo kwa kutumia wafadhili mbalimbali hivyo wananchi wamtumie vizuri katika ufanikishaji wa maendeleo ya chalinze.