Friday, October 26, 2018

CCM YASHINDA KITI CHA MWENYEKITI WA HALMASHAURI MONDULI

CHAMA Cha Mapinduzi CCM kimeshinda kwa kishindo katika uchaguzi wa mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Monduli mkoani hapa baada ya aliyekuwa  mgombea wa wa nafasi hiyo kwa tiketi ya CHADEMA Rita Mona kujitoa kwenye kinyang’anyiro hicho.


Na Ahmed Mahmoud Arusha
 
Licha ya Rita diwani wa kata ya Monduli Mjini Issac Kopriano maarufu kwa jina la kadogoo alikuwa anawania nafasi hiyo kwa tiketi ya CCM.

Pia makamu mwenyekiti ameshinda kwa kishindo baada ya mpinzani wake Fadhili Mbwambo diwani wa kaya ya Majengo (CHADEMA)kujitoa ukumbini wakati akiomba kura.

Baada ya wagombea hao wawili kujito kwenye kinyang’anyiro hicho msimamizi wa uchaguzi huo ambaye pia ni mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Monduli Steven Ulaya alisema kwa mujibu wa kanuni lazima zipigwe kura za ndiyo na hapa.

Kufuatia agizo hilo madiwani wa 23 wa vyama vya CHADEMA na CCM walipiga kura ambapo madiwani tisa wa CHADEMA walimpigia Kadogoo kura za ndiyo na kuibuka na ushindi wa kishindo wa kura 23 kati ya kura zote 23 zilizopigwa.

Kwa upande wa nafasi ya  makamu mwenyekiti wa halmashauri CCM  ilishinda kwa kishindo baada ya diwani wa kata ya Naalarami  Edward Lenanu kupata kura 22 kati ya kura 23 zilizopigwa baada ya kura moja kuharibika.

Akizungumza mara baada ya kutangazwa mshindi Kadogoo aliishukuru CCM kwa kuendelea kumwamini na kumteua kugombea nafasi ya udiwani kwenye uchaguzi mdogo wa marudio ambapo alipita bila kupingwa na kufanikiwa kuwa diwani wa kata hiyo.

Kadogoo aliwataka wananchi,madiwani wa Monduli  pamoja na watumishi wa halmashauri ya Monduli kuweka tofauti zao pembeni na kusimamia ajenda moja tuu ya maendeleo.

“Niwaombe wana Monduli wimbo wetu wa kila siku uwe ni maendeleo popote tutakapokuwa ili tuweze kwenda na kasi ya rais Dk John Magufuli ya kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo ya dhati”.

TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) KUTOA HUDUMA YA KLINIKI YA MOYO INAYOTEMBEA MKOANI KAGERA

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera wanatarajia kutoa huduma ya kliniki ya Moyo inayotembea (Cardiac Mobile Clinic) katika Mkoa wa Kagera kuanzia tarehe 5 hadi tarehe 11 Novemba, 2018.

Huduma tutakazozitoa ni pamoja na upimaji wa vihatarishi vya Magonjwa ya Moyo, ushauri wa kiafya kuhusiana na Magonjwa ya Moyo, na kutoa rufaa kwa wananchi watakaokutwa na matatizo ya Moyo yanayohitajika kupewa rufaa kuja kwenye Taasisi yetu kwa uchunguzi wa tiba zaidi.

Matibabu ya kliniki ya moyo inayotembea ni matibabu endelevu yanayolenga kuhakikisha kuwa wagonjwa wa Moyo waliopo mikoani wanapata huduma bora ya matibabu ya Moyo na kuwa na elimu inayohusiana na magonjwa ya Moyo.

Wananchi wote wa Mkoa wa Kagera pamoja na mikoa ya jirani tunawakaribisha mfike katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera ili muweze kupata huduma za uchunguzi za matibabu ya Moyo.


MAJALIWA AKUTANA NA WAKUU WA MIKOA YA LINDI, MTWARA, PWANI NA RUVUMA NA VIONGOZI WA BODI YA KORSHO KUJADILI BEI YA KOROSHO

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na  Wakuu wa Mikoa  ya Lindi, Mtwara, Pwani na Ruvuma  ambao mikoa yao imeanza kuuza korosho, Wenyeviti wa Vyama Vikuu vya Ushirika na Watendaji Wakuu wa Bodi ya Korosho kwenye ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Oktoba 26, 2018. Kulia ni Naibu Waziri wa Kilimo, Omari Mgumba.

Washirki wa Mkutano ulioitishwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  uliowajumuisha Wakuu wa Mikoa  ya Lindi, Mtwara, Ruvuma na Pwani ambao mikoa yao imeanza kuuza korosho, Wenyeviti wa Vyama Vikuu vya Ushirika na Watendaji Wakuu wa Bodi ya Korosho wakimsikiliza Waziri Mkuu wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Oktoba 26, 2018. 

Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


WEMA SEPETU AFUNGIWA NA BODI YA FILAMU KWA MUDA USIOJULIKANA

Msanii Wema Sepetu kushoto akihojiwa na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bi.Joyce Fisoo kulia leo kutokana na vitendo vyake vya kurusha picha zisizo na maadili kwa jamii kwenye mitandao ya kijamii katikati ni Neema Ndepanya Msaidizi wa Wema Sepetu.

MAGAZETI YA LEO OKTOBA 26, 2018.