Thursday, October 25, 2018

IGP SIRRO AWATAKA WANANCHI WA UVINZA MKOANI KIGOMA KUENDELEA KUTOA TAARIFA SAHIHI ZITAKAZOFANIKISHA KUWAKAMATA WALIOJIHUSISHA NA MAUAJI YA ASKARI POLISI

Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akizungumza na wananchi (hawapo Pichani) wa Tarafa ya Nguruka wilayani Uvinza mkoani Kigoma Jana 24/10/2018, na kuwataka kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kufichua uhalifu na wahalifu pamoja na watu wanaojihusisha na matukio ya mauaji ili waweze kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akisalimiana na Mkuu wa wilaya ya Uvinza Mhe. Mwanamvua Mlindoko, wakati alipowasilia wilayani Uvinza Tarafa ya Nguruka mkoani Kigoma Jana 24/10/2018, kwa lengo la kuzungumza na wananchi kufuatia tukio la kushambuliwa na kuuawa kwa askari wawili na wingine mmoja kujeruhiwa wakati wakitekeleza zoezi la kuwaondoa wananchi waliovamia eneo la Ufugaji Ranchi ya Taifa NARCO kwa kuendesha shughuli za kilimo kinyume cha sheria na taratibu za nchi. 

Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akiondoka baada ya kumaliza mkutano na wananchi wa Tarafa ya Nguruka wilayani Uvinza mkoani Kigoma Jana 24/10/2018, ambapo IGP Sirro, aliwataka wananchi kuendelea kutoa taarifa sahihi zitakazofanikisha kukamatwa kwa watu waliojihusisha na tukio la kuwashambulia na kuwaua askari wawili na wananchi wawili wilayani humo. PICHA NA JESHI LA POLISI.

Dkt. ABBASI ATEMBELEA ETEMBELEA MAGAZETI YA CHINA.

Picha mbalimbali za ziara ya Msemaji Mkuu wa Serikali  Dkt. Hassan Abbasi na Ujumbe wake Beijing, China inaendelea ambapo ametembelea Vyombo vya Habari vya People’s Daily na China Daily.
.................................

Na Beatrice Lyimo- MAELEZO, CHINA

Mkurugenzi wa Idara ya Habari- MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi Jumatano Oktoba 24, 2018  ametembelea magazeti ya People’s Daily Online na China Daily nchini China  kwa lengo la kujifunza na kujadiliana namna bora zaidi ya kushirikiana katika sekta ya habari.

Akiwa katika vyombo hivyo,  Dkt. Abbasi amesema kuwa China na Tanzania zimekuwa na ushirikiano wa muda mrefu kwenye masuala mbalimbali hivyo ni muda sasa wa kufanyia kazi mkataba wa ushirikiano wa Tanzania na China kwenye masuala ya utamaduni na habari uliosainiwa mwaka 2016
“Lengo la ziara yetu ni kujifunza wenzetu mnavyofanya kazi na pia kutafuta namna ya kuweza kufanya kazi kwa pamoja katika sekta ya habari,” ameongeza Dkt. Abbasi akiwa People’s Daily.

Amelitaka gazeti hilo linalomilikiwa na Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na linalofikisha habari zake kwa  wasomaji milioni 700 duniani kupitia mitandao mbalimbali kuenzi ushirikiano huo wa muda mrefu kwa kuzipa nafasi pia habari za maendeleo za Afrika na Tanzania.

Kwa upande wake Meneja Mawasiliano wa Hifadhi za Taifa (TANAPA), Bw. Pascal Shelutete amewakumbusha viongozi wa chombo hicho kuzipa fursa habari za utalii hasa vivutio vingi vilivyoko Tanzania.

Akiwa katika gazeti la China Daily lililoanzishwa na Serikali ya China zaidi ya miongo mitatu iliyopita, Dkt. Abbasi aliwaeleza wahariri wanaohusika na toleo maalum la Afrika kuzingatia kuwa nchi nyingi za Afrika hasa Tanzania zina maendeleo na vivutio vya uwekezaji  vinavyopaswa kujulikana kwa wekezaji wengi wa China maombi ambayo wahariri wa gazeti hilo waliyakubali.

Dkt. Abbasi anaendelea na ziara yake ambapo atatembelea television za China za CCTV na CGTN na baadaye kufanya mahojiano na Idhaa ya Kiswahili ya Redio China.