Monday, October 22, 2018

RIDHIWANI KIKWETE AWATAKA VIJANA KUJIEPUSHA NA MADAWA YA KULEVYA.

Mbunge Ridhiwani Kikwete akimkabidhi  Cheti cha ufaulu bora wa somo la Dini Husein  Juma  katika mahafari ya shule ya Sekondari ya Chalinze.
........................

Na Shushu Joel,Chalinze.


VIJANA wengi nchini wamejikuta wakikumbana na changamoto nyingi katika utafutaji wa maisha katika jamii zao na kupelekea kundi lingine kujiunga katika matumizi hatari ya utumiaji wa madawa ya kulevya na hivyo hata  taifa kukosa vijana wa kuitumikia serikali yao.

Kukithili kwa vitendo vya uvutaji wa bangi vijiweni kunasababishwa na wazazi walio wengi kwa kutojenga tabia ya kuwakanya watoto wao pindi wanapokuwa wadogo na hata inapotokea watoto wao kupewa hadhabu ya viboko na walimu au watu wengine wazazi wamekuwa wakiwaijua juu wale waliojitokeza kuwakanya watoto hao.

  Akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Chalinze katika mahafari ya shule hiyo mbunge wa jimbo hilo Ridhiwani Kikwete amewataka vijana kutokaa vijiweni na watu walioshindikana kwani watawashawishi vibaya na hata kuwataka waweze kujiunga katika makundi ambayo si mazuri.

Alisema kuwa vijana wengi wamekuwa wakishawishiwa na watu wenye nia mbaya na vijana ili kuwaona tu na wao wanaharibika kwa kufuata matendo mabaya wanayoyafanya kwenye mitaa ikiwemo ubakaji,uvutaji wa madawa ya kulevya na hata kwenye wizi.

Kikwete aliongeza kuwa serikali inawategemea kwa kiasi kikubwa ili muweze kuja kuisaidia katika Nyanja mbalimbali pindi mtakapokuwa wakubwa kwani uongozi ni mchezo wa kupokezana.

“Mimi mbunge wenu nawahakikishieni serikali ya awamu ya tano imekuwa imejiwekea mikakati mikubwa ya kuhakikisha vijana wote wanamaliza masomo yao na wanafaulu ni lazima waende shule bila cha kusingizia kukosekana kwa ada,hivyo nawatakeni wanafunzi wote katika jimbo la chalinze kuhakikisha kila mmoja wenu anafaulu ili kuja baadae kuisaidia serikali na Taifa kwa ujumla.

“Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli imrvutakila aina ya michango mashuleni kwa madhumuni ya kuona watoto wanapata elimu ya kutosha pia kuongeza ufaulu kwa watoto” Alisema Kikwete.

Shaabani Husein ni mmoja wa wahitimu katika shule hiyo alisema kuwa  anampongeza mbunge wa jimbo hilo kwa mchango mkubwa anaoufanya kwa vijana wa shule hiyo kwa lengo la kuhakikisha vijana wanasoma kwa bidii bila matatizo ya aina yeyote ile.

Aliongeza kuwa ushauri uliotolewa ni mkubwa sana hivyo tunamuhakikishia mbunge kuwa hakuna kijana atakaye potea katika na kujiingiza katika  mambo maovu ya uvutaji wa bangi,wizi na utumiaji wa madawa ya kulevya kutokana na wengi wetu kutambua madhara yake.

Aidha alisema kuwa wazazi walio wengi wamekuwa wakichangia watoto kujiingiza katika utumiaji wa madawa ya kulevya kutokana na kutokutumia muda wao wa ziada kutuelimisha majumbani kwetu na badala yake kazi kubwa kuwaachia walimu tu.

Naye Mriamu Patrik alisema kuwa madawa ya kulevya yanachangia kwa kiasi kikubwa  kupoteza nguvu kazi ya vijana wetu ambao mara baada ya kujidunga madawa hayo ulala tu hivyo kupelekea watu hao kutokuwa na nguvu za kufanya kwani miili yao uzoefu.

“Nampongeza mbunge Ridhiwani Kikwete kwa ushauri alioutoa kwa vijana juu ya kutambua jinsi gani ijana na kumhakikishia kuwa vijana hao wa shule hiyo wanazingatia kila ushuri wa viongozi wao wa dini na wale wa serikali kwani wanahitaji tuwe kwenye maisha yanayositahili”Alisema
Kwa upande wake mkuu wa shule hiyo Emanuel Kahabi  amewapongeza wanafunzi wake wanaotarahiwa kufanya mtihani wa kidato cha nne mwaka huu kwa nidhamu kubwa wanayoionyesha shuleni na mitaani hii ni kutokana na ushirikiano mkubwa uliopo kati ya walimu na wazazi katika kuwajengea watoto hao maisha yao ya baadae.

Aliongeza kuwa wanafunzi watakao maliza kidato cha nne mwaka ni 307 hivyo kulingana na vile walivyowaandaa wanatarajia matokeo mazuri yatakayofurahisha zaidi ya mwaka jana.

Aidha amempongeza mbunge wa chalinze Ridhiwani Kikwete kwa misaada mbalimbali anayoitoa katika shule hiyo kwa lengo la kuhakikisha shule hiyo inakuwa miongoni mwa shule za kisasa na za kuvutia katika jimbo lake.

“Mbunge wetu katusaidia vitu vingi katika kuhakikisha shule hii inakuwa ya kipekee kwani katuwesheza komputa,mabati,saruji,mbao na vitu vingine vingi nab ado anaendelea kutusaidia kweli huyu ni kiongozi wa kipekee sana” Alisema mkuu wa shule hiyo.
Mbunge wa Ridhiwani Kikwete akisisitiza jambo kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Chalize ambapo alikuwa mgeni rasmi katika mahafari ya shule hiyo.
Mbunge Ridhiwani Kikwete akimkabidhi  Cheti cha ufaulu bora wa somo la Kiswahili mmoja wa wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Chalinze katika Mahafari
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari wakiwa na nyuso za furaha huku wakimsikiliza mgeni rasmi katika Mahafari hayo.

HALMASHAURI ZATAKIWA KUFANYA UTAFITI WA WAKANDARASI KABLA YA KUWAPA KAZI.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo, Sophia Kizigo (kulia) na wataalamu katika chanzo cha mradi wa Milonde, Namtumbo, mkoani Ruvuma.
.................................
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa ameziagiza Halmashauri zote kufanya utafiti wa kina kwa wakandarasi kabla ya kuingia nao mikataba ya ujenzi wa miradi ili kuweza kumaliza tatizo la utekelezaji mbovu wa miradi ya maji nchini.

Alisema tatizo la miradi mingi ya maji kwenye Halmashauri linatokana na kuwapa wakandarasi wasio na sifa, wengine wakishindwa hata na miradi midogo.

Waziri Mbarawa aliyasema hayo wakati akikagua miradi ya maji ya Kumbara-Litola, Milonje-Matemanga na Milonde katika Wilaya za Namtumbo na Tunduru, mkoani Ruvuma.

Profesa Mbarawa alisema Halmashauri nyingi zimekuwa zikitoa zabuni kwa wakandarasi katika mazingira ya rushwa, bila kuzingatia uwezo wao kifedha, vifaa vya kazi na kazi zao kwa sababu hawafanyi uchunguzi wa kina hivyo  kusababisha matatizo kwenye utekelezaji wa miradi.

Alisema Jambo la kutoa zabuni kusikozingatia sheria na taratibu kunapelekea kubadili wakandarasi na kuvunja mikataba mara mara kwa sababu ya utendaji mbovu wa wakandarasi, na kurudisha nyuma juhudi za Serikali kuwapatia wananchi wake huduma ya maji safi na salama.

“Serikali haitakubali kurudishwa nyuma kimaendeleo na mtu yeyote, tutawafukuza wakandarasi wasio na sifa na tutashughulika na wale wote wanaotoa zabuni pasipo kufuata utaratibu lazima niwaambie ukweli”, amesema Profesa Mbarawa.

“Ni lazima mfanye uchunguzi wa kina kwa kila mkandarasi kwa kuzingatia vigezo vyote, ikiwa ni pamoja na kwenda kuangalia kazi walizozifanya kwa lengo la kujiridhisha uwezo wake kabla hamjaingia nao mkataba”, ameonya Profesa Mbarawa.

Aidha, Profesa Mbarawa ameagiza Kampuni ya Service Plan Ltd isipewe tena kazi na wizara yake, baada ya kubainika imetoa taarifa ya usanifu wa mradi wa Kumbara-Litola isiyo sahahi uliopo Wilaya ya Namtumbo ambapo ungeigharimu Serikali fedha nyingi bila sababu.

Kulingana na usanifu wa awali kuonyesha gharama kubwa, ililazmika kufanya usanifu upya na kuonekana unaweza kutekelezwa kwa Shilingi Bilioni 1.2 baadala ya Shilingi Bilioni 6 kama ilivyoonyesha awali na mradi huo unategemewa kukamilika mwezi Disemba mwaka huu.
Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akikagua tenki la mradi wa Kumbara-Litola, Namtumbo na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo, Sophia Kizigo
Mradi wa maji Milonde ukiwa katika hatua ya utekelezaji.