Saturday, October 20, 2018

SERIKALI KUIMARISHA ULINZI MAENEO YA UTALII.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza  na wadau wa sekta ya Utalii ambapo aliwahikikishia nia ya serikali kuimarisha ulinzi maeneo yanayotumika kwa shughuli za utalii lengo ikiwa ni kuongeza mapato  kwa nchi na kutumia fursa zinazopatikana katika sekta hiyo. 

Kikao hicho kimefanyika Katika Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdul Wakil, visiwani Zanzibar. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
............................................

Serikali imedhamiria kuimarisha ulinzi katika maeneo mbalimbali ya utalii kwa kuweka vituo vya polisi vinavyohamishika ikiwa ni mpango wa kuwawekea mazingira salama wadau wa sekta hiyo na kuongeza mapato kwa nchi.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhandisi Hamad Masauni, wakati akizungumza na Wadau wa Sekta ya Utalii katika Ukumbi wa Sheikh Idrisa AbdulWakil, visiwani Zanzibar.

Alisema Serikali inatambua mchango wa sekta ya utalii na inajiandaa kuweka mipango madhubuti kuhakikisha ulinzi na usalama unakuwepo katika maeneo yote ya utalii.

“Tunatambua fursa na maendeleo yanayoletwa na utalii na jinsi pato la nchi litakavyoweza kuongezeka kwa kuimarisha sekta hiyo, hivyo serikali inakusudia kuweka vituo vya polisi katika maeneo ya utalii huku polisi wakishirikiana na polisi jamii waweze kuimarisha ulinzi kwa wageni wetu hawa,” alisema.

Akizungumza kwa niaba ya wadau wa utalii Visiwani Zanzibar, Abdallah Mwinyi aliiomba serikali kuwafundisha askari polisi elimu ya kumuhudumia mteja ili waweze kuwahudumia watalii hao pindi wakiwa nchini kwa shughuli za utalii.

“Tunaomba askari wetu wafundishwe elimu ya kuwahudumia watalii ikiwepo ukaguzi wa magari na watalii pindi wakiwa katika shughuli zao za kitalii lakini nawapongeza katika kupunguza matendo ya kihalifu katika maeneo kadhaa wanakopita watalii,” alisema.
Mdau wa Sekta  ya Utalii, Abdallah  Mwinyi akizungumza wakati  wa Kikao cha wadau wa sekta  hiyo, kilichoitishwa na Naibu Waziri  wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad  Masauni, lengo ikiwa ni kusikiliza changamoto wanazokutana nazo katika shughuli zao za utalii. Kikao hicho kimefanyika Katika Ukumbi wa  Sheikh Idrissa Abdul Wakil, visiwani Zanzibar. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kaimu Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, (SACP) Saleh Mohamed Saleh, akijibu maswali  ya wadau wa utalii yaliyoelekezwa katika idara yake kuhusu utaratibu wa polisi  wa usalama barabarani katika kukagua magari yanayobeba watalii. Kikao hicho kimefanyika  katika Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdul Wakil, visiwani Zanzibar. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu  Kamishna  wa Uhamiaji, (D.C.I.) Ali Nassor , akijibu  maswali ya wadau wa utalii  yaliyoelekezwa katika idara  yake kuhusu utaratibu wa kuingia  nchini kwa watalii. Kikao hicho kimefanyika  katika Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdul Wakil, visiwani  Zanzibar. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

KUTEKWA HADI KUPATIKANA KWA MO DEWJI- IGP SIRO

Inspekta Jenerali wa Polisi Tanzania IGP Saimon Sirro akionyesha mbele ya waandishi wa habari  moja ya silaha mbili  aina  ya Bastola  ziliyopatikana kwenye gari lililohusika katika utekaji wa mfanyabiashara Mohamed Dewji Oktoba 11 mwaka huu katika hoteli ya Collesium jijini Dar es salaam.
..............................

KAMANDA wa Polisi Nchini IGP Simon Sirro amesema kuwa baada ya kupatika kwa mfanyabiashara Mohamed Dewji Moo. Jeshi la polisi linaendelea na msako kuhakikisha waliokuwa wamemteka mfanyabiashara huyo wanapatikana popote walipo.


Kamanda Sirro amesema kuwa atahakikisha watekaji hao wanapatikana wakiwa hai au wamekufa huku akitoa onyo kali kwa vikundi ambavyo vinaingilia majukumu ya jeshi hilo nakubainisha kwamba anamashaka na uraia wao.

IGP Sirro ameyasema haya wakati akizungumza na waandishi wa habari Makao makuu ya  Jeshi la Polisi ambapo amesema katika kuhakikisha wanapoteza ushahidi walijaribu kuliunguza Gari hilo ambalo lilikuwa limetelekezwa katika eneo la Ghymkana.

Amesema taarifa za kupatikana kwa Mohamed Dewji  zilitolewa na  Askari wa Getini katika eneo hilo la  Ghymkana  ambapo Mo alimtaka Askari huyo kutoa taarifa kwa  familia yake ndipo walipokuja katika eneo hilo.

Amesema kuwa baada ya kuja katika eneo hilo ndipo walipojulishwa Polisi nawenyewe kufika katika eneo la tukio na kujiridhisha kupatikana kwa Mfanyabiashara huyo Dewji.

“Ilikuwa majira ya saa saba usiku Maeneo ya Gymkhna gari aina ya Toyota Sulf  Lilitelekezwa ndani yake likiwa na mfanyabiashara Mohamed Dewji ambapo baada ya kumwacha katika eneo hili walijaribu kutaka kupoteza ushahidi kwa kulichoma moto gari ambalo lilimbeba.” amesema Sirro.

Akifafanua zaidi amesema Gari hilo ni lile ambalo alilionyesha mbele ya waandishi wa habari mapema wiki hii. gari lenye namba za usajiri  T314AXX Na kwenye vioo vya pembeni kulikuwa na namba za usajili AGX 404 MC yenye rangi ya blue nyeusi na ufito wa rangi ya shaba kwa chini.

Kamanda Sirro amesema kuwa baada ya kufanya mazungumzo na Mo Dewji aliwaeleza waliomteka walikuwa wanazungumza lugha ya kingereza na mmoja lugha ya kiswahili cha hovyo.

Kwamujibu wa kamanda sirro amesema Mo aliwaeleza kuwa baada ya kumteka walitaka atoe fedha ambapo aliwaeleza yeye alikuwa hana hela na badala yake aliwaeleza awape namba za simu za baba yake.

Amesema hata walipopewa na za simu za baba yake hawakuweza kumpigia bila shaka waliogopa mtego wa polisi hivyo.” Sisi kama polisi tunashukuru Mo kapatikana lakini Jeshi la Polisi tutaendelea na msako na tunawataka wananchi.kuendelea kushirikiana nasi ili kuhakikisha tunakomesha matukio haya.”amesema Sirro.

Pia Kamanda Sirro amesema kuwa atahakikisha waliomteka Mo Dewji wanakamatwa .tena wakiwa hai au wamekufa ili kukomesha vitendo hivi na taifa kuendelea kuwa mahala salama wakati wote.

Katika hatua nyingine Kamanda Sirro ametoa Onyo kali kwa kikundi cha baadhi ya watu ambao wanaingilia utendaji wa Jeshi la Polisi kupitia mitandao ya kijamii.

” Kuna kikundi ambacho chenyewe kipo kwa ajili ya kuingili majukumu ya polisi jamani Polisi wanafanya kazi usiku kucha tena wakipita kukagua katika kila eneo nakwamba wenyewe wamelala na wake zao lakini kazi yao kuingilia kazi za polisi.”amesema Sirro.

Pia amezitaja baadhi ya nchi ambazo wanashirikiana kuhakikisha watekaji wanatiwa nguvuni.ambazo ni Afrika kusini,kenya,Uganda,Msumbini,…nakwamba ndani ya siku tisa askari wake hawajalala kuhakikisha Mo anapatikana.

Mo Dewji alitekwa Oktoba 11,2018 majira ya alfajiri katika Hoteli ya Colessum iliyopo masaki ambapo mara zote amekuw akifanya mazoezi ya Gym.
Hizi ndiyo silaha AK 47 moja na bastola tatu zilizopatikana kwenye gari lililohusika katika tukio la utekaji wa mfanyabiashara Mohamed Dewji hivi karibuni jijini Dar es salaam.
Gari lililohusika katika utekaji huo lililokutwa eneo la Gymkana jijini Dar es salaam.

 

MAGAZETI YA LEO 20 OKTOBA 2018.