Tuesday, October 16, 2018

ARIF ABRY APONGEZWA NA WAZAZI WA CCM IRINGA KWA KUISADIA CCM.

Mwenyekiti wa jumuiya ya  wazazi wa  chama  cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Iringa vijijini  Marco Kihongo (kushoto)  akipokea msaada wa fedha  kiasi  cha shilingi milioni 1  kwa ajili ya ununuzi wa kadi  za chama ,kutoka kwa mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa  Arif Abri
...............................................


JUMUIYA  ya  wazazi wa chama  cha mapinduzi  (CCM)  wilaya ya  Iringa  vijijni mkoani Iringa  kimepongeza  jitihada mbali mbali  zinazofanywa na mjumbe wa  mkutano  mkuu wa CCM Taifa  anayewakilisha  wilaya ya  Iringa vijijini Arif Abri katika  kuiwezesha  jumuiya  hiyo  kuwa na miradi yake .

Mwenyekiti  wa  jumuiya  hiyo Marco Kihongo ametoa  pongezi  hizo  leo    wakati akipokea  pesa  kiasi cha shilingi milioni 1 kutoka kwa  mjumbe  huyo kwa ajili ya kutekeleza  ahadi yake aliyoitoa kwa jumuiya  hiyo   ya  kuchangia  pesa hizo kwa ajili ya  ununuzi wa kadi  za jumuiya kwa  wanachama  wapya.

Kihongo alisema  kuwa mchango huo  wa  fedha  ni mtaji mkubwa kwa  jumuiya  hiyo kuweza kuongeza idadi kubwa  zaidi ya  wanachama wake  na  kuwa zoezi la  uongezaji  wanachama  litaanza mara moja  kuanzia sasa .
Huku  katibu  wa  jumuiya   hiyo  Martin Mfala alisema  pamoja na mjumbe  huyo  kuchangia  kiasi hicho  cha fedha  pia aliwaagiza  kutafuta  mashamba  kwa  ajili ya  kupanda  miti pamoja  mbali mbali  ikiwemo ya korosho katika  tarafa ya  Idodi na  kuwa  tayari wamefanikisha kupata ardhi kwa  ajili ya  kununua na  kukodi kwa kupanda miti hiyo .

Hivyo alisema  iwapo  watafanikiwa  kupata  ardhi  hiyo wataweza kupanda miti ambayo itakuwa ni sehemu ya miradi ya  jumuiya ya  wazazi katika wilaya  hiyo  huku akiomba  kusaidiwa  kutengeneza  pikipiki mbili za jumuiya hiyo ambazo kwa  sasa ni mbovu kwa  ajili ya  kusaidia  usafiri  wa  kwenda  kutembelea miradi ya  jumuiya .

Awali  mwanachama  wa  CCM wilaya ya  Iringa vijijini Thom Malenga  ambae ni katibu wa mbunge wa jimbo la Ismani ,Wiliam Lukuvi alisema  kuwa  jitihada kubwa  zimekuwa  zikifanywa na  Arif Abri katika  wilaya ya  Iringa  ni mfano wa kuigwa na  kuwa kazi mbali mbali amekuwa  akichangia  hivyo  kuchangia fedha  hiyo ni mwendelezo wa misaada mbali mbali ambayo amekuwa akitoa.

”  Tunaamini Mungu  humjalia   zaidi  yule anayetoa kwa  ajili ya  wengine  kifupi  tunashukuru  sana  kwa  misaada  mbali mbali ya kijamii na  chama katika  wilaya  ya Iringa vijijini ”  alisema Thom .

Akikabidhi  fedha   hizo  Arif  alisema  pamoja na  kuwa amefanya kazi na makatibu  wengi  wa  wilaya ndani ya  wilaya  ya  Iringa vijijini  ila utendaji kazi wa katibu Dodo Sambu ambaye  kwa  sasa ni mstaafu amekuwa  mchapakazi  sana na kw  muda wa miaka  mitatu aliyokuwepo  Iringa kazi yake imeonekana.

Hivyo  amesema  mategemeo yake  ni kwa katibu  ajaye  kuendeleza  umoja na mshikamano  uliokuwepo kamanguvu ya  ujenzi wa chama hicho katika  wilaya ,mkoa na Taifa  ili  ushindi wa CCM uzidi  kuongezeka  daima.
” Jana  wakati namtafuta  katibu wa jumuiya ya  wazazi  nilimpigia  mwenyekiti wa  umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM)wilaya ya Iringa vijijini ambae pia  aliomba kusaidia  pikipiki  nilimuahidi kuwa asiwe na hofu  nitampa  pikipiki   hiyo nilitegemea  leo kuja kukabidhi hapa  ila kasema yupo nje  ya mji kikazi  sasa  akirudi nitamkabidhi ”  alisema Arif 

Kuwa maombi ya jumuiya ya  wazazi kuhusu kutengenezewa   pikipiki  mbili atayafanyia kazi  haraka pamoja na  utengenezaji wa gari la  chama  wilaya .

Mjumbe  huyo pia alisema  juu ya mradi wa shamba atalitekeleza kwa  kununua shamba hilo  lenye ukubwa wa hekari 20  kama  mradi na  kuwa  pamoja na  miradi hiyo  pia umoja wa  wanawake   Tanzania (UWT) wilaya ya  Iringa nao  watasema  wanahitaji nini  ili wasaidiwe .

” Nataka  kuwaeleza kuw  katika familia  yangu  mimi  kutoka babu zangu   wote ni CCM na tunaipenda sana  CCM na  tupo tayari kuendelea   kusaidia  uhai wa chama ili kuona  CCM inaendelea  kutawala  daima” alisema Arif Abri .

Akishukuru  kwa misaada  hiyo katibu mstaafu wa CCM wilaya  ya  Iringa vijijini Dodo Sambu alisema  kuwa heshima   na ushindi wa CCM wilaya ya  Iringa  vijijini na mjini imetokana na jitihada za mjumbe   huyo wa mkutano mkuu wa CCM Taifa  kupitia  wilaya ya Iringa vijijini  pamoja na mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) anayewakilisha mkoa wa Iringa Salim Asas ambao  wamekuwa  wakijitoa kwa nguvu  zote .



RAIS DKT. MAGUFULI ATEUA MAKAMISHNA WA TUME YA KUREKEBISHA SHERIA NA NARCO

KAMATI YA SIASA BAGAMOYO YAITAKA CHALINZE KUONGEZA KASI YA UKUSANYAJI MAPATO


NA MWAMVUA MWINYI,CHALINZE

KAMATI ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Bagamoyo, haijaridhishwa na kushuka kwa ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri ya Chalinze, kipindi cha mwaka 2017/2018 ,na kuiasa iongeze jitihada ili kuinua ukusanyaji huo.

Kwa miaka miwili mfululizo Halmashauri hiyo imesifika kwa ukusanyaji mzuri unaovuka malengo lakini kwa taarifa kutoka wizara ya TAMISEMI inaonyesha haimo kwenye Halmashauri bora kwa ukusanyaji wa mapato .

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bagamoyo, Alhaj Abduli Zahoro Sharif alisema ,wamelazimika  ,kukutana na wakuu wa idara, wataalamu na madiwani wa Halmashauri hiyo, kuangalia endapo kuna mapungufu ama mianya yaliyosababisha kushuka kwa makusanyo hayo ili yadhibitiwe .

“Usimamizi sio mzuri katika makusanyo hali inayosababisha kushuka kwa makusanyo Halmashauri ya Chalinze na kushuka kuwa nafasi ya tatu kimkoa kutoka nafasi ya kwanza “

“Achani kufanya kazi kimazoea na bado sijaridhishwa na hali ya makusanyo na mtasababisha ilani kushindwa kutekelezeka kwa wakati ,alisema Alhaj Sharif.

Aliwataka washirikiane baina ya wataalamu, watendaji na madiwani kwa pamoja kubuni vyanzo vipya vya mapato.

“Tuna taarifa zipo, posi (EFD) 80 lakini wanatumia posi 30 ,na eneo ambalo ndio chanzo kikuu cha makusanyo ni ushuru wa kokoto ambapo hawatumii posi wanatumia karatasi wanazoziita vocha.” alifafanua Alhaj Sharif.

Kwa upande wake ,Mweka hazina wa Halmashauri ya Chalinze (DT) David Rubibira alisema kwa siku moja wanakusanya makusanyo katika malori ya kokoto 197-200 ambapo kwa siku wanakusanya sh.mil.8.9 .

Ofisa mipango wa Halmashauri ya Chalinze ,Shabani Millao alisema ,kuhusu suala la kushuka kwenye makusanyo ya mapato ya Halmashauri hiyo linatafsirika sivyo kwani wapo vizuri katika makusanyo .

Millao alitaja sababu za kutofikia kwenye makusanyo kwa kipindi hiki kuwa ni pamoja na kushushwa kwa makusanyo ya mazao ya chakula yasiyozidi tani moja ,na kuzuiwa kwa ushuru wa mabango .

Alisema ,wamejipanga kurekebisha makadirio  kutegemeana na hali halisi ya makusanyo kulingana na chanzo husika.

Kwa upande wake ,Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze Saidi Zikatimu alifafanua ,ukusanyaji 2016/2017 walikusanya kiasi cha shilingi  Bilioni 3.800 wastani wa asilimia 118.

“Tukaona kama tumevuka lengo tukaona tujiwekee malengo ya juu na tuongeza ongezeko la asilimia 26 ambalo tumekusanya sh.Bilioni 4 badala ya kukusanya Bilioni 4.3″alisema Zikatimu.

Alisema, katika malengo ya mwaka huo walivuka lengo kwa kukusanya kwa asilimia 17 badala ya asilimia 26 .

Zikatimu alielezea ,wameanza kujipanga kusaidia na idara ya fedha ili kufikia malengo wanayojiwekea ,ambapo kwa mwaka huu wameshajiwekea Bilioni tano ambalo ni ongezeko la asilimia 30.

Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo ,Amina Kiwanuka alisema wamepokea maagizo yaliyotolewa na kamati hiyo na kuahidi kuyafanyia kazi ili kuboresha makusanyo.

TAMASHA LA SANAA BAGAMOYO WANANCHI WAKARIBISHWA.

Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Dkt. Herbart Makoye ametoa wito  kwa wakazi wa Bagamoyo na nchi nzima kuhuduria Tamasha la kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo linalotarajiwa kuanza Tarehe 20 Oktoba 2018.

Akizungumza na waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Chuo hicho Dkt. Makoye alisema kuhudhuria Tamasha hilo ni fursa kwa watanzania na wale wa nje ya Tanzania kujionea taaluma mbalimbali zinazofundishwa chuoni hapo.

Alisema chuo hicho ambacho ni kikongwe hapa nchini kwa kutoa taaluma za sanaa na utamaduni kinawapa fursa vijana kujiajiri katika fani wanazopata chuoni hapo.

Aidha, aliongeza kwa kusema kuwa, Tamasha la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo hufanyika kila mwaka na kuandaliwa na Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) likiwa na malengo ya

>Kutunza na kuenzi sanaa na utamaduni wa Mtanzania.

>Kutengeneza jukwaa ambalo wanafunzi wa TaSUBa wanalitumia kupima kiwango chao cha umahiri katika sanaa kwa mwaka katika fani za sanaa za maonyesho na zile za ufundi.

>Kukutanisha watu wa tamaduni mbalimbali kutoka sehemu mbalimbali Duniani ili kuonyesha utajiri wao wa sanaa na utamaduni.

>Kutengeneza jukwaa ambalo ni kiungo cha kujenga mahusiano ya wasanii wa ndani na nje ya nchi kupitia maonyesho ya sanaa na pia kubadilishana uzoefu na mawazo katika kuendeleza tasnia ya  ya sanaa.

Dkt. Makoye alisema mwaka huu Tamasha linafanyika kwa mara ya 37 na litapambwa na mambo mbalimbali ikiwemo Sarakasi, maigizo pamoja na maonyesho ya sanaa za ufundi.

Aidha, alisema katika Tamsha hilo kutakuwa na warsha na semina zitakazohusu mambo mbalimbali ya kijamii.

Jumla ya vikundi vya sanaa 100 vimethibitisha kushiriki na kati ya hivyo vikundi 10 ni kutoka nje ya nchi ambazo ni Kenya, Uganda, Zimbabwe, Ivory Coast, Ufaransa, Zambia,Cameroon, Ujerumani na Finland.

Aliongeza kwa kusema kuwa, ufunguzi rasmi  wa Tamasha hilo utafanyika Tarehe 20 Oktoba 2018 ambapo mgeni rasmi atakuwa Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Dkt. Harrison Mwakyembe na litafungwa Tarehe 27 Oktoba 2018  ambapo mgeni rasmi atakuwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Juliana Shonza.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni Sanaa na Utamaduni katika kukuza Uzalendo.

Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Dkt. Herbart Makoye akizungumza na waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Chuo hicho Mjini Bagamoyo leo Tarehe 16 Oktoba 2018.
  
Baadhi ya wakufunzi na wageni kutoka nje ya nchi wakimsikiliza Mtendaji Mkuu wa TaSUBa Dkt. Herbert Makoye alipokuwa akizzungumza katika ukumbi wa TaSUBa, Bagamoyo.