Tuesday, May 8, 2018

STENDI FC BAGAMOYO YAWAKILISHA MKOA WA PWANI MASHINDANO YA KUINGIA DARAJA LA PILI.

Wachezaji wa Timu ya Mpira wa miguu ya Stendi Fc ya mjini Bagamoyo wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Alhaj, Majid Mwanga (mwenye fulana ya punda milia) wakati wa kuwaaga kuelekea kwenye mashindano ya kuwania kuingia ligi Daraja la pili yanayofanyika Mkoani Kilimanjaro. 
.............................
Timu ya Mpira wa miguu ya Stendi Fc ya mjini Bagamoyo imeingia kwenye kinyang'anyilo kutafuta ushindi wa kuingia ligi daraja la pili.

Timu hiyo ya Bagamoyo ni timu pekee,  ambayo inawakilisha  mkoani Pwani katika mashindano hayo ambapo imeondoka kuelekea wilaya ya Moshi mkoani kilimanaro.

Katika kufanikisha safari ya vijana hao wawakili wa Mkoa wa Pwani, Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Alhaj, Majid Mwanga amepokea fedha taslimu shilingi milioni tano laki mbili na elfu sabini na tano 5,275,000 kutoka kwa wafugaji wa Halmashauri ya Chalinze ili kuiwezesha timu hiyo.

Akizungumza mara baada ya kupokea fedha hizo Mkuu huyo wa wilaya amewashukuru wafugai hao kwa uzalendo wao kwani wameweza kuonyesha umoja wao kwa timu hiyo.

Miongoni mwa wadau walioweza kuchangia timu hiyo ni pamoa na Hifadhi ya Taifa Saadan ambapo waliweza kuchangia Jezi pea 3 kwa kila mchezaji.

Aidha, Mkuu huyo wa wilaya ametoa wito kwa wadau mbalimbali kujitokeza kuisadia timu hiyo ili iweze kufanya vizuri katika mashindano hayo.

Alisema timu hiyo ina uwezo mkubwa wa mpira hivyo ni matumaini yake kuwa itarudi na ushindi ili iweze kupnda daraa kutoa daraja la tatu kwenda la pili.

Aliongeza kuwa, ili timu iweze kufanya vizuri inapaswa kutizamwa kwa umakini katika mahitaji yake hasa inapokuwa nje ya nyumbani kwake ambapo wachezai na viongozi wa timu wasiwe na mawazo ya nyumbani na badala yake wacheze mpira vizuri na kurudi na ushindi nyumbani.

Kwa upande wake Nahodha wa timu hiyo ya Stend FC Soudi Abdalla Dondola lisema wananmshukuru Mkuu wa wilaya kwa kuwapa msada mkubwa wa kuwawezesha kufanya safari yao.

Akizungumzia namna walivyojipanga katika mchezo Dondola alisema timu iko vizuri na kwamba mashabiki wa Mkoa wa Pwani wategemee kuwa timu yao itaibuka na ushindi.

Kocha Mkuu wa timu hiyo Sheikh Abdallaah Sheikh alisema timu yake iko vizuri na kwamba wameipanga kushiriki mechi zote tano za kundi hilo

Alisema lengo ni kurudisha ushindi Bagamoyo na kuifanya timu hiyo uweze kusonga mbele mpaka kufikia ligi daraja la kwanza.
   
Wachezaji wa Timu ya Mpira wa miguu ya Stendi Fc ya mjini Bagamoyo wakiwa katika harakati za kuanza safari.
Muwakilishi wa Hifadhi ya Tifa ya Saadan akimkabidhi jezi Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo kwaajili ya timu ya Stendi FC.
 
 
Wafugaji wa Halmashauri ya Chalinze wakimkbidhi Fedha taslimu Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo kwajili ya timu ya Stendi FC

Friday, May 4, 2018

NAIBU WAZIRI WA NISHATI AWASHA UMEME VIJIJI VYA CHALINZE,

  
Naibu waziri wa Nishati Mh. Subira Hamisi Mgalu akiwa kijiji cha saleni Halmashauri ya Chalinze kwaajili kuwasha umeme Mradi wa Umeme Vijijini Kwa kupitia Ujazilizi Densification ulioanza kutekelezwa April 2017 na kukamilika Sasa.Wananchi wameanza kuunganishiwa umeme Kwa gharama ya 27000 tu.
 Image may contain: 6 people, including Subira Mgalu, people smiling, people sitting
Naibu waziri wa Nishati, Mh. Subira Mgalu amesema Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Dkt. John Magufuli imedhamiria kufikisha umeme kila kijiji ili kuwaondolea adha wananchi walikosa huduma ya umeme kwa muda mrefu.

Naibu waziri huyo wa Nishati ambae pia ni Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Pwani aliyasema hayo katika ziara yake Halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo ambapo aliweza kuzindua miradi ya umeme vijijini REA kwa kuwasha umeme katika vijiji kadhaa vya Halmashauri hiyo.

Aidha, alisema ni fusa kwa wananchi sasa kujitokeza kuchukua fomu na kulipa gharama ya shilimngi 27,000 kwaajili ya kuunganishiwa.

Alisema uzinduzi wa miradi hiyo ya umeme ni utekelezaji wa ahadi zilizotolewa na serikali ya awamu ya tano katika kampeni za uchaguzi na kwamba kilichobaki sasa ni utekelezaji tu.

katika hatua nyingine Naibu waziri huyo amewashukuru wadau wa Elimu katika Halmashauri hiyo wakiongozwa na Mrs Barbara na Wentworth Africa Foundation kwa msaada wao walotoa katika Sekondari ya wasichana Mandela ambapo waliweza kukabidhi taulo maalum kwaijili ya matumizi ya wasichana na kila msichana amepata Taulo Za kutumia Mwaka Mzima Kwa Wasichana Mia Tano Hamsini.
Wakati huo huo Naibu waziri huyo wa Nishati aligawa Taa za sola kwa Zahanati ambazo hazijafikiwa na umeme ili kuwarahishia kina mama wakati wa kujifungua.

Image may contain: 4 people, people smiling, people standing, outdoor and nature
Naibu waziri wa Nishati Mh. Subira Hamisi Mgalu akiwa ziara katika vijiji vya Chalinze ambapo aliweza kuwasha umeme katika vijiji vya Hondogo na Saleni pmoa na kugawa Taa za sola katika Zahanati ya Mihuga.
 Naibu waziri wa Nishati Mh. Subira Hamisi Mgalu ambae pia ni Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Pwani akikabidhi Taulo maalum kwaijili ya matumizi ya wasichana Kwa Shule ya Sekondari ya Wasichana Mandela ambapo kila msichana amepata Taulo Za kutumia Mwaka Mzima Kwa Wasichana Mia Tano Hamsini, Msaada huo umetolewa na Mrs Barbara na Wentworth Africa Foundation, Wadau hao wa Elimu Pia wameahidi kufadhili ujenzi wa Maktaba.
 Image may contain: 4 people, people smiling, people standing, crowd and outdoor 
Mh. Subira Mgalu amekabidhi, Mabox ya Vitabu Kwa Maendeleo ya Shule.
Image may contain: 4 people, including Subira Mgalu, people sitting
Naibu waziri wa Nishati, Subira Mgalu akiwa katika zoezi la kugawa Taa za solar Kwa ajili ya Wadi za kuzalishia Kina Mama Kwa ajili ya Zahanati za Mihuga , Masimbani na Kweikonje Maeneo ambayo hayana MiundoMbinu ya Umeme.
Image may contain: 1 person, crowd, tree, sky and outdoor 
Naibu waziri wa Nishati, Subira Mgalu akiwa kijiji cha Hondogo kata ya Miono Halamshauri ya Chalinze ambapo aliweza kuzindua mradi wa umeme viijini REA ambapo kijiji hicho sasa kimepata umeme.

Wednesday, May 2, 2018

DKT. ABBAS AKUTANA NA WAANDISHI, WASOMI WA MAWASILIANO YA UMMA MKOANI MWANZA

Mkurugenzi Mtendaji wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania Abubakar Karsan akimuonesha  Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi bango lenye kuonesha majukumu ya klabu za waandishi wa habari nchini,Jana 1/05/2018 mkoani Mwanza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania Abubakar Karsan akikabishi  Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi kalenda ya chama hicho,Jana 1/05/2018 mkoani Mwanza.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi  akiongea na wasomi wa Mawasiliano ya Umma wa Chuo cha Mtakatifu Agustino (SAUT) Mwanza kuhusu Maadili ya Uandishi wa Habari na umuhimu wa uandishi katika kufuata weledi, Jana 1/05/2018 mkoani Mwanza.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akishiriki kipindi cha TUJADILIANE kinachoendeshwa na Doto Bullendu chenye lengo la kuhamasisha maendeleo katika nchi kwa kutumia vyombo vya Habari, Jana 1/05/2018 mkoani Mwanza
Mkurugenzi Mtendaji wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania Abubakar Karsan akiongea wakati wa kumkaribisha Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO Dkt. Hassan Abbasi kabla hajashiriki kipindi cha TUJADILIANE kilicho hudhuriwa na waandishi mbalimbali wa vyombo vya habari vya kanda ya Ziwa, Jana 1/05/2018 mkoani Mwanza.


Tuesday, May 1, 2018

MAADHIMISHO YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI KUFANYIKA DODOMA KITAIFA.

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe anatarajiwa kuwa  mgeni rasmi katika Kilele cha Maadhimisho ya Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini .

Akizungumza na  Waandishi wa Habari  Jijini Dodoma , Katibu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Nevile Meena alisema mada mbalimbali zitakazojadiliwa ni pamoja na  changamoto zinazovikumba vyombo vya habari katika kipindi cha miaka 27 tangu Azimio la Windhoek, Namibia, lilipopitishwa linalohusu uhuru wa vyombo vya habari.

 Akieleza zaidi alisema, Kilele cha Maadhimisho hayo kitafikiwa      kesho, Mei 3, mwaka huu, mkoani Dodoma, ambapo siku moja kabla kutakuwa na majadiliano kuhusu hali ya vyombo vya habari nchini ambayo yatafunguliwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai.

“Tutapata Wakati muafaka wa kujadili mada kuu ya changamoto zetu, pia kutakuwa na mada nyingine zitakuwa zinaendelea katika vikundi, ikiwemo inayohusu mitandao ya kijamii kama inatakiwa kudhibitiwa au watumiaji ndio wajidhibiti wenyewe,” alisema Meena.

Pamoja na hayo alisema kutakuwa na mada kuhusu unyanyasaji wa kingono ndani ya vyombo vya habari, na kuona kama suala hilo bado ni kikwazo hasa kwa waandishi wanawake kupata nafasi za juu kwenye vyombo vya habari.

Aidha Katibu huyo wa TEF alisema, kutakuwa na mada kuhusu usalama wa waandishi wa habari, ni kiasi gani waandishi wanakuwa salama wanapofanya kazi zao katika maeneo mbalimbali.

“Suala la haki za kupata habari, japo limeingizwa kwenye sheria tangu mwaka 2016 na kanuni zake Februari mwaka huu, na namna gani mwandishi anaweza kudai haki hiyo,” alisema.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Klabu za Waandishi Tanzania (UTPC), Jane Mihanzi aliyataja maadhimisho hayo kuwa ni fursa kwa wadau wa habari kujadili namna vyombo vya habari vilikotoka, vilipo na wapi vinaelekea.

” Sisi kama wadau wa habari tunaotambua na kuwajali wananchi kupata habari, tumekuwa tukisaidia waandishi kuwapamafunzo na vifaa vya kazi,”alisema. 
Kwa upande wake mwakilishi wa Mfuko wa Habari Tanzania (TMF), Razia Mwawanga alisema kupitia maadhimisho hayo wanahabari na jamii kwa ujumla wataelewa umuhimu na wajibu wa kuwajibika.

Alisema,japo kuwa taaluma hii ina vikwazo vingi kuna ,waandishi watapaswakuwajibika kwa kujitolea ikiwa ni pamoja na  kuhamasika kuacha kuandika habari kwa mazoea na bafala yake wajikite katika kuandika habari zenye maslahi za kueleza wajibu wa serikali kwa umma na umma kwa serikali yao.

  Hata hivyo alisema fani ya uandishi habari inapaswa kujikita katika maadili ya uandishi bora kwa kuzingatia vigezo weledi na si vinginevyo  kwani hii itasaidia ukuwaji wa fani hiyo hapa nchini na kuondokana na uandishi wa kimazoea katika kutekeleza majukumu ya wanahabari ya kila siku.

MAGAZETI YA LEO TAREHE 01 MAY 2018.