Tuesday, March 20, 2018
Monday, March 19, 2018
MAKAMU WA RAIS ASHIRIKI UJENZI WA SEKONDARI MICHEWENI.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki
ujenzi wa skuli ya Sekondari Micheweni mkoa wa Kaskazini Pemba.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki
ujenzi wa skuli ya Sekondari Micheweni mkoa wa Kaskazini Pemba.
Picha
ya kuchora inayoonyesha muonekano wa skuli hiyo pindi itakapokamilika.
Picha
na Ofisi ya Makamu wa Rais.
RAIS DKT MAGUFULI AENDESHA MKUTANO WA 11 WA BARAZA LA TAIFA LA BIASHARA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara
na Uwekezaji, Mhe. Prof. Elisante Ole Gabriel akisoma muhtasari
wa mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa
na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam
leo Machi 19, 2018.
Mwenyekiti wa Baraza
la Taifa la Biashara ITNBC) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli akiwa meza kuu na Waziri Mkuu Mhe Kassim
Majaliwa Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
walemavu Mhe. Jenista Joakim Mhagama na kushoto kwake ni Katibu
Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Prof. Elisante
Ole Gabriel na Mwenyekiti wa Sekta Binafsi Dkt. Reginald Mengi
akijiandaa kufungua mkutano wa 11 wa baraza hilo Ikulu jijini Dar es
salaam leo Machi 19, 2018.
Taasisi
ya sekta binafsi nchini (TPSF) Dkt Reginald Mengi akiongea katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara
unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar
es salaam leo Machi 19, 2018
Viongozi wa taasisi
mbalimbalui wakiwa katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara
unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar
es salaam leo Machi 19, 2018
SERIKALI KUSAMBAZA UMEME VIJIJI VYOTE VILIVYO KWENYE MPANGO WA REA KISHAMPU.
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe.
Subira Mgalu (kushoto) akiwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mkuu wa Mkoa wa
Shinyanga, Mhe. Zainab Telack na Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mhe. Nyabaganga
Taraba wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ilipotembelea
mradi wa umeme kijiji cha Negezi.
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe.
Subira Mgalu akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara wakati Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ilipotembelea miradi ya umeme.
........................................
Naibu
Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu amesema Serikali itaendelea na usambazaji
wa nishati ya umeme katika vijiji vyote 50 katika Wilaya ya Kishapu kama ambavyo iliahidi.
Amesema
hayo wilayani humo wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini
ilipofanya ziara wilaya Kishapu kukagua miradi ya umeme inayotekelezwa na
Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
Kamati
hiyo ikiwa kwenye vijiji vya Negezi na Bulimba ikiambatana pia na uongozi wa
Mkoa na Wilaya, Mhe. Mgalu alisema kuwa mpango wa usambazaji umeme ni wa awamu
na kuwa wananchi wasiwe na hofu kila kijiji kitafikiwa na mradi.
Aliongeza
kuwa vijiji 33 kati ya 50 vitapata umeme wa REA awamu hii ya tatu wakati 17
vitapata nishati hiyo kupitia njia kuu inayounganisha mikoa ya Iringa, Dodoma, Singida na
Tabora.
Kwa
upande wake, Kamati hiyo ya Bunge ilisema wataendelea kuikumbusha Serikali
iendelee kutimiza ahadi zake kwa wananchi za kukamilisha miradi ya umeme.
Iliwataka
wananchi ambao wamepitiwa na miradi hii katika vijiji vyao kuichangamkia fursa
na kuomba kuunganishiwa ili kupata huduma hiyo na kujiletea maendeleo.
Aidha
iliwataka wananchi kuboresha aina za makazi yao kadiri ya uwezo wao na kuezeka nyumba zao
kwa bati na kuachana na matembe na hatimaye kuwa na nyumba zilizo bora.
Katika
ziara hiyo kijiji cha Bulimba kilichopo kwenye kata ya Ukenyenge kumezinduliwa
rasmi huduma ya umeme mradi uliokamilshwa kupitia REA na hivyo kutarajiwa
kuwanufaisha wananchi.
Baadhi ya wajumbe Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakiwa kwenye mkutano wa hadhara kijiji
cha Negezi wakati ilipotembelea miradi ya umeme vijijini wilayani Kishapu.
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe.
Subira Mgalu (kushoto) akishirikia kucheza ngoma ya Kisukuma akiwa akiwa kijiji
cha Bulimba mabako umeme uliwashwa rasmi baada ya kukamilika usambazaji.
ULEGA AIPONGEZA HALMASHAURI YA WILAYA YA UVINZA KWA MKAKATI MZURI WA KUINUA SEKTA YA MIFUGO NA UVUVI
Katika picha katikati kushoto
Afisa Uvuvi wa Wilaya ya Uvinza Bw. Haroon Chande akimueleza Naibu Waziri wa
Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega Anayeangalia Chaga kuhusu chaga hizo za
kuanikia dagaa zilizojengwa na mradi wa kuhifadhi mazingira wa ziwa Victoria
LIVEMP chaga ambazo ameeleza zimekuwa na msaada mkubwa kwa wavuvi wa dagaa
wanaotumia mwalo wa Muyobozi uliyobo Wilayani uvinza katika kijiji cha
Mwakizega.
Chaga za kisasaa za kukaushia
dagaa katika mwalo wa Muyobozi, uliyopo katika kijiji cha Mwakizega Wilayani
Uvinza, Mwalo ambao ulijengwa na Mradi wa kuhifadhi mazingira ya ziwa Victoria
LIVEMP , chaga hizo zinatumika na wavuvi kukaushia dagaa.
Wavuvi wakiteketeza wao wenyewe
nyavu haramu zilizokamatwa katika oparesheni ya kupambana na uvuvi haramu
katika ziwa Tanganyika Mbele ya Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah
Ulega alipofanya ziara katika Mwalo wa Muyobozi Wilayani Uvinza.
............................
Naibu
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega ameipongeza Halmashauri ya wilaya
ya Uvinza kwa kuwa na mikakati thabiti ya kupambana na uvuvi haramu na kutatua
kwa kiasi kikubwa migogoro ya wakulima na wafugaji kwa kuwekeza kwenye Ranchi
za mifugo.
Ulega
ameyasema hayo alipokuwa katika ziara ya kugagua Mwalo wa Muyobosi uliyopo
Wilayani uvinza ambapo alisema jitihada hizo za wilaya zitachangia kwa kiasi
kikubwa katika kuongeza mapato ya Halmashauri hiyo na serikali kwa ujumla,
kwani ina mkakati wa kutenga maeneo ya Ranchi kwa ajili ya wafugaji.
“Nataka
niwahakikishie mimi na wizara yangu tutakuwa tayari kuhamia hapa kulisimamia
jambo hili mtakapo tenga hayo maeneo ya kufugia, ili kuwaweka tayari wafugaji
katika maeneo hayo na huo ndiyo muharobaini wa kwenda kuondoa matatizo ya
wakulima na wafugaji katika nchi yetu kwa mipango ya namna hii inawezekana
kabisa, hicho ni kipaumbele chetu mimi na waziri wangu Mhe. Luhaga Mpina katika
uongozi wetu tutahakikisha kama siyo kupunguza migogoro ya wakulima na wafugaji
basi tutaindoa kabisa, kwa kushirikiana vyema na Halmashauri zetu” Alisema
Ulega.
Ulega
alisisitiza suala la mapambano dhidi ya uvuvi haramu na ulinzi wa Rasilimali za
uvuvi na suala zima la ufugaji wa samaki, nakuwaasa kuachana kabisa na
utamaduni wa kuagiza samaki kutoka nje ya nchi.
Naibu
Waziri Ulega alisema kuwa fedha nyingi zimewekwa katika mwalo huo wa
Muyobozi na kuwataka wavuvi katika eneo hilo kuutumia vizuri mwalo huo wenye
hadhi ya kimataifa ambapo ameleza kwa mwaka wa fedha uliopita mwalo huo peke
yake umechangia kiashi cha shilingi milioni 28 “ Ninaamini kama mtapasimamia
vyema mahala hapa patachangia pato la taifa mara nne zaidi ya mwaka jana. Ninyi
ndo muwe walinzi wa kwanza wa rasilimali hizi ili nchi yetu iweze kuinuka”
Alisisitiza
Awali,
akiongea katika ziara hiyo mwenyekiti wa kijji cha Mwakizega ambapo mwalo wa
Muhyobozi umejengwa Bw. Jaffari Abdalah, alisema mwalo huo unakabiliana na
changamoto mbalimbali ikiwa nipamoja na gati la mwalo huo kuwa na urefu wa mia
20 ambazo ni chache kwa boti kuegesha kupakua na kupakia kabla na baadha ya
shuguli za uvuvi , hivyo ameiomba serikali kuongeza urefu wa gati hiyo ili
mitumbwi mikubwa na midogo iweze kufanya shughuli za uvuvi vizuri.
Bw.
Jaffar pia alisema wavuvi wa Muyobozi wanakabiliana na changamoto ya kukosa
elimu kupitia mafunzo yanayoendana na wakati huu wa kisasa katika sekta ya
uvuvi.
Subscribe to:
Comments (Atom)


















