Monday, March 19, 2018

MAKAMU WA RAIS ASHIRIKI UJENZI WA SEKONDARI MICHEWENI.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki ujenzi wa skuli ya Sekondari Micheweni mkoa wa Kaskazini Pemba. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki ujenzi wa skuli ya Sekondari Micheweni mkoa wa Kaskazini Pemba.

Picha ya kuchora inayoonyesha muonekano wa skuli hiyo pindi itakapokamilika.

 Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais.

RAIS DKT MAGUFULI AENDESHA MKUTANO WA 11 WA BARAZA LA TAIFA LA BIASHARA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO



 Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Prof. Elisante Ole Gabriel  akisoma muhtasari wa mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018.

 Mwenyekiti wa Baraza la  Taifa la Biashara ITNBC) Rais wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akisalimiana na Mwenyekiti wa Sekta Binafsi Dkt. Reginald Mengi  alipowasili kuendesha mkutano wa 11 wa baraza hilo Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018.


Mwenyekiti wa Baraza la  Taifa la Biashara ITNBC) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa meza kuu  na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa  Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na walemavu Mhe. Jenista Joakim Mhagama na kushoto kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Prof. Elisante Ole Gabriel  na Mwenyekiti wa Sekta Binafsi Dkt. Reginald Mengi  akijiandaa kufungua  mkutano wa 11 wa baraza hilo Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018. 


Sehemu ya wafanyabiashara wakiwa katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018.


Taasisi ya sekta binafsi nchini (TPSF) Dkt Reginald Mengi akiongea katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018 




Viongozi wa taasisi mbalimbalui wakiwa katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018


MAZISHI YA JOHN MPONDA TaSUBa YATOA RATIBA.



SERIKALI KUSAMBAZA UMEME VIJIJI VYOTE VILIVYO KWENYE MPANGO WA REA KISHAMPU.


Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu (kushoto) akiwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Telack na Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mhe. Nyabaganga Taraba wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ilipotembelea mradi wa umeme kijiji cha Negezi.
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ilipotembelea miradi ya umeme.
........................................

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu amesema Serikali itaendelea na usambazaji wa nishati ya umeme katika vijiji vyote 50 katika Wilaya ya Kishapu kama ambavyo iliahidi.

Amesema hayo wilayani humo wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ilipofanya ziara wilaya Kishapu kukagua miradi ya umeme inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

Kamati hiyo ikiwa kwenye vijiji vya Negezi na Bulimba ikiambatana pia na uongozi wa Mkoa na Wilaya, Mhe. Mgalu alisema kuwa mpango wa usambazaji umeme ni wa awamu na kuwa wananchi wasiwe na hofu kila kijiji kitafikiwa na mradi.

Aliongeza kuwa vijiji 33 kati ya 50 vitapata umeme wa REA awamu hii ya tatu wakati 17 vitapata nishati hiyo kupitia njia kuu inayounganisha mikoa ya Iringa, Dodoma, Singida na Tabora.

Kwa upande wake, Kamati hiyo ya Bunge ilisema wataendelea kuikumbusha Serikali iendelee kutimiza ahadi zake kwa wananchi za kukamilisha miradi ya umeme.

Iliwataka wananchi ambao wamepitiwa na miradi hii katika vijiji vyao kuichangamkia fursa na kuomba kuunganishiwa ili kupata huduma hiyo na kujiletea maendeleo.

Aidha iliwataka wananchi kuboresha aina za makazi yao kadiri ya uwezo wao na kuezeka nyumba zao kwa bati na kuachana na matembe na hatimaye kuwa na nyumba zilizo bora.

Katika ziara hiyo kijiji cha Bulimba kilichopo kwenye kata ya Ukenyenge kumezinduliwa rasmi huduma ya umeme mradi uliokamilshwa kupitia REA na hivyo kutarajiwa kuwanufaisha wananchi.
Baadhi ya wajumbe Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakiwa kwenye mkutano wa hadhara kijiji cha Negezi wakati ilipotembelea miradi ya umeme vijijini wilayani Kishapu.
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu (kushoto) akishirikia kucheza ngoma ya Kisukuma akiwa akiwa kijiji cha Bulimba mabako umeme uliwashwa rasmi baada ya kukamilika usambazaji.

ULEGA AIPONGEZA HALMASHAURI YA WILAYA YA UVINZA KWA MKAKATI MZURI WA KUINUA SEKTA YA MIFUGO NA UVUVI


Katika picha katikati kushoto Afisa Uvuvi wa Wilaya ya Uvinza Bw. Haroon Chande akimueleza Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega Anayeangalia Chaga kuhusu chaga hizo za kuanikia dagaa zilizojengwa na mradi wa kuhifadhi mazingira wa ziwa Victoria LIVEMP chaga ambazo ameeleza zimekuwa na msaada mkubwa kwa wavuvi wa dagaa wanaotumia mwalo wa Muyobozi uliyobo Wilayani uvinza katika kijiji cha Mwakizega.
Chaga za kisasaa za kukaushia dagaa katika mwalo wa Muyobozi, uliyopo katika kijiji cha Mwakizega Wilayani Uvinza, Mwalo ambao ulijengwa na Mradi wa kuhifadhi mazingira ya ziwa Victoria LIVEMP , chaga hizo zinatumika na wavuvi kukaushia dagaa.
Wavuvi wakiteketeza wao wenyewe nyavu haramu zilizokamatwa katika oparesheni ya kupambana na uvuvi haramu katika ziwa Tanganyika Mbele ya Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega alipofanya ziara katika Mwalo wa Muyobozi Wilayani Uvinza.
............................

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega ameipongeza Halmashauri ya wilaya ya Uvinza kwa kuwa na mikakati thabiti ya kupambana na uvuvi haramu na kutatua kwa kiasi kikubwa migogoro ya wakulima na wafugaji kwa kuwekeza kwenye Ranchi za mifugo.

Ulega ameyasema hayo alipokuwa katika ziara ya kugagua Mwalo wa Muyobosi uliyopo Wilayani uvinza ambapo alisema jitihada hizo za wilaya zitachangia kwa kiasi kikubwa katika kuongeza mapato ya Halmashauri hiyo na serikali kwa ujumla, kwani ina mkakati wa kutenga maeneo ya Ranchi kwa ajili ya wafugaji.

“Nataka niwahakikishie mimi na wizara yangu tutakuwa tayari kuhamia hapa kulisimamia jambo hili mtakapo tenga hayo maeneo ya kufugia, ili kuwaweka tayari wafugaji katika maeneo hayo na huo ndiyo muharobaini wa kwenda kuondoa  matatizo ya wakulima na wafugaji katika nchi yetu kwa mipango ya namna hii inawezekana kabisa, hicho ni kipaumbele chetu mimi na waziri wangu Mhe. Luhaga Mpina katika uongozi wetu tutahakikisha kama siyo kupunguza migogoro ya wakulima na wafugaji basi tutaindoa kabisa, kwa kushirikiana vyema na Halmashauri zetu” Alisema Ulega.

 Ulega alisisitiza suala la mapambano dhidi ya uvuvi haramu na ulinzi wa Rasilimali za uvuvi na suala zima la ufugaji wa samaki, nakuwaasa kuachana kabisa na utamaduni wa kuagiza samaki kutoka nje ya nchi.

Naibu Waziri Ulega  alisema kuwa fedha nyingi zimewekwa katika mwalo huo wa Muyobozi na kuwataka wavuvi katika eneo hilo kuutumia vizuri mwalo huo wenye hadhi ya kimataifa ambapo ameleza kwa mwaka wa fedha uliopita mwalo huo peke yake umechangia kiashi cha shilingi milioni 28 “ Ninaamini kama mtapasimamia vyema mahala hapa patachangia pato la taifa mara nne zaidi ya mwaka jana. Ninyi ndo muwe walinzi wa kwanza wa rasilimali hizi ili nchi yetu iweze kuinuka” Alisisitiza

Awali, akiongea katika ziara hiyo mwenyekiti wa kijji cha Mwakizega ambapo mwalo wa Muhyobozi umejengwa Bw. Jaffari Abdalah, alisema mwalo huo unakabiliana na changamoto mbalimbali ikiwa nipamoja na gati la mwalo huo kuwa na urefu wa mia 20 ambazo ni chache kwa boti kuegesha kupakua na kupakia kabla na baadha ya shuguli za uvuvi , hivyo ameiomba serikali kuongeza urefu wa gati hiyo ili mitumbwi mikubwa na midogo iweze kufanya shughuli za uvuvi vizuri.

Bw. Jaffar pia alisema wavuvi wa Muyobozi wanakabiliana na changamoto ya kukosa elimu kupitia mafunzo yanayoendana na wakati huu wa kisasa katika sekta ya uvuvi.