Saturday, October 14, 2017

MWIGULU NCHEMBA ATAKA SHERIA YA UHAMIAJI IREKEBISHWE KUWABANA WAHAMIAJI HARAMU.


 Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Mwigulu Nchemba akizungumza na waandishi wa Habari leo Tarehe 14 Oktoba 2017, katika Gereza la Kigongoni Bagamoyo.
.........................................
Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Mwigulu Nchemba amesema iko haja ya kufanya marekebisho ya sheria ili kuwabana wanaoingia nchini bila ya kufuata taratibu za Tanzania.

Waziri Mwigulu Nchemba alitoa kauli hiyo wilayani Bagamoyo leo Tarehe 14 Oktoba 2017 alipofanya ziara kutembelea Gereza la Kigongoni lililopo wilayani Bagamoyo.

Kauli hiyo ya waziri wa mambo ya ndani ya nchi imekuja kufuatia taarifa iliyotolewa na Mkuu wa magereza Mkoa wa Pwani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, SACP Boyd Mwambingu ambae alisema mkoa Pwani wafungwa ambao ni raia wa Ethiopia waliofungwa katika Magereza ya Mkoa huo ni 334, Mahabusu 12 na wanaosubiri kusafirishwa ni 91 ambao jumla ya raia kutoka Etheopia ni 437 wa Malawi ni 1 Msomali ni 1 wa DRC ni 1 wa Burundi 2 na kenya ni 2 ambapo jumla ya wafungwa wote raia wa kigeni waliopo ndani magereza ya mkoa wa pwani ni 339 na kufanya asilimia 40 ya wafungwa wote waliopo Mkoa wa Pwani ni raia wa kigeni.

Nae Mkuu wa Gereza la Kigongoni Mrakibu wa Magereza, SP. Muyengi Bulilo alisema gereza la kigongoni lina raia wa Etheopia 91 ambao wamemaliza kifungo chao na wanasubiri kusafirishwa.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Pwani, Plasd J. Mazengo  alisema sheria inataka wafungwa ambao ni raia wa kigeni walioingia nchini bila ya kufuata utaratibu wanapomaliza kifungo wanapaswa kurudishwa kwa fedha za serikali.

Kufuatia hali hiyo Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba alisema haiwezekani wahamiaji haramu wasafirishwe kwa gharama za serikali ambazo ni kodi za wananchi hali yakuwa tayari wameshatia hasara ya kula chakula cha serikali pindi walipotumikia kifungo.

Aidha, alisema iko haja ya kupitiwa upya kwa sheria hizo ili kuona namna ya kutoa adhabu kubwa zaidi kwa wahamiaji haramu na sio kufungwa mwezi mmoja na kisha wanarudia makosa hayo.

Aliongeza kwa kusema kuwa mwezi mmoja hautoshi kwa mtu kujutia kosa lake na badala yake atavumilia baada ya mwezi akitolewa na kurudishwa kwenye nchi yake atarudia tena kwakuwa kifungo cha mwezi mmoja hakijamuathiri.

Wakati huohuo waziri Mwigulu alisema wale wote watakaobainika kuwasafirisha wahamiaji haramu sheria kali zitachukuliwa dhidi yao ikiwa ni pamoja na kutaifisha magari yao. 
  Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Mwigulu Nchemba akisikiliza ripoti ya kutoka kwa mkuu wa Gereza la Kigongoni,Mrakibu wa Magereza, SP. Muyengi Bulilo

Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Mwigulu Nchemba akizungumza na maafisa wa magereza, Uhamiaji na Polisi katika Gereza la Kigongoni Bagamoyo, leo Tarehe 14 Oktoba 2017, alipotembelea Gereza hilo ili kujua changamoto zinazowakabili.

Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Mwigulu Nchemba akizungumza na maafisa wa magereza, Uhamiaji na Polisi katika Gereza la Kigongoni Bagamoyo, leo Tarehe 14 Oktoba 2017, alipotembelea Gereza hilo ili kujua changamoto zinazowakabili.

RAIS MAGUFULI AGOMA KUUFUTA MWENGE WA UHURU



RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli ambaye leo Oktoba 14, 2017 alikuwa Mgeni Rasmi kwenye Maadhimisho ya Kumbukumbu ya kifo cha Rais wa kwanza wa Tanzania Mwl. Julius Kambarage Nyerere na Kilele cha Mbio za Mwenge amesema amejisikia faraja kuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo ikiwa ni mara yake ya kwanza kushiriki maadhimisho hayo tangu awe Rais.

Aidha, Magufuli amemuelezea Hayati Mwl. Nyerere kama kiongozi shupavu aliyepigania maslahi ya wanyonge na kupambana na wakoloni katika kufanikisha kupatikana kwa Uhuru wa Tanganyika, Zanzibar na nchi nyingine za Afrika.

Amesema Nyerere alianza harakati za siasa mwaka 1953 baada ya kuchaguliwa kuwa Rais wa Chama cha TAA ambacho baadaye kilizaa TANU huku akiwa Mwalimu wa Shule ya Sekondari ambayo kwa sasa inaitwa Pugu Sekondari ambapo baadaye aliacha kazi hiyo ya kufundisha na kujikita kwenye siasa za ukombozi.

Rais Magufuli pia alisema iwapo Mwl. Nyerere angekuwa kiongozi mwenye tamaa au mbinafs, basi angechukua fukwe zote za Msasani, jijini Dar es Salaam na kuzifanya ziwe mali yake, lakini hakufanya hivyo kwa sababu ya uzalendo mkubwa aliokuwa nao.

Rais amesisitiza kuwa kamwe hatokukubali mbio za Mwenge wa Uhuru zifutwe katika kipindi chake cha uongozi, kwani mwenge huo una manufaa makubwa kwa Taifa ikiwemo kuzindua miradi mbalimbali za maendelo pamoja na kuwa nembo muhimu kwa Taifa letu.

Amesema wanaotaka mwenge huo ufutwe huenda hawajui historia ya nchi hii na kwamba kama wanaweza kukubali fimbo na kombe la dunia vikaletwa nchini na wakavipokea basi mbio za mwenge ni muhimu zaidi kuliko wanavyodhani.

Akizungumzia hali ya uchumi wa nchi, rais amekanusha wanaodai kuwa uchumi umeshuka huku akieleza kuwa uchumi wa Tanzania unazidi kupanda hukui mfumuko wa bei ukishuka na matokeo yake yanaonekana kwenye bidhaa pamoja na kushuka bei zake. Pia ameeleza kuongezeka kwa viwanda na wawekezaji wa kibiashara hapa nchini.

Friday, October 13, 2017

MKE WA RAIS MAGUFULI ATOA MSAADA WA CHAKULA KWA WATOTO YATIMA ZANZIBAR



Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janet Magufuli kushoto akiwa pamoja na Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein wapili kulia na Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Vijana Wanawake na Watoto Mama Maudline Cyrus Castico katikati wakikabidhi msaada ya Chakula kwa ajili ya Watoto yatima wanolelewa katika Kituo hicho.Wamwisho kulia ni Mkuu wa Kituo cha kulelea Watoto Mazizini Mjini Unguja.

Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janet Magufuli kushoto akisalimiana na Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein mara baada ya kuwasili katika nyumba ya kulelea Watoto Mazizini kwa ajili ya kusalimiana nao na kuwapa msaada wa Chakula ikiwa ni miongoni mwa Ziara yake  Zanzibar.

Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janet Magufuli akiwa amembeba Mtoto Yussuf ambae analelewa katika kituo cha Watoto Mazizini baada ya kuzaliwa na Kutelekezwa na Wazazi wake.katikati ni Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Vijana Wanawake na Watoto Mama Maudline Cyrus Castico na wa mwisho ni Naibu Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Vijana Wanawake na Watoto Mama Shadya  Mohammed Suleiman.