Tuesday, August 15, 2017

SHULE YA MWASAMA YAPEWA TUZO NA UMOJA GROUP YA UJERUMANI.

Mkurugenzi wa shule ya msingi MWASAMA, Mwajuma Saidi Masaigana, kushoto akipokea tuzo maalum kutoka kwa Umoja Group ya nchini Ujerumani, mara baada ya kutembelea shuleni hapo na kufurahishwa na namna shule hiyo inavyowaandaa watoto katika kupata Elimu bora huku wakiwa katika mazingira mazuri ya kujifunzia, anaemkabidhi zawadi hiyo kulia ni Mwenyekiti wa umoja Group, Veronika Tereh.
 Baadhi ya wanakikundi cha umoja Group kutoka nchini Ujerumani, wakiwa kwenye jukwaa ambapo waliimba wimbo unaohimiza umoja kwa lugha kiswahili, wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika shule ya msingi MWASAMA, mara walipotembelea shuleni hapo, Mwenye shati ya njano katikati ni
Mwenyekiti wa umoja Group, Veronika Tereh.
    
Mkurugenzi wa shule ya msingi MWASAMA, Mwajuma Saidi Masaigana, akiwa na wageni waalikwa meza kuu wakati wa kuwakarisha wageni wa Umoja Group kutoka nchini Ujerumani walipotembelea shuleni hapo.
   
Sehemu ya wgeni kutoka nchini Ujerumani wakiangalia burudani iliyokuwa ikitolewa na wanafunzi wa shule ya MWASAMA.
 wageni wa Umoja Group kutoka nchini Ujerumani wakipata vinywaji mara kumaliza kufanya mazungumzo na wenyeji wao walipotembelea shule ya msingiMWASAMA iliyopo mjini Bagamoyo.
 Afisa Utamaduni wilaya ya Bagamoyo, Hamisi kim, (kushoto) alipowasili katika shule ya msingi MWASAMA ili kushiriki hafla fupi ya kuzungumza na wageni wa kikundi cha Umoja Group kuoka nchini Ujerumani walipotembelea katika shule ya MWASAMA, kulia ni Mratibu wa shughuli hiyo, ambae pia ni mjumbe wa bodi ya shule, Hamza Mfaume.
 Mkurugenzi wa KAYA FM. RADIO ya mjini bagamoyo, Marie Shaba, akizungumza na wageni kutoka nchini ujerumani katika hfla fupi ya kuwapokea iliyofanyika shule ya Msingi MWASAMA mjini Bagamoyo.
 Mjumbe wa kamati ya CCM wilaya ya Bagamoyo, Mwinyi Hashim Akida, akizungumza na wageni hao, kushoto ni Mwalimu John Mponda kutoka Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa)
 
Wageni hao walipata fursa ya kutembelea eneo la shule ambapo ndani yake walijionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na shule hiyo ikiwemo ufugaji wa Samaki kama hapa wanavyoangalia Samaki waliofugwa kwenye Bwawa.

RIDHIWANI KIKWETE AHIMIZA MAZINGIRA BORA YA UWEKEZAJI

r1
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh Ridhiwani Kikwete (kulia Pichani) amesema Maendeleo ya Viwanda na uwekezaji yanategemea sana Mazingira Bora yaliyowekwa na Njia sahihi zisizo na mikwamo. 

Mbunge huyo aliyasema hayo wakati wa ziara ya Taasisi ya Kibunge inayopambana na Magonjwa ya Milipuko na Malaria wakati walipotembelea Kiwanda Cha Vyandarua Cha A To Z-Arusha. 

Alisema Mazingira ya Uwekezaji Tanzania Ya Viwanda yanapaswa kuwa mazuri zaidi ili kuwawezesha wawekezaji kuvutiwa na kuendelea kuwekeza katika sekta mbalimbali hapa nchini.
 r3 
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh Ridhiwani Kikwete akiwa na wabunge na wenzake wa Taasisi ya Kibunge inayopambana na Magonjwa ya Milipuko na Malaria wakati walipotembelea Kiwanda Cha Vyandarua Cha A To Z-Arusha.
 r2
Baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha Vyandarua cha A to Z cha Arusha.

Sunday, August 13, 2017

IGP SIRRO AWAAGA ASKARI POLISI WANAOKWENDA SUDANI

1
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akiwakabidhi bendera ya taifa askari kumi (10) waliopata uteuzi wa kwenda kuiwakilisha nchi ya Tanzania kwenye kazi ya Ulinzi wa Amani nchini Sudani ya Kusini (UNMISS) IGP Sirro, amewataka askari hao kufanya kazi kwa weledi na kwa kuzingatia misingi ya sheria na taratibu. Picha na Jeshi la Polisi.
 2
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, AKIWA KWENYE PICHA  na askari waliopata uteuzi wa kwenda kuiwakilisha nchi ya Tanzania kwenye kazi ya Ulinzi wa Amani nchini Sudani ya Kusini (UNMISS) IGP Sirro, amewataka askari hao kufanya kazi kwa weledi na kwa kuzingatia misingi ya sheria na taratibu. Picha na Jeshi la Polisi.