Sunday, August 13, 2017

MBUNGE WA CHALINZE APOKEA MSAADA WA MADARASA YENYE THAMANI YA MILIONI 30 KUTOKA KWA WAPAKSTAN

IMG-20170813-WA0008
 Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwan Kikwete ,akizungumza wakati wa uzinduzi wa madarasa sita na ofisi moja ya walimu katika shule ya msingi Pakistan utete kata ya Pera,yaliyokarabatiwa kwa ufadhili wa marafiki wa Pakistan.
 IMG-20170813-WA0015
 Balozi wa Pakistan nchini Tanzania,Amir Khan akizungumza baada ya kuzindua majengo ya madarasa sita na ofisi moja ya walimu yaliyokarabatiwa na marafiki wa Pakistan katika shule ya msingi Pakistan utete iliyopo kata ya Pera,kushoto kwake ni mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwan Kikwete
 
 Mbunge wa jimbo la Chalinze, Mh. Ridhiwani Kikwete, amezindua Madarasa sita yenye yaliyokarabatiwa na marafiki wa Pakstani kwa gharama ya shilingi milioni 30
Madarasa hayo sita na ofisi moja ya walimu yamejengwa katika shule ya msingi Pakistan Utete iliyopo kata ya Pera, Halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo, mkoa wa Pwani. 

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa madarasa hayo, Mbunge huyo wa Jimbo la Chalinze aliwataka wananchi waache tabia ya kusubiri kila kitu kufanywa na serikali na badala yake wawe mstari wa mbele kujitolea katika shughuli mbali mballi za maendeleo.

Aidha amesema ofisi yake na halmashauri wataendelea kuunga mkono juhudi za wafadhili na wadau mbalimbali wanaojitokeza kushirikiana nao kutatua changamoto zinazowakabili zilizopo katika jimbo hilo ikiwemo elimu.

Alisema baadhi ya wafadhili wanasaidia endapo wanaona jamii husika ikichukua juhudi juu ya jambo fulani na kufikia hatua mbalimbali .

 Aliwataka wananchi wa Chalinze kushirikiana na serikali, halmashauri na wafadhili wanaojitokeza ili kukamilisha miradi ya maendeleo iliyopo kwenye maeneo yao.

Aliongeza kwa kusema kuwa kipaumbele katika Halmashauri ya Chalinze ni kuondoa changamoto zote zilizopo katika sekta ya Elimu.

 Ridhiwani alisema wakati marafiki wa Pakistan wakiwezesha ukarabati huo,lakini halmashauri ya Chalinze imeshatenga fedha kwa ajili ya kujenga matundu ya vyoo nane katika shule ya Pakistan Utete.

 Aliongeza kwa kusema kuwa, wanajenga matundu ya vyoo katika shule ya msingi Mbala sanjali na madarasa mawili ya shule ya msingi Makombe.

 Ridhiwani alieleza,ujenzi wa matundu ya vyoo utasaidia kuondoa kero ya uchafu wa mazingira ambapo baadhi ya wanafunzi wamekuwa wakijisaidia ovyo maporini ,vichakani .

  Akizungumzia msaada walioupata kutoka kwa marafiki wa Pakistan, Mh. Ridhiwani aliwaomba marafiki hao kuendeleza ushirikiano baina yao na Halmashauri ya Chalinze ili kufanikisha mambo mbalimbali ya maendeleo.

 Alitumia nafasi hiyo kumpongeza mwenyekiti wa kitongoji Hussein Mramba na diwani wa kata ya Pera kwa jitihada walizozichukua kusukuma jambo hilo.

 Aidha,  alimuomba Balozi wa Pakistan nchini Tanzania, Amir Khan ,kuwasaidia ujenzi wa jengo la kulaza wagonjwa  na mashine za kupima magonjwa katika kituo cha afya Chalinze.
 IMG-20170813-WA0015
 Balozi wa Pakistan nchini Tanzania,Amir Khan akizungumza baada ya kuzindua majengo ya madarasa sita na ofisi moja ya walimu yaliyokarabatiwa na marafiki wa Pakistan katika shule ya msingi Pakistan utete iliyopo kata ya Pera,kushoto kwake ni mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwan Kikwete.


 Kwa upande wake Balozi wa Pakistan hapa nchini, Amiri Khan, alisema amefurahishwa na ushirikiano uliopo baina ya nchi hiyo na Tanzania,na alishauri kuwepo na mahusiano kati  ya wabunge wa Pakistan na Tanzania.

 “Nilipoambiwa kuja shuleni hapa ni km 120 kutoka Dar es salaam nikaona nije kutembea na kuona kilichofanyika, Nawapongeza kwa kuanzisha ujenzi huu  ili watoto wapate elimu”alisema Khan.

 Alisema ili watoto hao wasome vizuri ni vyema kukajengwa uzio katika shule hiyo ili kuweka usalama zaidi na kwamba wanaweza kusaidia kuujenga.

 Balozi huyo,aliahidi na kukubali ombi la kusaidia mashine na vifaa vya kituo hicho cha afya lakini kwasasa wanachotakiwa kufanya ni kuandika maombi ya msaada huo.
 
 Balozi wa Pakistan nchini,Amir khan wa kushoto na mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwan Kikwete,wakikagua majengo ya madarasa sita na ofisi moja ya walimu katika shule ya msingi Pakistan utete kata ya Pera,yaliyokarabatiwa kwa ufadhili wa marafiki wa Pakistan
 
 Balozi wa Pakistan nchini,Amir khan wa kushoto na mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwan Kikwete,wakiingia katika lango kuu la  majengo ya madarasa sita na ofisi moja ya walimu katika shule ya msingi Pakistan utete kata ya Pera,yaliyokarabatiwa kwa ufadhili wa marafiki wa Pakistan
 IMG-20170813-WA0009
 Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwan Kikwete kushoto akiagana na balozi wa Pakistan nchini Amir Khan baada ya kuzindua majengo ya madarasa sita na ofisi moja ya walimu katika shule ya msingi Pakistan utete kata ya Pera,yaliyokarabatiwa kwa ufadhili wa marafiki wa Pakistan.

MAGAZETI YA LEO TAREHE 13 AUG.2017.

Saturday, August 12, 2017

RIDHIWANI KIKWETE AGAWA VIFAA VYA MICHEZO JIMBO LA CHALINZE.

ch6
 Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Mh. Ridhiwani kikwete, wapili kushoto akikabidhi vifaa vya michezo kwa timu ya kata ya Kiwangwa, ambapo kulia ni Diwani wa kata ya Kiwangwa akiwa na Mtendaaji wa kata yake wakipokea vifaa hivyo kwa niaba ya timu yao.
................................................
 
Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Mh. Ridhiwani kikwete amegawa vifaa vya michezo kwa timu za jimbo la chalinze zinazoshiriki mashindano ya kombe la Mazingira linaloshirikisha timu kutoka kata zote za wilaya ya Bagamoyo.

Sherehe hizo zilizofanyika kata ya Kimange zilihudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo Madiwani wote wa Jimbo la Chalinze na watendaji wao wa kata ambao walipokea jezi kwa niaba ya timu zao. 

Sherehe hizo pia zilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya, Mh. Alhajj, Majid Mwanga, ambaye ndiye muandaaji mkuu wa mashindano hayo akishirikiana na wabunge wa majimbo yote mawili ya Bagamoyo na Chalinze pamoja na DAWASCO Bagamoyo, lengo likiwa ni kuihamasisha jamii ya wana Bagamoyo kuendeleza usafi wa mazingira.

Pamoja na kugawa jezi hizo, mbunge wa Chalinze aliziahidi timu za Jimbo la Chalinze kwamba mshindi wa pili wa mashindano hayo atapatiwa Pilkipiki ya Miguu miwili, na jezi kwa timu zote Tatu za juu.

Kombe hilo la Mazingira Wilayani Bagamoyo linashirikisha timu 28 ambazo kati ya hizo 11 kutoka kata za jimbo la Bagamoyo, 15 kutoka kata za jimbo la Chalinze na 2 Bodaboda wa Chalinze na Bagamoyo na kufanya idadi ya timu kuwa 28.

Kwa udhamini wa Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo pamoja na DAWASCO Bagamoyo, Mshindi wa kwanza atapatiwa Pikipiki ya miguu mitatu (TOYO) ambayo itawasaidia katika uzoaji wa taka katika kata husika.
 Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Mh. Ridhiwani kikwete, watatu kushoto akifurahia jambo pamoja na viongozi wengine, wakati wa kukabidhi vifaa vya michezo kwa timu ya kata ya Miono ambapo Diwani wa Kata ya Miono, Mh. Juma Mpwimbwi ameshika vifa hivyo pamoja na wajumbe wake kutoka kata ya miono, wa kwanza kushoto, ni Diwani wa kata ya Talawanda ambae pia ndiye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze, Mh. Saidi Zikatimu na wa nne kushoto mwenye miwani ni Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Mh. Alhajj, majid Mwanga.


ch1

ch3 
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Mh. Alhajj, majid Mwanga, akionesha moja ya jezi zilizotolewa, pembeni yake ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze, mh. Ridhiwani Kikwete.

ch2
ch4 
Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Mh. Ridhiwani kikwete, wapili kushoto akikabidhi vifaa vya michezo.
 
Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Mh. Ridhiwani kikwete, wapili kushoto akikabidhi vifaa vya michezo kwa Diwani wa kata ya Mbwewe, Mh. Ramadhani Mahamba, wa nne kushoto mwenye miwani ni Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Mh. Alhajj, majid Mwanga.
  
Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Mh. Ridhiwani kikwete, wapili kushoto akikabidhi vifaa vya michezo.
  
Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Mh. Ridhiwani kikwete, wapili kushoto akikabidhi vifaa vya michezo.

BANDARI BUBU BAGAMOYO KUDHIBITIWA.

IMG_20170727_130233
Jeshi la Polisi mkoani Pwani limesema limejipanga kudhibiti Bandari bubu zilizopo Bagamoyo ili kukomesha Biashara ya kusafirisha kutoka nje ya nchi kinyume na utaratibu,

Akizungumza na waandishi wa Habari Ofisini kwake Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP Jonathan Shanna, alisema Bagamoyo pekee ina Bandari bubu 18 na kwamba miongoni mwa njia zinazotumika kupitisha wahamiaji wa kigeni bila ya kufuata utaratibu ni pamoja hizo.
 
Aidha, Kamanda Shanna alisema Jeshi la polisi mkoani Pwani limejipanga kudhibiti njia zote za panya zinazotumika kupitisha magendo ya aina mbalimbali. 
 
Kamanda Shanna alitoa kauli hiyo wakati akitoa Taarifa kuhusu wahamiaji 72 walioingia nchini kinyume cha sheria ambao walikamatwa hivi karibuni katika shamba la Kampuni ya Ranchi ya Taifa (NARCO)huko Vigwaza wilaya ya kipolisi Chalinze.
 
Kamanda Shanna ,amesema kuanzia sasa.watataifisha mali zote za watu wanaojihusisha na biashara ya usafirishaji wa wahamiaji haramu.

Aidha amewatahadhalisha wale wanaotoa vyombo vyao vya majini na nchi kavu kusafirisha wahamiaji hao  kwani navyo vitataifishwa .

Alisema wanaojihusisha kusaidia na kuwawezesha kufika wahamiaji haramu watawachunguza mali mbalimbali walionazo kama imetokana na utakatishaji fedha na endapo itabainika imetokana na biashara hiyo zitafilisiwa.

Kamanda Shanna alibainisha,wataiomba mahakama kutaifisha mali zote za wale watakaobainika kuhusika kupata mali hizo na fedha na biashara haramu.

Alisema sheria ipo wazi inasema watu hao wapewe kifungo ama kupigwa faini hivyo itapendeza na itafurahisha jeshi la polisi kama watakuwa wanapewa adhabu zote na kufungwa .

Kamanda Shanna ,alisema taarifa ikifika kwao kuwa wanafungwa na kupewa adhabu kali ndipo wataacha kuingia nchini kwani watajua Tanzania sio mahala pa mchezo wala kukimbilia.

“Hii kuwakamata kuwapiga faini na kuwarudisha kwao ndio maana wanafanya mchezo mchezo kukimbilia huku,ukiwapiga faini wanakwenda wanarudi ni mchezo wa kuigiza”alisema .

Kamanda Shanna alielezea kwamba,Tanzania ina sheria zake endapo sheria zitawabana wahamiaji hao na kukoma kugeuza nchi kuwa lango lao la kupita kwenda nchi jirani ikiwemo Afrika ya kusini.
 
Hata hivyo ,kamanda huyo alisema wahamiaji waliokamatwa wameshawafikisha ofisi ya uhamiaji mkoani Pwani na watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.

Pamoja na hilo,Kamanda Shanna alisema wanafanya oparesheni kusaka wahalifu mbalimbali ,zoezi ambalo ni endelevu.