Saturday, December 31, 2016

RC. PWANI ATOA SIKU 30 WAFUGAJI WALIOHAMIA MKOANI HUMO KUONDOKA.


Mkuu wa mkoa  wa Pwani,  Mhandisi Everist Ndikilo, akizungumza katika mkutano  wa hadhara uliofanyika kijiji cha Kitonga, kata ya Vigwaza, Halmashauriya Chalinze wilayani Bagamoyo.
 
Mkuu wa mkoa  wa  Pwani, Mhandisi Everist Ndikilo, akizungumza na wananchi katika mkutano huo,  waliokaa chini, wa kwanza  kulia  ni  Diwani  wa  kata ya Vigwaza, Muhsini  Baruani, na  wa pili ni  Mbu nge wa  Jimbo  la Chalinze,  Ridhiwani  Kikwete .
.................................
Mkuu wa mkoa wa  Pwani Mhandisi  Everist Ndikilo, ametoa siku  30  kwa wafugaji waliohamia mkoani humo kuondoka baada ya kushamiri kwa migogoro ya wafugaji na wakulima.

Kauli hiyo aliitoa katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika kijiji cha  Kitonga kata ya Vigwaza katika Halmashauri ya Chalinze Wilayani Bagamoyo.

Alisema Serikali haiwezi kufum bia macho  ikiona  kila siku vurugu  za wafugaji na  wakulima ambazo  kimsingi  wanaosababisha ni wafugaji wahamiaji ambao  sio wenyeji wa mkoa huo.

Mhandisi Ndikilo  alisema kila mfugaji anajiona alihamia mkoani Pwani arudi alikotoka na wala hapaswi kuuliza aende wapi hali ya kuwa alipoingia mkoani humo aliingia  bila ya  kukaribishwa.

Wakati huohuo, Mkuu wa mkoa  Ndikilo  amewaagiza  wakuu wa wilaya  wote  mkoani humo, kusimamia zoezi la kuwaondoa  wafugaji hao na kuacha  mkoa  ukiwa salama.

Aidha, ameonya wale wote watakaokaidi amri hiyo hatua za kisheria  zitachukuliwa dhidi yake. 
   
Migogoro ya wafugaji na wakulima mkoani  Pwani, imekuwa  ikiongezeka  kila siku hali inayopelekea machafukoya mara  kwa mara na hata mauaji kwa kile kinachodaiwa kuwa ni jeuri inayofanywa na  wafugaji kwa kuingiza mifugo kwenye mashamba ya wakulimana kuharibu mazao.
 
 Mkuu wa Mkoa wa  Pwani, Mhandisi  Everist Ndikilo, kulia ni mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete,  wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi  wa Halmashauri ya Bagamoyo, Fatuma Omari  Latu, na wapili  kushoto ni  mkuu  wa wilaya ya Bagamoyo, Alhaji, Majid  Hemed  Mwanga.
 
wanakijiji cha Kitoga wakisikiliza katika mkutano wa kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji katika kijiji cha Kitoga kata ya Vigwaza
 
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Alhaji, Majid Hemed Mwanga akizungumza katika mkutano wa kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji, kijiji cha Kitonga kata ya Vigwaza katikaHalmashauriya Chalinze wilayani Bagamoyo.
 Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Alhaji, Majid Hemed Mwanga akizungumza katika mkutano wa kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji, kijiji cha Kitonga kata ya Vigwaza katikaHalmashauriya Chalinze wilayani Bagamoyo.
 
Watumishi   wa Halmashauri ya Chalinze wakifuatilia mkutano huo.
 
Mbunge wa Jimbo  la Chalinze, Ridhiwani Kikwete, mwenye miwani, akisalimiana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze, Saidi Zikatimu, aliyevaa shati  la Kitenge katikati ni Mkurugenzi wa HalmashauriyaChalinze,  Edesi  Lukoa.

VICHWA VYA HA BARI, MAGAZETI YA LEO 31 DESMBA 2016.

mtik

Friday, December 30, 2016

EWURA YARIDHIA TANESCO KUPANDISHA BEI YA UMEME

eura 
 
MAMLAKA ya Udhibiti wa huduma za Nishati na Maji, (EWURA), imetangaza ongezeko la bei ya umeme kwa asilimia 8.5%.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Felix Ngamlamgosi, (pichani), ongezeko hilo la bei ni kufuatia maombi ya Shirika la Umeme Nchini, (TANESCO), ambalo liliwasilisha maombi EWURA ya kutaka ongezeko la bei kwa asilimia 18.19, ifikapo Januari mwaka 2017.

Akitangaza bei hizo mpya jijini Dar es Salaam, leo Mkurugenzi Mkuu huyo wa EWURA amesema, baada ya kufanya uchambuzi wa kina,

Mamlaka yake imefikia uamuzi wa kuongeza
asilimia 8.5 itakayoanza kutumika Januari Mosi, 2017 kutokana na kuongezeka kwa gharama za uzalishaji wake.

Shirika la umeme Zanzibar (ZECO) ambalo linanunua umeme wa jumla kupeleka Zanzibar limeongezewa kwa asilimia 5.7% ya bei ya umeme.

Hata hivyo ongezeko hilo halitaathiri wateja wa majumbani ambao matumizi yao hayazidi uniti 75 kwa mwezi.

Kundi laTIB linalohusisha viwanda vidogo, mabango na minara ya mawasiliano litakua na tozo ya mwezi ya shilingi 5,520.

Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), linaendelea kufanya maboresho ya miundombinu ya umeme na kutekeleza miradi mipya ya kuunganisha wateja ili kuboresha huduma za umeme nchini.