Saturday, December 3, 2016

DC BAGAMOYO AWAONYA WAZAZI WATAKAOACHA KUPELEKA WATOTO WAO SHULE JANUARI 2017.

Mkuu wailaya ya Bagamoyo akizungumza na mwanafunzi katika shuleya  msingi Mbwewe ambae mahudhurio yake Darasani siyo mazuri katika mojaya  ziara zake za kutembelea shule zilizopo katika Wilaya yake.
.....................................
 Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga, amewaagiza watendaji kata kuandaa mikataba  na wazazi na walezi wote wilayani humo, itakayothibitisha kuwapeleka watoto wao shule kuanza kidato cha kwanza kwa wale waliofaulu elimu ya msingi.

Kauli hiyo ameitoa kwenye mikutano ya hadhara kwa nyakati tofauti alipofanya ziara kwenye  kata mbalimbali wilayani humo.

Majid alisema kila mzazi au mlezi anapaswa kumuandaa mwanae aliyefaulu darasa  la saba ili ampeleke kuanza kidato cha  kwanza mara tu shule zitakapofunguliwa mwezi Januari.

Alisema kila mtendaji wa kata aandae mkataba ambao mzazi au mlezi atathibitisha kwamba atampeleka mtoto shule kuanza kidato cha kwanza na kwamba asipompeleka apelekwe mahakamani na mkataba huo usainiwe na mzazi au mlezi huku mwenyekiti wa kijiji na mtendaji wa kijiji wanatakiwa kusaini  kama  mashahidi.

Alisema Elimu ndiyo urithi  pekee usiofilisika kwa mtoto hivyo kila mzazi anapaswa kuweka mikakati ya kumsomesha mwanae kwaajili ya faida yake na taifa kwa ujumla.

Aliongeza kwa kusema kuwa dhamira ya Rais Dkt.  John  Magufuli  kuweka sera  ya  elimu bure hapa nchini ni  kuhakikisha kila mtoto anapata haki yake ya  msingi ya  kupata  elimu hivyo wazazi  wasiwe sehemu ya  kuwanyima watoto wao   haki hiyo.

Aidha, alisema kuwa kufuatia mkakati wa Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli wa kutengeneza madawati nchi nzima, katika wilaya ya  Bagamoyo kwa sasa hakuna upungufu wa madawati baada ya  kuwa zoezi  la utengenezaji  madawati  kukamilika kwa zaidi ya  asilimia  mia moja.
 Wanafunzi wakiwa wamesongamana kwenye Darasa moja kutokana na upungufu wa vyumba vya kusomea katika shuleya msingi Kibindu.
Hata hivyo alisema kuwa zipo baadhiya shule zinakabiliwa na upungufu wa vyumba vya madarasa hali inayopelekea watotokukaa Darasani kwa  msongamano, na kwamba tayari ameweka mikakati ya kiwilaya  kuhakikisha changamoto hiyo inaondoka.

Alisema amewaagiza watendaji wa kata kwa kushirikiana na wenyeviti wa vijiji na watendaji wa vijiji kuangalia mahitaji ya vyumba vya madarasa katika maeneo yao nu  kuweka mikakati ya  kujenga madarasa ili  kuondoa tatizo la madarasa.

Akizungumzia mkakati  huo wa ujenzi wa madarasa kwa wilaya ya  Bagamoyo, alisema kuwa unakwenda vizuri  ambapo kila kata yenye upungufu wa madarasa imeanza kutekeleza ujenzi wa madarasa  kwa  kushirikiana  na wananchi wa maeneo husika wakiongozwa na madiwani wao.

Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga menye fulana nyukundu akiwa juu ya jengo la darasa shuleya msingi Kibindu.

Mkuu huyo wa wilaya ya  Bagamoyo  ametoa wito kwa wadau  wa elimu kuchangia ujenzi wa madarasa katika wilaya hiyo ili kuondoa upungufu wa vyumba vya madarasa.
Alisema mahitaji ni vifaa mbalimbali vya ujenzi ikiwemo, Saruji, Mabati, Nondo huku wananchi akiwataka  kujitolea nguvu zao kufanikisha ujenzi  huo wa madarasa  katika  kata  mbalimbali  wilayani bagamoyo.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majidi Mwanga, akizungumza na wanafunzi wa shule ya  msingi  Kiwangwa katika  moja ya ziara  zake wilayani humo.

Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga, akizungumza na wanafunzi wa  shule ya Sekondari  Kiwangwa katika moja ya Ziara zake ndani ya wilaya yake.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga akiwa katika shule ya  msingi Mapinga  katika moja ya  ziara zake wilayani humo.
Mkuu wa wilayaya Bagamoyo, Majid Mwanga akizungumza na watoto wa jamii ya wafugaji ambao hawajapelekwa shule katika kata ya  Ubena alipofanya ziara yake katika eneo hilo.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid  Mwanga akipata  maelezo ya  kwanini  watoto hawaendi shule kutoka kwa kina mama wa jamii ya  wafugaji, kata ya Ubena katika moja ya ziara zake wilayani humo.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid mwanga akiwa katika shule ya msingi Fukayosi kata ya Fukayosi.

PICHA  ZOTE KUTOKA MAKTABA YA BAGAMOYO KWANZA BLOG.

Friday, December 2, 2016

WANANCHI WAZUIA MSAFARA WA MBUNGE WA JIMBO. LA MKURANGA ABDALLAH ULEGA

ule2
Mbunge wa  Jimbo la Mkuranga Mkoani Pwani, Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kibuyuni  Kata Panzuo baada kufunga barabara kwa lengo la kufikisha malalamiko yao.
 ule3
Mkazi wa kijiji cha Kibuyuni  Kata Panzuo,Juma Mwengele akizungumza kwaniaba ya wananchi wezake  wa Kata ya Panzuo juu ya Ng’ombe ambao wanapita kuharibu vyanzo vya Maji na hata mazao.
 ule4
Mbunge wa  Jimbo la Mkuranga ,Abdallah Ulega akikagua timu kabla ya mchezo wa Kombe la Ulega Cup.
...........................
 
WANANCHI wa Kata ya Panzuo wamelazimika kufunga barabara kwa lengo la kufikisha malalamiko yao Kwa  Mbunge wa Jimbo hilo Abdallah Ulega ambaye Alikuwa anatoka kijiji cha mkuruwili, kusikiliza kero yao hususani Ng’ombe ambao wamekuwa tatizo kubwa katika Wilaya ya Mkuranga.

Wananchi hao ambao walilazimika kukaa katikati ya barabara walimweleza Mbunge Ulega kwamba wanataka kusikia kauli yake juu ya uharibufu unaofanywa na Ng’ombe hao.
 
Akizungumza kwaniaba ya wananchi wezake  Mkazi wa kijiji hicho Juma Mwengele alisema kuwa wamelazimika kufunga barabara ili kuonesha hisia zao kwamba wanakerwa na uharibufu unaofanywa na Ng’ombe ambao wanapita kuharibu vyanzo vya Maji na hata mazao.
 
“Ndugu mbunge kwaza tunaomba samahani sana Kwa kuharibu utaratibu wako lakini tumeladhimika kufanya hivyo kutokana na wanyama wanaitwa ng’ombe,kwakweli wanatuasili mno na tuseme tu hatuwataki sisi.”alisema Mwengele.
 
Aliongeza kuwa ng’ombe wamekuwa tatizo kubwa na kadri siku zinavyokwenda hali inazidi kuwa mbaya mno kwani wanyama hao kila siku wanaingia Kwenye maeneo muhimu hususani kwenye vyanzo vya Maji pamoja na mashambani.