Sunday, November 27, 2016

DC BAGAMOYO APOKEA SARIJI MIFUKO 400 KUTOKA NYATI CEMENT KWAAJILI YA UJENZI WA MADARASA.

Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga, akipokea mifuko 400 ya Saruji kutoka Nyati Cement, kwaajili ya ujenzi wa  vyumba  vya madarasa anayemkabidhi katikati ni makamo wa rais wa kampuni ya Nyati Cementi, Mr Pathank,  wanaoshuhudia kulia ni meneja wa masoko, Mr, Mahesh Batt, upande wa kulia mwenye miwanini Mwenyekiti wa Halmashuri ya Bagamoyo, Aliy aliy, anafuata ni Mkurugenzi wa Halmashuri ya Bagamoyo, Fatuma Omari Latu.
 ............................................
 
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid mwanga amepokea Saruji mifuko mia nne kutoka kwa Nyati Cementi kwaajili ya ujenziwa Madarasa katika wilaya hiyo.

Akipokea msaada huo wa Saruji Mkuu huyo wa wilaya amewashukuru  wadau hao ambao wameahidi kusaidia mifuko 800 ambapo wameanza kwa kukabidhi mifuko 400.

Amesema maendeleo katika jamii yanaletwa kwa ushirikiano katiya serikali  na wananchi kwa kusaidiwa na wadau mbalimbali  katika kufanikisha mahitaji muhimu.

Aliongeza kuwa wilaya ya  Bagamoyo kwa imekamilisha utengenezaji wa madawati na hivyo  kufikia  lengo  la utenegenezaji wa  madawati lakini changamoto  iliyopo  ni  upungufu  wa vyumba vya madarasa.

Alisema kwa kutumia Saruji hiyo, itasaidia kuongeza nguvu  katika maeneo ambayo ujenzi wa madarasa unaendelea.

Aidha,alisema kuwa kata zitakazofaidika na Saruji hiyo  ni zile ambazo  tayari zimeanza ujen zi na kwamba watapata saruji hiyo  kwaajili ya umaliziaji tu.

Nae meneja  wa masoko wa Nyati Cement, Mahesh Batt,  amesema kuwa kampuni yake  imejipanga  kuwekeza katika wilaya ya Bagamoyo ambapo inatarajia  kujenga  kiwanda cha  Saruji  katika eneo  la Talawanda  wilayani hapa ili kutoa fusa ya ajira  na kusogeza huduma ya bidhaa hiyo kwa mikoa ya  Morogoro, Dodoma, Tanga na Pwani.

Kwa upande wake  mwenyekiti  wa  Halmashauri ya Bagamoyo, Aliy Aliy amepongeza mkuu  wa wilaya ya  bagamoyo  kwa kuunganisha  wadau  mbalimbali  katika kutekeleza miradi ya maendeleo na kuahidikutoa ushirikiano ili kufanikisha ujenzi wa kiwanda cha Saruji  katika eneo la  Talawanda.

Aliongeza kwa kusema kuwa licha ya kugawana halmashauri bado wilaya ya Bagamoyo ni moja na kwamba atashirikiana na mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze ili kuhakikisha Kiwanda  hicho  kinajengwa katika eneo  la Talawanda.






Sunday, November 20, 2016

WANANCHI WASHAURIWA KUENDELEA KUPIMA AFYA ZAO UKIMWI BADO NI TISHIO

Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juzi, ambapo aliwaasa wananchi kuchukua uamuzi wa  kupima afya zao na kupatiwa matibatu. Kulia ni Mwenyekiti wa Tume hiyo, Dk. Hedwiga Swai.
............................................
 
WANANCHI wametakiwa kupima kila wakati na kuendelea kutumia kinga ili kujiepusha na maambuki mapya ya VVU.

Mwito huo umetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko katika kikao cha makamishina wapya wa tume hiyo kilichoketi jijini Dar es Salaam juzi. 

“Tunapaswa kuwa ni mikakati endelevu ya kupambana na ugonjwa wa ukimwi kwani bado kunachangamoto kubwa” alisema Maboko.

Maboko alisema watanzania wasidanganyike kuwa ukimwi umekwisha ugonjwa huo bado upo na ni changamoto kubwa.

Alisema changamoto kubwa ya ugonjwa huo bado ipo katika baadhi ya mikoa hasa ile ya nyanda za juu kama Iringa na Njombe hivyo wananchi wasibweteke kuwa ugonjwa huo umekwisha.

Alisema kwa Tanzania Bara kunamaambukizi ya asilimia 5.3 sawa na watu milioni mbili waliopata maambukizi.


WALIOUNDA GROUP FACEBOOK KUTAFUTA MASHAMBA WATAPELIWA ZAIDI YA MILIONI 300 BAGAMOYO.

Watu  400 ambao walikutana kwenye ukurasa wa Facebook mwaka 2014 kwa lengo  la kutafuta  mashamba, wametapeliwa zaidi ya shilingi milioni 300 katika kijiji cha Kidomole kata ya Fukayosi wilayani  Bagamoyo baada ya  kuuziwa  eneo linalomilikiwa na Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) lililopo wilayani Bagamoyo  ambalo hujulikana kama Ranchi ya Ruvu.

Utapeli huo umebainika baada ya mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga kuunda tume ya kuchunguza migogoro mbalimbali iliyojitokeza  katika kijiji cha Kidomole hali iliyopelekea  serikali ya kijiji  kusimamishwa  ili kupisha uchunguzi.

Awali serikali ya kijiji imekuwa ikituhumiwa kwa matumizi mabaya  ya madaraka kwa kusimamia mauzo katika hifadhi za  serikali pamoja na ubadhilifu wa fedha na kusababisha kuzorota kwa shughuli mbalimbali za maendeleo katika kijiji hicho.

Akielezea hali hiyo mbele ya mkuu wa wilayaya Bagamoyo, kiongozi wa wanunuzi hao wapatao mia nne, Jackline Mushi alisema mnamo mwaka 2014 mwezi wa sita walitengeneza kikundi kupitia ukurasa wa Facebook kwa  lengo la kutafuta mashamba ambapo walifikia idadi ya watu mia nne.

Alisema mara baada ya  kusikia Bagamoyo kuna maeneo yanauzwa kijiji cha Kidomole  walifika kijijjini hapo ambapo walipewa namba zinazoonyesha kuwa eneo hilo limepimwa na kwamba wauzaji ndio wamiliki halali.

Aliongeza kuwa baada ya kupata  namba zinazoonyesha shamba hilo  limepimwa walifika ofisi za Ardhi Bagamoyo ili kujiridhisha  ambapo ofisi ya Ardhi Bagamoyo ilisema eneo hilo lipo katika mpango wa matumizi bora ya Ardhi, na limetengwa kwaajili ya  makazi na  kilimo.

Jackline, aliendelea kueleza kuwa  mara baada ya kutoka ofisiya Ardhi walirudi kijijini ambapo walionyeshwa kitabu cha mpango wa matumizi bora ya Ardhi ambacho kinafanana na kile  walichoonyeshwa ofisi ya  Ardhi.

Alisema mara baada ya kujiridhisha waliomba kuelekezwa taratibu za manunuzi ili waweze kufanya malipo ambapo katika kikundi cha watu miane kila mmoja  alinunua kulingana na uwezo wake ambapo Jackline alinunua heka 50, wengine ni heka 30 kila mmoja na zaidi ya watu miambili walinunua heka mojamoja.

Mara baada ya kuuziwa maeneo hayo ambapo kila  heka  waliuziwa  shilingi  laki tatu, 300,000 na kufanikiwa kuuziwa  heka  elfu moja  na  hamsini  1,050 sawa na shilingi milioni mia tatu na kumi na tani, 315,000,000/=  walitakiwa kulipa asilimia kumi ya kijiji  ili wajadiliwe kwenye mkutano mkuu wa kijiji na kupitishwa.

Katika mauzo hayo ambayo yameidhinishwa na mwenyekiti wa kitongoji cha Kinyemvuu Mrisho Saidi, wauzaji walikuwa 27 ambao wao waliodai kuwa ni wamiliki wa eneo hilo ambao waliongozwa na Salum Kagunia na Selemani Mkwamba.

Hata hivyo Jacqueline amekiri kuwa, mara baada ya kununua eneo hillo mwezi wa  sita 2014  ilipofika mwezi wa 11 mwaka 2014 alifika aliyekuwa  mkuu wa mkoa wa  Pwani wakati huo Hajat Mwantumu Mahiza, na kuwaambia kuwa eneo hilo ni mali NARCO na kwamba  wao wametapeliwa.  

Taarifa ya uchunguzi kutoka ofisi ya mkaguzi Halmashauri ya Bagamoyo, iliyosomwa mbele ya mkuu wa wilaya imewataja  aliyekuwa mwenyikti wa kitongoji cha Usigwa Elizabeth Nazari na aliyekuwa mtendaji wa  kijiji cha Kidomole Seifu Mohamedi mayala kuhusika katika kujipatia fedha za asilimia 10 ambazoni miloni thelasini na  moja na  laki tano,  31,500,000 kinyume cha  utaratibu baada ya kubainika  asilimia kumi ya mauzo ya  shamba  hayakuingizwa  kwenye akaunti yakijiji kama walivyodai  hali inayoashiria kuwa kulikuwa na njama za kuwatapeli wanunuzi hao.

Kufuatia Taarifa ya wakaguzi kutoka Halmashauri ya Bagamoyo, mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga aliamuru waliohusika na mauzo hayo ya eneo la NARCO  wakamatwe na kwamba  wale wote walionunua waende mahakamani kudai haki zao.

Aidha, mkuu wa wilaya ya  Bagamoyo amewataka wanachi wanaotaka kununua Ardhi katika wilaya ya Bagamoyo kufuata  taratibu  za  kisheria  ikiwa ni  pamoja na kufika ofisi za Ardhi kwaajili ya kupata ushauri wa kitaalamu kabla ya kufanya  manunuzi.

Wanaoshikiliwa na  polisi ni Selemani Mkwamba  na Salum Kagunia  ambao ni viongozi wawauzaji Mrisho Saidi mwenyekiti wa kitongoji cha Kinyemvuu, huku Elizabeth Nazari akiendelea kutafutwa ili kutoa maelezo ya namna walivyopokea milioni  31,500,000  kama asilimia kumi ya mauzo.

VICHWA VYA HABARI, MAGAZETI YA LEO