Sunday, November 6, 2016

RC. PWANI, DC. BAGAMOYO, WASHIRIKI UJENZI WA MADARASA SHULE YA MSINGI KIBINDU WILAYANI BAGAMOYO.



Mkuu wa mkoa wa  Pwani Mhandisi Everist Ndikilo akijenga ukuta wa darasa katika ujenzi wa shule ya msingi kibindu akiwa pamoa na Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga.


Wananchi wa kijiji cha kibindu wilayani Bagamoyo wakionyesha ushirikiano wao mbele ya  mkuu  wa wilaya mara baada ya mkuu wa wilaya kuweka kambi  katika shule  hiyo  kushiriki ujenzi wa madarasa



Jeshi  la akiba,(mgambo) nalo halikuwa nyuma katika kushiriki ujenzi huo wa madarasa.



Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo akiwa kwenye ujenzi wamadarasashule ya msingi  Kibindu ambapo alishiriki kazi  zote katika kipindi cha siku nne.



Katikati ni mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Everist Ndikilo, akiwa  amebeba Tofari, kulia ni m kuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga na  kushoto ni Diwani  wa kata ya Kibindu Mkufya Ramadhani Mawazo, wakisomba matofari  kuyasogeza sehemu ya ujenzi.



Kushoto ni kamanda wa polisi mkoa wa Pwani, Kamishna msaidizi wa Polisi, ACP-Boniventure Mushongi akiwa  ameb eba tofari  kwenye  ujenzi wa shule ya msingi Kibindu.



Kulia ni kamanda wa polisi mkoa wa  Pwani, ACP- Boniventure Mushongi, akibeba tofali kushoto ni Afisa wamagereza ASP Yusufu.



Kulia ni mkuu wa  Polisi wilaya ya kipolisi Chalinze, Mrakibu  Mwandamizi wa Polisi,  SSP- Janeth Magomi, akiwa amebeba  Tofari, anaefuata mwenye  nguo nyekundu ni Afisa tarafa kwaruhombo Renitha Luzabico wakishiriki kwenye ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Kibindu.



Mshauri wa mgambo wilaya ya Bagamoyo, Meja Iddi Musira akiwa amebeba tofari kwaajili ya ujenzi wa madarasa katika shule ya  msingi Kibindu.

Saturday, November 5, 2016

BUNGE LAPITISHA MUSWADA WA SHERIA YA HUDUMA ZA HABARI

1
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye alipokuwa akitoa hoja kabla Kamati ya Bunge zima kujadili Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa 2016 ambao umepitishwa leo mjini Dodoma.
...............................


Mkutano wa Tano wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umepitisha rasmi Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa mwaka 2016 ambapo hatua inayofuata ni kuridhiwa na kusainiwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli ili uwe Sheria kamili ya nchi.

Muswada huo umepitishwa leo Bungeni mjini Dodoma ambapo mkutano huo uliongozwa na Mwenyekiti wa Bunge hilo, Mhe. Andrew Chenge.

Wabunge walijadili Muswada huo kifungu kwa kifungu na kuunga mkono upitishwaji wake baada ya Waziri mwenye dhamana na habari kutoa hoja ili Muswada huo uweze kujadiliwa.

Akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kupitishwa Muswada huo, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye amewashukuru wadau wote walioshiriki katika kutoa maoni juu ya Muswada huo kwani ndiyo yamepelekea kukamilisha mchakato mzima wa Muswada huo.

“Kwa niaba ya Serikali napenda kuwashukuru wadau wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine katika kuhakikisha tunatimiza malengo ya takribani miaka 20 iliyopita ya kuifanya taaluma hii ya habari kuheshimika kama zilivyo taaluma zingine”, alisema Waziri Nape.

Waziri Nape ameongeza kuwa kwa sasa Muswada huo umeshapitishwa hivyo kilichobaki ni utungaji wa Kanuni ambapo ameomba wadau wa tasnia ya habari kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kutoa maoni yatakayopelekea kuwa na kanuni zenye tija kwa wanahabari na taifa kwa ujumla.

Aidha, Mhe. Nape amewaasa wadau wa habari kuunganisha nguvu kwa pamoja hasa katika kipindi hiki ambacho Muswada huo umepitishwa pia amewataka wadau hao wasiruhusu mgawanyiko utokee kati yao bali washirikiane na Serikali katika kutekeleza wajibu wao wa kihabari kwa jamii.

Kwa upande wake Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju amesema kuwa Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa mwaka 2016 ni mwanzo mpya wa tasnia ya habari nchini ambapo amewaasa wadau wa habari wakiwemo waandishi wa habari kutambua kuwa haki mara zote huendana na wajibu, hivyo hakuna haki isiyo na wajibu.

Muswada huo uliopitishwa leo umejadiliwa na Bunge hilo kwa siku mbili ambapo kwa mara ya pili ulisomwa mbele ya Kamati ya Bunge zima na hatimaye kusomwa kwa mara ya tatu ili kukidhi hatua za utungwaji wa Sheria nchini.


TANGAZO KWA WALIOSOMA SHULE YA MSINGI NIANJEMA BAGAMOYO.

TANGAZO        TANGAZO           TANGAZO

   Watu wote  walio maliza katika  shule ya msingi Nianjema iliyopo Bagamoyo mjini, wanatangaziwa mkutano utakaofanyika siku ya jumapili tarehe 6/11/2016, katika eneo la shule hiyo saa 3:00 Asubuhi.

  Tangazo hili linawahusu watu woote waliomaliza shule ya msingi nianjema, bila kujali amemaliza mwaka gani, atakae sikia tangazo hili amjulishe na mwenzie.

 Tangazo hili limetolewa na mwanyekiti wa kitongoji cha nianjea A.
Kwa maelezo zaidi piga 0653370250.