Tuesday, October 11, 2016

DC. SAME ASIMAMIA ZOEZI LA KUTEKETEZA SHAMBA LA MIRUNGI.

Shamba la Mirungi likiteketea baada ya agizo la Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe Rosemary Staki.
 

Wakazi wa Kijiji cha Kisesa Kata ya Vudee wakishuhudia zoezi la uteketezaji wa shambala Mirungi.
 

Mkulima wa zao la Mirungi Johnson Charles Kangara akiwa ameshika mafuta ya taa tayari kwa ajili ya kuteketeza shamba lake la Mirungi.
 

Dc Staki akiwasisitiza wananchi kutojihusisha na kilimo cha zao la Mirungi
 

MKAZI WA KIBAHA AENDA JELA MIAKA 30 KWA KUBAKA MTOTO WA MIAKA 4.

Mahakama ya hakimu mkazi Kibaha imemuhukumu mkazi wa maili moja Kibaha, Kulwa Kisitu mwenye umri wa miaka 35 kwenda jela miaka 30 baada ya kutiwa hatianai kwa kosa la kubaka mtoto wa miaka 4 (jina linahifadhiwa).

Mtuhumiwa huyo ambae alikuwa akijihusisha na kubeba  mizigo katika soko la maili moja ametiwa hatiani baada ya mahakama hiyo kujiridhisha na ushahidi uliowasilishwa na upande wa Jamhuri.

Mwendesha mashtaka wa serikali, Rashidi Chamwi aliiambia mahakama hiyo kuwa, mtuhumiwa Kulwa Kisitu ambae anaishi nyumba moja na bibi na babu wa mtoto huyo alimbaka mtoto huyo alimbaka mtoto huyo mnamo Tarehe 28-05-2016 majira ya jioni, wakati alipokuwa ameachwa na bibi yake.

Mwendesha mashtaka huyo ameongeza kuwa, mtuhumiwa alianza kuchezesha uume wake kwenye sehemu za siri za mtoto huyo na  alipoona hamalizi haja yake ndipo alipoamua kujaribu kumuingiza mtoto huyo ndani na alipoona mtoto huyo anapiga kelele aliamua kuacha.

Mtoto huyo alibainika  kuingiliwa wakati bibi yake aliporejea na kuanza kumuogesha ndipo mtoto huyo akamtaja Kulwa Kuwa ndiye aliyefanya tukio hilo.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu mkazi wa Mahakama ya  Kibaha, Aziza Mbadyo amesema mahakama hiyo imeridhika na ushahidi uliotolewa mahakani hapo na kutoa adhabu ya miaka 30 jela ili kuwa fundisho kwa wengine.

Awali mtuhumiwa huyo aliomba mahakama hiyo kumpunguzia adhabu kwani hata yeyeanajutia kosa alilofanya kwakuwa ni tamaa tu za mwili na shetani alimpitia.   

Monday, October 10, 2016

RAIS DK. MAGUFULI APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO WA MABALOZI

hun

ZOEZI LA KUHAKIKI WASTAAFU LAANZA MKOANI PWANI.

l1
Baadhi ya wastaafu mbalimbali wakiwa tayari kwa ajili ya kufanyiwa uhakiki mkoani Pwani.Uhakiki huu unahusisha wanaolipwa kupitia  Wizara ya Fedha na Mipango Pekee.
................................................


Wizara ya Fedha na Mipango imeanza zoezi la Uhakiki wa Wastaafu wanaolipwa na wizara hiyo katika mkoa wa Pwani, Kibaha. 

Uhakiki huu hautausisha wastaafu wanaolipwa kupitia mifuko ya hifadhi za jamii kama vile PSPF, NSSF, PPF na GEPF.

Hayo yamebainishwa na Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali Bw.Mohamed Mtonga alipokuwa akiongea na waandishi wa Habari kuhusu mpango huo wa uhakiki ulioanza leo mkoani Pwani.

“Uhakiki huu unatokana na utaratibu uliojiwekea Wizara ya Fedha na Mipango wa kufanya uhakiki wastaafu ili kuhuisha orodha ya malipo ya wastaafu na inasaidia kubaini mabadiliko ya taarifa za wastaafu kama vile kufariki na hivyo kuepuka kulipa wasiostahili”Alisema Bw. Mtonga.

Aidha akizungumzia kuhusu utaratibu wa uhakiki huu amesema kuwa zoezi hili litafanyika nchi nzima  na limeanzia katika Mkoa wa Pwani wilaya ya Kibaha na litafanyika kuanzia leo tarehe 10 mpaka tarehe 14 mwezi huu na kuendelea kwenye wilaya zote za mkoa wa pwani mpaka tarehe 21 mwezi huu.

Baada ya uhakiki katika mkoa wa Pwani zoezi litaendeshwa kikanda nyanda za juu kusini katika mikoa ya Mbeya, Iringa, Rukwa, Njombe, Songwe na Katavi kuanzia tarehe 31 Octoba mpaka tarehe 11 Novemba mwaka huu.

Pia zoezi litafanyika katika kanda ya kati likijumuisha mikoa ya Dodoma, Morogoro  na Singida kuanzia tarehe 21 mpaka 25 Novemba.

Akizungumza na waandishi wa habari mwakilishi wa wazee wastaafu Bw.Benedict Kalaguza amesema kuwa wanaishukuru serikali kwa kufanya uhakiki huu wa wastaafu na kwamba zoezi limekuwa ni zuri lisilokuwa usumbufu wowote na limeboreshwa zaidi kwa kutumia teknolojia nzuri zaidi.

Aidha Wastaafu wanaohakikiwa wanatakiwa kufika kwenye vituo hivyo wakiwa na nyaraka kama Kadi ya Benki, Picha za passport mbili, Barua ya Ajira ya Kwanza, Barua ya Kustaafu au kupunguzwa kazi kazini, barua ya Tuzo la Kustaafu, Nakala ya Hati ya Malipo ya kiinua mgongo au mkupuo, kitambulisho cha pensheni na barua ya Kudhibitishwa kazini.