Tuesday, September 13, 2016

MKURUGENZI MTEULE, HADSON KAMOGA AANZA MAJUKUMU YAKE KWA KUOMBEWA KANISANI.

kamoga1
Apostle Onesmo Ndegi Kiongozi wa Kanisa la Living Water Center Kawe akimwombea Mkurugenzi mteule wa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu Hudson Kamoga aliyepiga magoti

Mkurugenzi mteule wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Hudson Kamoga akiwa na Baba yake wa Kiroho Apostle Onesmo Ndegi Kiongozi wa Kanisa la Living Water Center Kawe akimsiliza kwa makini akielezea uteuzi wake.

Mkurugenzi mteule wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Hudson Kamoga

Waumini wa Kanisani Living Water Center Kawe wakiwa wamenyoosha mikono kwa Mkurugenzi mteule wa Halmashauri ya wilaya  ya Mbulu, Hudson Kamoga kwaajili ya kumuombea katika  majukumu yake mapya.
........................ 


Mkurugenzi mteule wa Wilaya ya Mbulu, Hudson Kamoga, ambaye ameteuliwa mwishoni mwa wiki jana amesema anaamini ni Mungu aliyemuweka kwenye nafasi hiyo ili  awatumikie wananchi wa Mbulu kwa wakati huu. 

Akiongea kwenye ibada ya Jumapili hii  ndani ya  Kanisa la Living Water Center Kawe, wakati alipopewa nafasi na mtumishi wa  Mungu  Apostle Onesmo Ndegi  ili asalimia Kanisa Mheshimiwa Kamonga  alisema, anakwenda kwenye wilaya yenye changamoto nyingi za kimaendeleo ila anaamini Mungu atamwezesha kuzitatua kwa nafasi yake akishirikina na wananchi pamoja na  viongozi wengine kati halimashauri ya Mbulu.

Kamonga alisisitiza kuwa kwa kupata  nafasi hii ya  Ukurugenzi bado  ataendelea na utumishi wake kwa Mungu maana anaamini huo ndio uliomfanyakufikia hatua hiyo,hivyo kuamua kuwa anamtanguliza Mungu kaika kila atakachokuwa anafanya, alisema Kamoga.

Pia alitoa shukurani za dhati kwa Mtumishi wa Mungu Apostle Ndegi pamoja na  watumishi wengine kanisani hapo na kusema kuwa kati ya vitu ambavyo hawezi kuvisahau na malezi mazuri ya kiroho pamoja na mafindisho ambayo amekuwa akiyapata kutoka  kwa Apostle Ndegi na watumishi wengine kanisani hapo, akisema mafundisho hayo yamesababisha kuwa vile alivyo sasa!.

Mwisho Mtumishi wa Mungu Mtume Onesmo Ndegi  na waumini walifanya maombi kwa ajili yake ili Mungu aambatane naye katika utumishi wake kwenye nafasi hiyo ya Ukurugenzi!.


MAGAZETI YA TANZANIA LEO TAREHE 13 SEPTEMBA 2016.

leo

Monday, September 12, 2016

MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA SULUHU HASSAN AWASILI LUSAKA KUMWAKILISHA RAIS DKT. MAGUFULI KWENYE SHEREHE ZA KULA KIAPO RAIS WA ZAMBIA EDGAR LUNGU

bil2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akilakiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Vijana, Michezo na Maendeleo ya Watoto Mhe. Anes Musunga mara baada ya kutua  katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kenneth Kaunda jijini Lusaka, Zambia, leo Jumatatu Septemba 12, 2016  tayari kwa kumuwakilisha Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt John Pombe Joseph Magufuli kwenye sherehe za kuapishwa rais wa sita wa nchi hiyo Mhe. Edgar Lungu kesho Jumanne Septemba 13, 2016 katika uwanja wa Mashujaa jijini Lusakabil4

Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea shada la maua  mara baada ya kutua  katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kenneth Kaunda jijini Lusaka, Zambia, leo Jumatatu Septemba 12, 2016  tayari kwa kumuwakilisha Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt John Pombe Joseph Magufuli kwenye sherehe za kuapishwa rais wa sita wa nchi hiyo Mhe. Edgar Lungu kesho Jumanne Septemba 13, 2016 katika uwanja wa Mashujaa jijini Lusakabil5

Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Katibu Mkuu Katibu Mkuu Wizara ya Vijana, Michezo na Maendeleo ya Watoto Mhe. Agnes Musunga   mara baada ya kutua  katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kenneth Kaunda jijini Lusaka, Zambia, leo Jumatatu Septemba 12, 2016  tayari kwa kumuwakilisha Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt John Pombe Joseph Magufuli kwenye sherehe za kuapishwa rais wa sita wa nchi hiyo Mhe. Edgar Lungu kesho Jumanne Septemba 13, 2016 katika uwanja wa Mashujaa jijini Lusaka