Sunday, September 11, 2016

WAKURUGENZI WATEULE WATAKIWA KUWASILI DODOMA NA VYETI HALISI VYA TAALUMA ZAO

kamoga
Mmoja wa wakurugenzi wateule Bw.Hudson Stanley Kamoga Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, ambae kitaaluma ni mtangazaji.
................................. 


Wakurugenzi  wa Halmashauri ya Mji, Manispaa na Wilaya, walioteuliwa  siku ya  Jumamosi  Septemba 10,  2016 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wametakiwa kuwasilisha nakala halisi za vyeti vyao vya taaluma, kabla ya kuapa.

Zoezi la uhakiki wa vyeti hivyo litakalofanyika Ofis ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) katika jengo la Mkapa mjini Dodoma siku ya Jumanne Septemba 13, 2016 kabla ya kuanza kwa zoezi la kuapa.

Wakurugenzi hao 13 ni pamoja na Mkurugenzi wa  Halmashauri ya Manispaa mmoja, Mkurugenzi wa Mji mmoja na Wakurugenzi wa  Halmashauri za Wilaya 11, wanatakiwa kuwasili Ofisi ya Rais TAMISEMI mjini Dodoma  saa 2:00 asubuhi kwa ajili ya uhakiki wa vyeti vyao vya taaluma.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na  Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhandisi Mussa Iyombe na kusainiwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Rebecca Kwandu, Septemba 11, 2016 inawataka Wakurugenzi hao kuhakikisha wanawasilisha nakala halisi ya vyeti vyao vya taaluma kwa ajili ya kiapo cha uadilifu wa uongozi wa umma.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa uhakiki wa vyeti halisi vya kitaaluma, unafanywa kwa lengo la kujiridhisha baada ya mchakato wa kawaida wa uhakiki kufanywa kwa kutumia vyeti visivyokuwa halisi yaani vivuli.

Wakurugenzi hao ni Godwin Emmanuel Kunambi Manispaa ya Dodoma, Elias R. Ntiruhungwa Mji waTarime, Mwantumu Dau Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba, Frank Bahati  Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe, Hudson Stanley Kamoga Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Mwailwa Smith Pangani, Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo, Godfrey Sanga, Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama na Yusuf Daudi Semuguruka Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga.

Wakurugenzi wengine ni Bakari Kasinyo Mohamed Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea, Juma Ally Mnweke Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo, Butamo Nuru Ndalahwa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, Waziri Mourice Halmashauri ya Wilaya ya Karatu na Fatma Omar Latu Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo.


WANAFUNZI WAISLAMU KINGANI BAGAMOYO, WAFANYA MAHAFALI YA KUMALIZA KIDATO CHA NNE.

Wanafunzi waislamu wanaomaliza kidato  cha  nne katika  shule ya  sekondari Kingani wilayani Bagamoyo wakiwa katika mahafali ya kiislamu.
..................................................
 

Vijana wa kiislamu wametakiwa kuwa mfano wa tabia njema katika jamii kwakuwa na maadili mema huku wakitakiwa kuonyesha tofauti kati ya mtu aliyepata elimu na mtu asiyepata elimu.
 
Wito huo umetolea na katibu wa ustawi wajamii kutoka Taasisi ya Sirajul Munir Islamic Center (SIMIC) yenye  m akao makuu  majani  mapana mjini  Bagamoyo, ustadhi, Omari  Kisina alipokuwa  akizungumza  katika mahafali hayo.

Ust.Kisina  amb ae ndiye  aliyekuwa  mgeni rasmi, katika  mahafali hayo  am ewataka  vijana  wanaomaliza  elimu yaoya sekondari  kutambua  kuwa elimu hiyo  waliyoipata  ili  iwaletee manufaa wanapaswa  kuwa  tofauti  na mtu  asiyepata  elimu.

Aliongeza kuwa, madhara yanayopatikana katika jamii yanatokana nakutofuata sheria za Mwenyezimungu hivyo  amewataka vijana hao kuacha  kuiga mambo ambayo yanakwenda  kinyume na sheria za dini  ili kujiwekea  mazingira mazuri kwa  mwenyezimungu na jamii kwa ujumla.

Awali wakisomarisla wanafunzihao  walisema wanakabiliwa na chnagamoto kadhaa  katika kutekeleza ibada na  kujifunza  mambo yadini kwasababu  hawana eneo lamsikiti huku wakiwa  na uhaba wa vitabu  v ya  kujifunzia  pamoja na  walimu  wa  masomo  ya  maarifa  ya  uislamu.

Akijibu risala hiyo, Ust. Kisina alisema kuwa Sirajul Munir kwa kushirikiana  na Taasisi  ya  The Islamic Foundation wataangalia uwezekano wa kuwajengea msikiti  kam aene   litapatikana.

Kwa  upande   w ake Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wa  CCM wilaya ya Bagamoyo,  Abduli Rashidi  Sharifu  alisema  kutokana  na  changamoto zinazowakabili   wanafunzi  hao  katika  kujifunza  dini  wakiwa  shuleni  yeye atajitolea misahafu 20 na kuongeza kuwa  ujenzi  wa  m sikiti  ukiinza atachangia  tofali 1,000  kwaajili ya  ujenzi wa msikiti





Mwenyekiti  wa   jumuiya ya  wazazi  wilaya ya  Bagamoyo, Abduli Rashidi  Sharif  kulia akiwa na  katibu  wa  ustawi  wa  jamii kutoka  taasisi  ya  Sirajul   munir Islamic   Center kushoto  wakati wa  mahafali ya  vijana  wa  kiislamu katika  shule ya  Sekondari  Kingani.