Saturday, August 13, 2016

MAALIM SEIFU NA VIONGOZI WENGINE WA CUF WAMTEMBELEA SPIKA WA BUNGE, JOB NDUGAI NYUMBANI KWAKE.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad (Kushoto) akisalimiana na Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai mara baada ya kumtembelea nyumbani kwake leo jijini Dar es salaam.
 
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (Kulia) akiwaeleza jambo viongozi wa CUF walioongozwa na Katibu Mkuu wa Chama hicho Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad (Katikati) na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Julius Mtatiro waliomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam leo Agosti 13, 2016. Mhe. Spika, Job Ndugai amerejea nchini hivi karibuni akitokea nchini India alikokwenda kwa ajili ya uchunguzi na matibabu.
 
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (Kulia) akifurahia jambo na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad (Katikati) na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Julius Mtatiro waliomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam leo leo Agosti 13, 2016 .
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (Kulia) akimweleza jambo Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad (kushoto) aliyeambatana na viongozi wenzake wa CUF nyumbani kwa Mhe. Spika Job Ndugai leo leo Agosti 13, 2016 jijini Dar es salaam.
 

Naibu katibu mkuu wa CUF, Bara na Mbunge wa Kaliua, Tabora Mhe. Magdalena Sakaya akimweleza jambo Mhe. Spika, Job Ndugai (hayupo pichani) mara baada ya kumtembelea Mhe. Spika leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad.
Viongozi wa Chama cha Wananchi CUF wakimwombea dua Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (kulia) ili aendelee kuwa na afya njema ya kumuwezesha kutekeleza majukumu yake kikamilifu walipomtembelea nyumbani kwake leo jijini Dar es salaam.


LAPF YAWAPA SOMO WAHARIRI

1

Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa LAPF Bw. James Mlowe akizungumza wakati wa semina na wahariri wa Vyombo vya habari mbalimbali kuhusu maandalizi ya mafao ya kustaafu inayofanyika kwenye jengo la LAPF Tower Makumbusho jijini Dar es salaam, ambapo mada mbalimbali zimetolewa kuhusu mafao yanayotolewa na mfuko huo Kutoka kulia ni Kafifi Kafifi Afisa  Matekelezo Mwandamizi Kanda ya Mashariki LAPF, Amina Kassim Meneja wa Kanda LAPF.
2

Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa LAPF Bw. James Mlowe akizungumza wakati wa semina ya wahariri wa Vyombo vya habari mbalimbali kuhusu maandalizi ya mafao ya kustaafu inayofanyika kwenye jengo la LAPF Tower Makumbusho jijini Dar es salaam, Kutoka kulia ni Kafifi Kafifi Afisa  Matekelezo Mwandamizi Kanda ya Mashariki LAPF, Amina Kassim Meneja wa Kanda LAPF, Theophil Makunga Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri na kushoto ni Victor Kikoti Meneja Matekelezo LAPF.


 3

Baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari wakiwa katika semina hiyo inayofanyika kwenye jengo la LAPF Tower jijini Dar es salaam.
 5

Afisa Habari wa LAPF Rehema Mkamba akigawa vifaa kwa ajili ya semina ya wahariri wa vyombo vya habari katika semina ya mafao ya kustaafu yaliyofanyika kwenye jengo la LAPF Tower jijini Dar es salaam.
 

Wahariri wakuu wa vyombo vya habari Tanzania wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa kwenye mkutano huo uliondaliwa na LAPF .