Sunday, July 10, 2016

KIFO CHA ELIZABETH MAYEMBA, TASWA YAOMBOLEZA.






Chama Cha Waandishi wa Habari za Michezo (TASWA),kimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba wa mwanachama wake,Elizaberth Mayemba kilichotokea jana  jioni huko nyumbani kwake Tabata kwa Swai.

TASWA imestushwa na kuhuzunishwa  sana kutokana  na kifo hiki cha  Elizaberth ambaye mchango wake katika tasnia ya habari za michezo bado ulikuwa unahitajika sana.

Waandishi wa Habari za michezo wataendelea kumkumbuka Elizaberth kutokana na ucheshi,kujituma na  uwajibikaji katika kufanikisha kazi zake na kuwa mfano kwa waandishi chipukizi.

TASWA inatoa pole kwa familia ya marehemu, marafiki na waandishi wote wa habari na kuwatakia moyo wa  subira katika wakati huu wa majonzi ya kuondokewa na mpendwa wetu.

Mwenyezi Mungu aipumzishe mahala pema peponi roho ya marehemu. 

TASWA ipo pamoja na familia ya marehemu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.

Juma Pinto
Mwemyekiti TASWA

WATENDAJI MKOA WA PWANI WATAKIWA KUONESHA USHIRIKIANO KWA WAANDISHI WA HABARI.


Naibu Waziri wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi ya Mkoa Pwani (hawapo pichani) alipofanya ziara yake ya kikazi leo mkoani  kwa lengo la kujua maendeleo ya kisekta kwa upande wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo.



Watendaji wa Mkoa wa Pwani watakiwa kuwa wawazi kwa waandishi wa habari pale wanapotaka kupata taarifa kutoka kwao.

Hayo yamesemwa leo Mjini Kibaha, Mkoani Pwani na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura alipofanya ziara ya kikazi mkoani hapo kufuatilia utekelezwaji wa maendeleo ya kisekta kwa wizara yake. 

“Kwa kuwapa ushirikiano wakutosha waandishi wa habari kutasaidia kuepuka kuandikwa kwa habari zisizona taarifa kamili ambazo huleta mkanganyiko kwa jamii na kuharibu taswira ya ofisi, hivyo ni vyema mshirikiane nao”,alisema Naibu Waziri Wambura.

Pamoja na hayo Mhe. Naibu Waziri aliangiza kuwa katika bajeti ya mwaka 2016/2017 Kitengo cha Habari kipewe kipaumbele na kitengewe bajeti itakayokidhi mahitaji pamoja na kununuliwa vitendea kazi ili kurahisisha utekelezaji wa majukumu yao kwa urahisi ikiwa ni pamoja na kutangaza shughuli za maendeleo ya Mkoa.

Kwa upande wa Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Pwani Bw.Shangwe Twamala alisema mkoa huo unakabiliwa na changamoto ya uhaba wa Maafisa Michezo kwa baadhi ya Wilaya pamoja na Maafisa Utamaduni ila suala hilo kwasasa limeshawasilishwa kwa ngazi husika na wanalifanyia kazi.

Pamoja na hayo Kaimu wa Mkoa huyo aliendelea kusema Mkoa huo unakabiliwa pia na changamoto ya usikivi wa matangazo ya Redio na Televisheni kwa baadhi ya maeneo kama Rufiji,Mafia na mengineyo.

Naye Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Mashariki Bw.Bernard Haule alitoa ufafanuzi kuhusu suala la kukatwa kwa matangazo katika chaneli zote pale malipo yanapoisha katika ving’amuzi vya Azam na Zuku kwa kusema leseni zao ni tofauti na zile za Startimes na Continental ambazo mbali na malipo ya kifurushi yanapokwisha wao bado huonyesha chaneli tano za taifa bure ambazo ni ITV,Star Tv,Channel Ten, EATV na TBC 1.

Pamoja na hayo Mhe.Wambura aliagiza kuwa watendaji wahakikisheni wanatenga maeneo ya viwanja vya michezo yasiyo na mgogoro kwani michezo ni ajira na inasaidia vijana kujikwamua kiuchumi,hivyo ni vyema ipewe kipaumbele.

Halikadhalika Naibu Waziri Wambura alitoa wito kwa wasanii Muziki wa Mkoa wa Pwani kuiga mfano wa marehemu Baraka Mwishehe kwa kutunga nyimbo zenye maadili na zenye kubeba ujumbe wa kuelimisha na kuburudisha jamii.

Hata hivyo Naibu waziri aliendelea kuwasisitiza watanzania wote kwa ujumla kuenzi lugha ya Kiswahili kama yanavyofanya mataifa mengine duniani kuenzi lugha zao mfano China.


Kaimu Mkuu wa Mkoa Pwani Bw.Shangwe Twamala akitoa taarifa maendeleo ya kisekta kwa Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura (katikati) alipofanya ziara ya kikazi mkoani hapo leo Mjini Kibaha.
Afisa Tawala Wilaya ya Kibaha Bi. Sozy Mgate akieleza changamoto za sekta ya michezo kwa Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura (wa kwanza kushoto) alipofanya ziara ya kikazi leo Mjini Kibaha kujionea maendeleo ya kisekta katika Mkoa huo.

Friday, July 8, 2016

CLOUDS TV YAKEMEWA KWA KUTANGAZA USHOGA.

Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Maudhui, Joseph Method Mapunda.


Kamati ya maudhui ya Mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA, imekionya kituo cha utangazaji cha Clouds Television kufuatia kuzungumzia ushoga katika kipindi chake cha TAKE ONE, kilichorushwa tarehe 28/06/2016 ambapo mwendeshaji wa kipindi hicho alimualika mtu aliyejitambulisha kwamba yeye ni shoga.

Akisoma maelezo ya hukumu yaliyochukua dakika 27, katika ofisi za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Makamu Mwenyekiti wa kamati ya maudhui ya TCRA, Joseph Method Mapunda alisema kituo hicho cha Television kilikiuka kanuni na maadili ya utangazaji kutokana na mambo yafuatayo

1.   Kipindi kimeonyesha waziwazi jinsi ushoga unavyofanyika pamoja na mbinu zinazotumika.
2.   Shoga aliyehojiwa hajuti kujiingiza katika katika tabia hii mbaya hasa pale anaposema kuwa, ataendelea kufanya ushoga hadi mwisho wa maisha yake.

3.   Lugha iliyotumika katika mahojiano haina staha.
4.   Tabia ya ushoga inaanzia shuleni.

5.    Mtangazaji alikuwa anauliza maswali yanayoashiria kushabikia ushoga.
Aidha, Mapunda aliongeza kuwa, kamati hiyo ya maudhui ya TCRA ilibaini kuwa, kipindi kilikuwa hakina ubora kwakuwa maswali mengi aliyokuwa anauliza mtangazaji yalilenga kuhamasisha ushoga ikiwa ni pamoja na matumizi ya lugha isiyo na staha.

Aliongeza kuwa, kila mwenye leseni ya utoaji huduma za utangazaji lazima ahakikishe kuwa, vipindi vyake vinaepuka kufuru katika jamii na vizingatie unyeti wa imani za kidini na utamaduni katika jamii.
Alisema watanzania kwa kuzingatia imani zao za kidini na utamaduni hawakubaliani na ushoga.

Katika utetezi wake Clouds Television walisema kuwa jamii imebadilika kwa kiasi kikubwa na kwamba ukubwa tatizo la ushoga lipo kwenye mitandao ya kijamii hadi kufikia matangazo kutolewa katika mitandao hiyo.

Aidha, Clouds Television walikiri kuwa, ushoga ni kitu kibaya na kuongeza kuwa ifike wakati mtu akifanya kitendo cha ushoga aogopwe.

Makamu mwenyekiti huyo wa kamati ya maudhui ya TCRA alisema kuwa baada ya kusikiliza na kutafakari kwa kina maelezo ya utetezi yaliyotlewa na uongozi wa Clouds Television, kamati ya maudhui imeridhika kuwa mada ya ushoga kupitia kipindi cha TAKE ONE kilichorushwa hewani tarehe 28/06/2016 kilikiuka baadhi ya kanuni za huduma za utangazaji (Maudhui) 2005, ambazo ni 5(b), 5(c), 5(d), 15(c) na 16(2).

Mapunda aliongeza kuwa hukumu iliyotolewa kwa Clouds Television ni kuwa
1.   inatakiwa kuwaomba radhi watazamaji wake na watanzania kwa ujumla kutokana na kuwakwaza pamoja na kuwasababishia usumbufu kwa kurusha mada inayoongelea ushoga kwa namna upotoshaji kupitia kupitia kipindi cha TAKE ONE kilichorushwa tarehe 28/06/2016.

Aidha, Taarifa ya kuomba radhi itoke siku tano mfululizo kwenye Taarifa za habari za saa 1:30 usiku na saa 5:00 usiku kuanzia siku ya kusomwa hukumu na uthibitisho wa taarifa hizo uwasilishwe Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania siku ya jumatano ya tarehe 13/07/2016 kabla ya saa 10:00 jioni.

2.   Clouds Television inatakiwa kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza na kuhakikisha inazingatia kanuni zote za utangazaji nchini katika kutekeleza majukumu yake ya utangazaji.

3.   Kamati ya Maudhui, inawaonya vikali Clouds Television kwa kukiuka kanuni za utangazaji (Maudhui), 2005 na 5(b), 5(c), 5(d), 15(c), na 16(2).

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Clouds Television Ruge Mutahaba alisema wamepokea kwa masikitiko hukumu hiyo kwakuwa lengo la kipindi hicho ni kuielimsha jamii madhara ya ushoga na si vinginevyo.

AMANA BANK YAWAZAWADIA WATEJA WAKE.

Mkurugenzi wa Bank ya Amana DR MUHSIN MASOUD akimkabidhi zawadi ya Television mshindi wa kwanza wa kampeni ya Faidika na Amana Bank Bi PIKIRA NLONGANE wakati wa Hitimisho la kampeni hiyo iliyokuwa na lengo la kuwajengea uwezo watanzania wa kuwekeza zaidi.

Hitimisho la Kampeni hiyo limefanyika wakati wa siku ya maonyesho ya kimataifa ya biashara saba saba Jijini Dar es salaam ambayo Bank ya amana ni moja kati ya wafanyabiashara waliokuwa na Banda katika Maonyesho hayo .

 Zawadi ya JOKOFU kwenda kwa mshindi wa pili ambaye ni SHAKIRA IBRAHIMU imekabidhiwa na kupokelewa na mwakilishi wake ambaye ni AHMED SANDE (Pichani) akikabidhiwa zawadi hiyo na Mkurugenzi wa Bank ya Amana DR MUHSIN MASOUD wakati wa utoaji wa zawadi hizo.


Mshindi wa nne amepata zawadi ya Table Feni ya kisasa yenye AC pia.Pichani ni Mkurugenzi wa Bank ya Amana DR MUHSIN MASOUD akimkabidhi zawadi Bwana HEMED SULEIMAN ambaye ameibuka mshindi wa nne katika kampeni ya Faidika na Amana Bank iliyochezeshwa ndani ya banda la Bank hiyo katika maonyesho ya kimataifa ya Biashara ya saba saba Jijini Dar es salaam ambapo washindi wanne wamejinyakulia zawadi mbalimbali zenye thamani ya shilingi za kitanzania Million Tano 

Katika kuadhimisha kilele cha kampeni ya FAIDIKA NA AMANA BANK,Bank imezawadiwa wateja wake waliobahatiika kushinda zawadi mbalimbali kutokana na kujiwekea akiba zao na Benk hiyo leo siku ya kilele cha maonyesho ya saba saba Tarehe 7/7/2016.

Wateja hao walichaguliwa kitaalam katika droo iliyochezeshwa ndani ya viwanja vya saba saba katika banda la amana bank na kupewa taarifa ya kufika kupokea zawadi zao kutoka uongozi mkuu wa bank hiyo wakiongozwa na Mkurugenzi mtendaji DR MUHSIN SALIM MASOUD.

Kampeni hiyo iliyojumuisha wateja wa akaunti za akiba binafsi kujiwekea akiba katika akaunti zao kuanzia kiasi cha shilingi 500,000 na kuendelea kwa muda wa miezi mitatu na kuweza kupata nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali za vifaa vya matumizi ya nyumbani kama Luninga,Jokofu,Microwevu,Pamoja na Table Feni yenye AC Pia.

Mkurugenzi wa Bank ya Amana DR MUHSIN MASOUD akizungumza na wanahabari wakati wa Utoaji wa zawadi hizo kwa washindi wanne wa Kampeni ya Faidika na Amana Bank ambapo amewataka watanzania kuwa na utamaduni wa kuwekeza kwani ni utamaduni mzuri na unaofaa kuendelezwa 
Akizungumza na wanahabari mapema leo wakati wa utoaji wa zawadi hizo kwa washindi hao meneja masoko wa Bank hiyo Ndugu DASSU MUSSA amesema kuwa bank ya amana imejipanga kuendelea kuwafikia na kuwapatia watanzania wote huduma bora zenye ubunifu na zenye tija kufuatana na mahitaji yao mbalimbali,huDuma pia ambazo zinafwata misingi ya sheria ya kiislamili kuwapatia faida iliyo halali na kuwaondoa katika mzigo wa riba.

Aidha amewahamasisha watanzania wote kujijiengea na kudumisha utamaduni wa kujiwekea akiba ya pesa kwa ajili ya malengo mbalimbali katika benk ya amana ili wapate kufurahia huduma bora zitowelewazo kwa ufanisi na weledi wa hali ya juu.


Meneja masoko wa Bank ya Amana Ndugu DASSU MUSSA akifafanua jambo kwa wanahabari ambao walifika kushughudia Utoaji wa zawadi hizo katika Banda lao lililopo katika maonyesho ya saba saba ambayo ndiyo yanaelekea ukingoni 

Ameongeza kuwa kampeni ya faidika na amana bank ni mwanzo tu wa kampeni za bank hiyo zitakazohusisha wateja kuweka fedha na kujishindia zawadi mbalimbali kutoka amana bank ukiachia faida nyingine zipatikanazo kwa wateja kujiwekea akiba huku akisema kuwa wanatarajia kutangaza kampeni nyingine kubwa itakayowezesha wateja wengiine Zaidi kujishindia zawadi lukuki kutokana na kujiwekea utaratibu wa kuweka akiba zao amana Bank Bank ambayo inafwata misingi ya kiislam kikamilifu.

MABADILIKO MADOGO UTEUZI WA WAKURUGENZI.


Thursday, July 7, 2016

KAMATI YA MAADILI TFF YAMFUNGIA JERRY MURO MWAKA MMOJA NA FANI MILIONI 3.


MKUU wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Yanga, Jerry Muro (pichani) amefungiwa mwaka mmoja kujihusisha na masuala ya soka pamoja na kutozwa faini ya Sh. Milioni 3, baada ya kikao cha Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kilichokaa leo kwenye Makao Makuu ya Shirikisho hilo, chini ya Mwenyekiti wake, Wakili Wilson Ogunde 

Muro amefungiwa baada ya kukutwa na hatia katika mashitaka mawili kati ya matatu yaliyowasilishwa na TFF mbele ya Kamati ya hiyo, ambayo ni kudharau maamuzi ya Kamati ya Nidhamu ya TFF mwaka 2015 alipotakiwa kulipa faini ya Sh. Milioni 5 baada ya kufanya makosa, lakini amekaidi kulipa hadi leo, akahukumiwa kutengana na kutojihusisha na masuala ya soka kwa mwaka mmoja, wakati shitaka lingine ni kuchochea vurugu na kuhatarisha amani kuelekea mchezo wa Kundi A Kombe la Shirikisho kati ya Yanga na TP Mazembe ya DRC.

Katika shitaka hilo, Jerry alidaiwa kuwashawishi mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu yao na kutowapa nafasi watani wao wa jadi (Simba) kuingia kwenye mchezo huo ambao timu yake ilifungwa bao 1-0 na Mazembe Juni 28, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 

Hata hivyo, Jerry Muro alifanikiwa kuishinda TFF katika shitaka la kupingana na maamuzi ya shirikisho hilo juu ya masuala ya utoaji wa haki za matangazo ya Televisheni.

“Kamati ilisikiliza kwa makini taarifa zake alipokuwa anazungumza na vituo vya Redio na kugundua alikuwa sahihi, hivyo hapa hana hatia,”kimesema chanzo.Hata hivyo, Jerry Muro amehukumiwa wakati mwenyewe hakuwepo kwenye kikao na inadaiwa hakutoa taarifa ya maandishi juu ya kutohudhuria kwake.

Badala yake, imeelezwa Katibu wa Yanga, Baraka Deusdedit alifika mapema leo kabla ya kikao kwa ajili ya kutoa taarifa ya mdomo kwamba Muro amekwenda kwao Kilimanjaro kusafisha makaburi ya wazee wake. 

Lakini Kamati ikaamua kuendelea na kikao kwa mujibu wa kanuni na hatimaye kuchukua hatua ilizochukua. Hata hivyo, Muro ana haki ya kukata rufaa Kamati ya Rufaa ya TFF.