Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda, akizungumza wakati alipotembelea Chuo cha Wakala wa Maendeleo ya uongozi wa Elimu (ADEM) kilichopo mjini Bagamoyo.
........................................................................
Na Athumani Shomari.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda amesema serikali chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan itajenga vyuo vya VETA katika kila wilaya nchini.
Waziri, Prof. Mkenda aliyasema hayo hivi karibuni alipokuwa akizungumza katika ziara aliyoifanya Chuo cha Wakala wa Maendeleo ya uongozi wa Elimu (ADEM) kilichopo mjini Bagamoyo, ambapo alisema Rais Samia tayari ameilekeza Wizara ya Elimu kuwa, kila wilaya iwe na chuo cha VETA.
Alisema tayari wizara ya elimu imejipanga kutekeleza maelekezo ya Rais samia ya kujenga chuo cha VETA kila wilaya ambapo wilaya zote 64 zitajengwa kwa mkupuo pamoja na kimoja kitakachojengwa mkoani Sngwe.
Prof Adolf Mkenda, aliyasema hayo kufuatia ombi la Mbunge wa Bagamoyo, Muharam Mkenge aliyemuomba Waziri huyo wa Elimu kujenga chuo cha VETA katika jimbo la Bagamoyo ili vijana wa Bagamoyo waweze kujifunza fani mbalimbali katika chuo hicho.
Mkenge alisema kwa sasa Bagamoyo inakuwa kwa kasi katika uwekezaji wa viwanda na kutoa fursa mbalimbali kwa vijana wazawa wenye ujuzi wa fani mbalimbali na kuongeza kuwa fursa hizo hazitakuwa na faida kwa vijana wa Bagamoyo ikiwa hawatakuwa na ujuzi wa fani yoyote.
Aliongeza kwa kusema kuwa kwa sasa kuna ushindani mkubwa katika soko la ajira hivyo uwepo wa chuo cha VETA chenye kutoa ujuzi wa aina mbalimbali kutasaidia kwaa vijana wa Bagamoyo kukabiliana na ushindani katika soko la ajira na kufaidika na uwekezaji unaofanyika katika jimbo hilo.
Alisema tayari mchakato wa kupata eneo la kujenga chuo hicho kwa Bagamoyo umeshakamilika na kupata eneo lenye ukubwa ekari 38 ambzo zitatumika kujenga chuo cha VETA.
Aidha, Mbunge Muharam Mkenge alitumia nafasi hiyo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuelekeza fedha za elimu katika jimbo la Bagamoyo hali iliyopelekea kuanzishwa kwa shule mpya za sekondari ambazo zimesaidia kuwapungzia watoto kwenda umbali mrefu kufika shuleni.
Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Muharami Mkenge, akizungumza mbele ya Waziri wa Elimu, katika Chuo cha Wakala wa Maendeleo ya uongozi wa Elimu (ADEM) kilichopo mjini Bagamoyo.
Katikati ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda, wakwanza kulia ni Mkurugenzi wa Fedha, Mipango na Utawala wa ADEM, Dkt. Emanuel Molel, wa pili kulia ni Mwakilishi wa Kamishna wa Elimu, Bw. Manori Venance, na watatu kulia ni Mwenyekiti wa bodi ya ushauri ADEM, Dkt. Naomi Katunzi, kutoka kushoto wa kwanza ni Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Muharami Mkenge, wapili kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Halima Habib Okash, na watatu kushoto ni Mtendaji Mkuu wa ADEM, Dkt. Siston Masanja.
No comments:
Post a Comment