Posts

SERIKALI KUJENGA VETA KILA WILAYA.

Image
    Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda, akizungumza wakati alipotembelea Chuo cha Wakala wa Maendeleo ya uongozi wa Elimu (ADEM) kilichopo mjini Bagamoyo. ........................................................................ Na Athumani Shomari. Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda amesema serikali chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan itajenga vyuo vya VETA katika kila wilaya nchini. Waziri, Prof. Mkenda aliyasema hayo hivi karibuni alipokuwa akizungumza katika ziara aliyoifanya Chuo cha Wakala wa Maendeleo ya uongozi wa Elimu (ADEM) kilichopo mjini Bagamoyo, ambapo alisema Rais Samia tayari ameilekeza Wizara ya Elimu kuwa, kila wilaya iwe na chuo cha VETA. Alisema tayari wizara ya elimu imejipanga kutekeleza maelekezo ya Rais samia ya kujenga chuo cha VETA kila wilaya ambapo wilaya zote 64 zitajengwa kwa mkupuo pamoja na kimoja kitakachojengwa mkoani Sngwe. Prof Adolf ...

WAZIRI WA ELIMU AKEMEA WIZI WA MITIHANI.

Image
  Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda, akizungumza wakati alipotembelea Chuo cha Wakala wa Maendeleo ya uongozi wa Elimu (ADEM) kilichopo mjini Bagamoyo, february 17, 2023. ................................................................ Na Athumani Shomari. Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda, amesema serikali haitafumbia macho wale wote watakaojihusisha na kuvujisha mitihani kwa namna yoyote ile.   Waziri Mkenda aliyasema hayo February 17, 2023 alipotembelea Chuo cha Wakala wa Maendeleo ya uongozi wa Elimu (ADEM) kilichopo mjini Bagamoyo   ambapo alisema kitendo cha kuiba au kuvujisha mitihani ni kitendo cha dhulma dhidi ya wale wanaojituma kufanya mitihani kwa akili zao.   Alisema tayari baadhi ya watu walioripotiwa kujihusisha na wizi wa mitihani wameshaanza kuchukuliwa hatua ikiwemo kukamatwa na jeshi la polisi na kuanza kuwahojiwa.   Prof. Mkenda amewapongeza polisi nchini kwa kufuatilia matukio ya wizi ...