Posts
RC. NDIKILO AWATOA HOFU BAGAMOYO NA KIBAHA.
- Get link
- X
- Other Apps
By
BAGAMOYO KWANZA BLOG
-
Naomba nichukue fursa hii kuwahakikishia wananchi wa maeneo ya Kibaha na Bagamoyo waliokuwa wanahudumiwa na substation ya Mlandizi iliyopata msukosuko jana wa kuungua moto kwenye moja ya transfoma zake kwamba juhudi zinafanyika ndani ya shirika la TANESCO kufunga transforma nyingine ili nishati ya umeme iendelee kupatikana majumbani kwetu na kwenye maeneo ya uwekezaji vikiwemo viwanda. Serikali yetu imejipanga vizuri ili kuhakikisha kwamba tatizo hili halitaathiri shughuli ze tu za kila siku za kujiletea maendeleo na kukuza uchumi wa mkoa wetu na nchi yetu kwa ujumla. Hatua za muda mfupi tayari zimeshachukuliwa na shirika la TANESCO ili tuendelee kupata huduma ya nishati ya umeme katika maeneo ya Kibaha na Bagamoyo. TANESCO itarejesha tranforma hiyo kubwa kama iliyokuwepo hapo awali ili iendelee kuhudumia viwanda vyetu. Naomba tuwe na subira. IMETOLEWA NA MKUU WA MKOA WA PWANI MHANDISI EVARIST NDIKILO. Hali ilivyokuwa katika kituo...
AMIRI JESHI MKUU RAIS MHE. DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AMETUNUKU KAMISHENI KWA MAAFISA WAPYA WA JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA (JWTZ) 146 IKULU JIJINI DAR ES SALAAM
- Get link
- X
- Other Apps
By
BAGAMOYO KWANZA BLOG
-
Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF) Jenerali Venance Mabeyo na Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Monduli Brigedia Jenerali Steven Mnkande wakati wakielekea kwenda kupiga picha za kumbukumbu Ikulu jijini Dar es Salaam. Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua Gwaride la heshma lililoandaliwa na Maafisa Wanafunzi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kabla ya kuwatunuku Kamisheni Maafisa wapya 146 wa kundi la 65 la mwaka 2018 katika viwanja wa Ikulu jijini Dar es Salaam. Maafisa Wanafunzi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakitoka katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya kutunukiwa Kamisheni na Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli. Maafisa Wanafunzi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakila k...