KAMANDA wa polisi mkoani Pwani ,kamishna msaidizi wa polisi (ACP ) Jonathan Shanna ,amesema amejipanga kupambana na wahalifu mbalimbali kwa kuwasaka uvungu kwa uvungu. Aidha amewataka wakulima na wafugaji kuheshimiana kwa lengo la kuondoa migogoro baina yao . Mbali na hayo amewaonya madereva wa vyombo vya moto ikiwemo mabasi yaendayo mikoani na magari madogo kutii sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali za barabarani zinazotokea mara kwa mara barabara kuu ya Dar as salaam -Morogoro . Akizungumza na baadhi ya viongozi wa jeshi la polisi Mkoani Pwani pamoja na waandishi wa habari Mkoani hapo,kamanda Shanna ,aliomba ushirikiano kwa askari polisi,waandishi hao pamoja na jamii . Shanna alieleza kwamba ,atakwenda kitanda kwa kitanda ,pori kwa pori kuhakikisha wanapunguza matukio ya kiuhalifu . Alisema yeye ni mgeni lakini ni mtu wa kazi alitaka ushirikiano kwa askari wa jeshi hilo mkoani hapa na wananchi baada ya kuchukua nafasi ya kamishna msaid...