Monday, August 1, 2022

DC MTANDA ASITISHA ZABUNIMPYA YA WAKANDARASI WANAOZOA TAKA HADI KUFANYIKA KWA TATHIMINI .

 No description available. 

Mkuu wa wilaya ya Arusha,Said Mtanda akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na sakata hilo jijini Arusha .

**************************

Julieth  Laizer ,Arusha

Arusha.Mkuu wa wilaya ya Arusha ,Said Mtanda amesitisha  zabuni mpya ya wakandarasi wa kuzoa taka ngumu iliyokuwa ianze agosti mosi  mwaka huu  hadi kufanyika kwa tathimini baada ya kuwepo tuhuma kuna waliopewa zabuni hawana sifa.

 

Mtanda ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha na ambapo alisema kuwa, amekuwa akipokea malalamiko mbalimbali juu ya wakandarasi hao kusitisha zoezi la ukusanyaji taka kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kushindwa kujua hatma yao kutokana na kuambiwa mikataba yao imeisha.

 

 “Mimi malalamiko hayo niliyapata na ninachotaka kusema hapa ni kuwa nawaomba wakandarasi wote waliokuwa wanazoa taka waendelee na shughuli zao za uzoaji taka kama kawaida hadi pale watakapofanyiwa tathmini  kila mmoja na kuweza kupewa mikataba mipya ila kwa sasa hivi nawaombeni mndelee na shughuli zenu kama kawaida.”amesema.

 

Mtanda amesema kuwa,kutokana na kuwepo kwa malalamiko mbalimbali ni lazima wakae chini wafanye tathmini ya utendaji kazi wa wakandarasi hao kipindi cha nyuma kama walifanya vizuri na kama kweli wanakidhi vigezo vya kuendelea na mchakato huo wa uzoaji taka kisheria  na sio vinginevyo.

 

“Nitamwandikia Mkurugenzi  wa Jiji barua kutaka zoezi hilo   na barua hizo zisitishwe na ifanyike tathmini ya kina juu mkandarasi gani alifanya kazi nzuri,yupi aliyelipa fedha ya serikali inavyotakiwa,na wapi hawakufanya vizuri  kwa mwaka huo uliopita na yupi bado anadaiwa fedha na serikali na tathmini hiyo itafanywa na kamati ya  pamoja katika idara ya manunuzi ya jiji,idara ya mazingira ya jiji ili haki iweze kutendeka sitaki mambo ya ujanja katika hili “amesema Mtanda.

 

Ameongeza kuwa, kata ambazo zitaondolewa wakandarasi baada ya tathimini ni zile ambazo zimegundulika kutofanya vizuri na hawataweza kuendelea tena hakuna biashara za kueleana katika hilo,watakaoendelea na zoezi hilo ni wale  waliofanya vizuri na wenye magari ya taka ili waendelee kuwekeza ,hivyo manung’uniko yote yakitolewa ndo mikataba mipya itatolewa na watu kuendelea na kazi katika maeneo yao waliyoomba na sio vinginevyo.

 

Aidha ameagiza  maafisa tarafa wote kuleta orodha ya wakandarasi ambao hawajakusanya taka taka katika kipindi hiki  kwa sababu za kutokuwa na uhakika kama watapatia mikataba mipya au lah kwani kwa kufanya hivyo ni kuhujumu juhudi za serikali za usafi wa mji na mazingira.

 

“Unajua kilichofanyika na jiji la Arusha ni kutoa barua la kusudio la kuingia mkataba rasmi ya wazoa taka katika maeneo mbalimbali,na wakiweka kusudio hatua inayofuata ni kusaini mikataba maalumu kwa ajili ya kuendelea na kazi hizo kila mmoja katika eneo aliloomba baada ya kukidhi vigezo Sasa nasitisha zoezi hilo la utoaji mikataba hadi tathmini ifanyike na kila mmoja ajiridhishe.”amesema Mtanda.

 

Aidha Mtanda ametoa  wito kwa wazoa takataka wahakikishe wanaweka  turubali ya kudhibiti taka zisimwagike  na wataoenda  kinyume cha hapo watachukuliwa hatua kali za kisheria .

 

Monday, July 11, 2022

TAASISI YA JAI YAWAFARIJI WAGONJWA KWA MISAADA, SHEIKH MKOA SINGIDA ANENA MAZITO.

 No description available.

Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issa Nassoro akimuombea dua mmoja wa wagonjwa aliyelazwa kwenye hospitali hiyo.

...............................................

Na Dotto Mwaibale, Singida

SHEIKH wa Mkoa wa Singida, Issa Nassoro amewaongoza wanajumuiya wa Taasisi Jamiyatul Akhlaaqul Islam (JAI) kwa kuwapatia msaada wa chakula na vinywaji wagonjwa waliolazwa katika Hospitali ya Mkoa na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida Mandewa.

Taasisi hiyo ambayo inajihusisha  kutoa huduma kwa wagonjwa na yatima imetoa misaada hiyo ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Sikukuu ya Eid Al-Adha ilyofanyika leo.

Akizungumza kabla ya kutoa msaada huo, Sheikh Nassoro alisema jambo linalofanywa na taasisi hiyo ni jambo jema kwani limejaa ucha Mungu na kila mwanajumuiya hiya malipo yake yapo kwa Mwenyezi Mungu.

“Hiki mnacho kifanya ni chema mmeacha shughuli zenu, waume zenu, watoto na marafiki badala ya kusherehekea nao sikukuu hii mmeona mje kutoa faraja kwa kuwatembelea hawa wagonjwa kwa kuwaletea chakula na vinywaji hongereni sana na dhawabu yenu mtaipata,” alisema Nassoro.

Naye Katibu wa Taasisi hiyo Mkoa wa Singida, Ramadhani Mtipa alisema kila sherehe za Eid wamekuwa wakiwatembelea wagonjwa na kuwafariji kwa kuwapa chakula, vinywaji  na vitu vingine kama saburi na kuwa jumuiya hiya hiyo inaendesha shughuli zake nchi nzima.

Amirat wa Taasisi hiyo Aisha Asi alisema wamekuwa wakitoka msaada wa kuwatembelea wagonjwa, yatima na wale wasio na ndugu kwa kuwapatia msaada wa chakula bila ya kubagua  dini na kuwa kazi hiyo wamekuwa wakiifanya asubuhi na jioni.

No description available.

Wanajumuiya wa Taasisi inayojihusisha na kutoa huduma kwa wagonjwa na yatima ya  Jamiyatul Akhlaaqul Islam (JAI) wakiwa na bidhaa mbalimbali na vyakula walivyotoa msaada kwa wagonjwa waliolazwa Hospitali ya Mkoa wa Singida ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Sikukuu ya Eid al-Adha 2022.

No description available.

Wanajumuiya wa Taasisi inayojihusisha na kutoa huduma kwawagonjwa na yatima ya  Jamiyatul Akhlaaqul Islam (JAI) wakiwa na bidhaa mbalimbali na vyakula walivyotoa msaada kwa wagonjwa waliolazwa Hospitali ya Mkoa wa Singida ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Sikukuu ya Eid al-Adha, 2022.

No description available.

Amirat wa Taasisi hiyo Aisha Asi akitoa msaada kwa mmoja wa wagonjwa.

No description available.

Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issa Nassoro akitoa msaada wa chakula kwa ndugu wa mgonjwa aliyelazwa kwenye hospitali hiyo.

 No description available.

Mmoja wa mtoto kutoka Taasisi hiyo (kulia) akionesha upendo wa kumpatia maji mtoto mwenzake aliyelazwa kwenye Hospitali hiyo kwa matibabu.

No description available.

Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issa Nassoro (katikati) akiwaongoza wanajumuiya hao kwenda kutoa msaada huo