Thursday, May 25, 2017

CCM YAITAKA SERIKALI KUCHUKUA HATUA MAUAJI YA PWANI.

POLEP
Chama Cha Mapinduzi kimeitaka Serikali kuchukua hatua za haraka kuhusu matukio ya Mauaji yanayoendelea katika Wilaya za Kibiti, Mkutanga na Rufiji Mkoani Pwani ili kuepusha mauaji hayo kuendelea kutokea.

          Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, HUMPHEY POLEPOLE, amesema hayo Jijini Dar es salaam   leo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mauaji yanayoendelea katika Wilaya hizo.

          POLEPOLE pia amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha vinaelekeza akili, nguvu zao katika Wilaya hizo kwa kuwa maujia hayo yanasababisha kuzorota kwa shughuli za maendeleo.

          Amesema chama kwa muda mrefu kimekaa kimya kikiamini hatua zitachukuliwa kwa kuwa wanachama wake na watendaji wameendelea kupoteza maisha ambapo amesema kwa sasa imetosha.

Kuhusu suala la uchaguzi ambao unaendelea ndani ya Chama hicho amesema mauaji hayo yanakiweka Chama katika mazingira magumu ya kufanya chaguzi zake hivyo ni vema hatua zikachukuliwa sasa.

          Katika hatua nyingine, POLEPOLE amesema Chama kimeipongeza Kamati Maalum ya kuchunguza Mchanga wa Madini kwa kazi nzuri iliyofanywa sanjari na kuwaomba wananchi kumuunga mkono Rais JOHN MAGUFULI kwa hatua alizozichukua kwa watendaji kutokana na Ripoti ya Mchanga wa Madini.

KIBAHA YAZINDUA JUKWAA LA UWEZESHAJI WANAWAKE KIUCHUMI

MSHAMA
Mkuu wa wilaya ya Kibaha ,Assumpter Mshama na mbunge wa viti maalum mkoani Pwani Subira Mgalu mwenye kiremba cha blue wakitembelea mabanda mbalimbali ya bidhaa za wajasiriamali wa Mji wa Kibaha ,baada ya kuzindua jukwaa la wanawake la kuwawezesha kiuchumi mjini hapo .(picha na Mwamvua Mwinyi )
....................


WILAYA ya Kibaha imezindua jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi na kuchagua viongozi wake watakaoongoza katika kipindi cha miaka mitano.

Jukwaa hilo limempitisha Betty Msimbe kuwa mwenyekiti huku Sada Duda akichaguliwa katibu kipindi hicho .

Afisa maendeleo ya jamii halmashauri ya Mji wa Kibaha ,Leah Lwanji aliwataja viongozi hao ambao wamechaguliwa na akina mama wajasiriamali mbalimbali .

Alieleza kuwa kuundwa kwa jukwaa hilo kutasaidia kuwezeshwa vikundi vya akinamama wajasiriamali kirahisi .

Leah alisema wanawake waungane waache kujiweka binafsi ili kupiga hatua kimaendeleo na kiuchumi .

Hata hivyo alisema ,katika kipindi cha mwezi april hadi may mwaka huu halmashauri ya Mji huo imechangia sh .mil 56 kwa kukopesha vikundi 34 vya wanawake ,kwenye kata 14 zilizopo mjini humo .

Leah alielezea kwamba ,July hadi desemba mwaka 2016 ,walitoa mil .16 kwa vikundi Tisa na Jan – march mwaka 2017 wametoa mil.70 kwa vikundi 46 .

Alisema kwa upande wa fungu la vijana afisa maendeleo huyo ya jamii ,wametoa asilimia kumi katika mapato ya ndani kwa kutoa sh.mil 32 zilizopelekwa saccos ya vijana .

“Tunamkabidhi mkuu wa wilaya ya Kibaha hundi ya sh.mil 56 kutoka NMB itakayogawiwa katika vikundi 34″ alisema Leah .

Nae diwani wa viti maalum Mji wa Kibaha ambae pia ni katibu wa jukwaa la uwezeshaji mkoani Pwani ,Elina Mgonja alisema ,umoja wao utawawezesha kuwa na sauti kupigania fursa za kiujasiriamali .

Alisema wamejipanga kuthubutu kuanzisha miradi mbalimbali na kushikana mkono ili kujikwamua kimaisha .

Elina alitoa rai kwa wanawake kujitambua na kujithamini .

Nae mkuu wa wilaya ya Kibaha ,Assumpter Mshama ,aliwataka wanawake wathubutu kuanzisha viwanda vidogo na vikubwa kwenda na sera ya uchumi wa viwanda .

Aliwaomba wajenge tabia ya kugombea nafasi za uongozi bila kuwaachia wanaume .

Assumpter alisema kinamama waamke waache kulala kwani sio wakati wa kuzorota na kusemana majungu na kukatishana tamaa .

YANGA YAPOKELEWA KWA SHANGWE BUNGENI LEO MAY 25, 2017.

unnamed
Mabingwa wa Ligi kuu Tanzania Bara Dar Young African “Yanga” kwa msimu 2016/2017 wakifurahia na mawaziri na wabunge mara baada ya kulileta kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara Bungeni Mjini Dodoma.
 YAN
Mabingwa wa Ligi kuu Tanzania Bara Dar Young African “Yanga” kwa msimu 2016/2017 wakifuatilia mijadala mbalimbali Bungeni Mjini Dodoma.
MBAO
Timu ya Mpira ya Mbao FC kutoka Mwanza wakifuatilia mijadala mbalimbali Bungeni, Mbao Fc wapo Mjini Dodoma kwa ajili ya maandalizi ya Mchezo wa fainali za FA kati yao na Simba Fc zitakazofanyika katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma Jumamosi ya May 27, 2017.
 BU
Mbunge wa kuteuliwa Mhe. Abdallah Bulembo akiuliza swali katika kikao cha thelasini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017.
FT
Mbunge wa Mbulu Vijijini Mhe. Flatei Massay akiuliza swali katika kikao cha thelasini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017.
 MC
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi  Mhe. Mwigulu Nchemba akijadiliana jambo na Mbunge wa Arusha Mjini  Mhe. Godbless Lema Mbunge wa Arusha Mjini katika kikao cha thelasini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017.
 BV
Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akijadiliana jambo na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Dkt Medard Kalemani katika kikao cha thelasini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017.