Monday, October 31, 2016

BONDIA THOMAS MASHALE ADAIWA KUUWAWA DAR ES SALAAM.

thomas-mashali
Bondia mtanzania Thomas Mashali maarufu kama (Simba Asiyefugika), amekutwa amekufa huku akiwa na majeraha  usiku wa kuamkia leo huko maeneo ya Kimara jijini Dar es salaam kutokana na sababu ambazo hazijajulikana mpaka sasa.

Kwa mujibu wa katibu mkuu wa Oganization ya ngumi za kulipwa nchini PST Antony  Lutta, amesema kuwa taarifa walizozipata ingawa bado  hazijathibitishwa inaonyesha Thomas Mashali ameuwawa.

Lutta ameongeza kwamba marehemu enzi za uhai wake amekuwa na tabia ya kufanya vurugu akiwa amelewa sasa hatujui nini kimempata ambapo  mwili wake umekutwa maeneo ya Kimara jijini Dare s salaam ukiwa na majeraha baada ya hapo  ulichukuliwa na kupelekwa kuhifadhiwa katika  hospitali ya taifa muhimbili.

Marehemu Mashali kabla ya kifo chake alikuwa  acheze na bondia Chimwemwe kutoka nchini Malawi ,pigano ambalo lilipangwa kufanyika mkoani  morogoro siku ambayo bondia mwenzake Dullah Mbabe alipangwa kucheza pigano la utangulizi.

Mashali ambaye  jina lake la  kuzaliwa ni Christopher Fabian Mashali,aliyezaliwa Septemba 09 mwaka 1989,ameacha rekodi ya kushinda mapambano 19 kati ya hayo 9 akishinda kwa KO,amepoteza mapambano 5 kati ya hayo amepigwa kwa KO mapambano 4 huku akitoka sare pigano moja tu.

Marehemu ameacha mke na watoto.
CHANZO FULL SAHNGWE BLOG.

Sunday, October 30, 2016

DC. KONGWA AZINDUA KAMPENI YA ONDOA NJAA KONGWA (ONJAKO).


Mkuu wa wilaya ya Kongwa Mh Deo Ndejembi akizindua kampeni ya kuondoa Njaa wilaya ya Kongwa, (ONJAKO)
 

Mkuu wa wilaya ya Kongwa Mh Deo Ndejembi akizungumza mara baada ya kuzindua kampeni ya kuondoa Njaa wilaya ya Kongwa, (ONJAKO)
 ...........................................


Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma Mhe Deo Ndejembi ameanzisha kampeni ya kuondoa Njaa wilaya ya Kongwa, (ONJAKO) yenye dhamira ya kuwasaidia wananchi kuondokana na hali yanjaa ambayo ni kadhia kubwa katika maeneo mbalimbali ya Wilaya hiyo sambamba na Taifa kwa ujumla.

Kuanzishwa kwa Kampeni ya Okoa njaa Wilaya ya Kongwa imejili wakati Mkuu huyo wa Wilaya ya Kongwa Akizungumza na Wakuuwa Idara na vitengo, Madiwani wa Kata zote zilizopo Wilayani humo, Watendaji wa Kata, Maafisa Tarafa, Waratibu Elimu Kata, Wenyeviti wa Vijiji vyote 87 vya Wilaya ya Kongwa na watendaji wao, pamoja na wadau waalikwa na Kilimo.

Akizindua kampeni hiyo Dc Ndejembi alisema kuwa Kampeni hiyo imezinduliwa Mwezi Octoba kwa ajili ya msimu wa mwaka 2016/2017 na inatarajiwa kuwa kampeni Endelevu katika kipindi cha Miaka mitano.
 
Ameeleza kuwa huu ni mkakati maalumu katika Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma ili kukabiliana na hali ya Ukame ambayo ni tatizo sugu katika maeneo mengi nchini.

Kutokana na hayo DC Ndejembi ameagiza kuwa na kilimo cha Mtama zaidi kuliko Mahindi. Kwani Wilaya ya Kongwa ina Kaya 59141, na kila kaya kama ikilima Heka mbili (2) za Mtama, Mavuno itakuwa Tani 71000, za Mtama sawa na 83% ya hitaji la chakula Wilayani Kongwa.

Katika kukabiliana na njaa mahitaji mengine mahususi yametajwa ikiwa ni pamoja na Kuongeza uzalishaji wa mtama toka tani 1/ Hekta mwaka 2016 hadi tani3/hekta ifikapo mwezi June 2021, Kuongeza Uzalishaji wa Muhogo mbichi toka tani 6/hekta Mwaka 2016 hadi tani 10 hekta mwaka 2029, Kuongeza uzalishaji wa zao la Alizeti toka tani 1.2/ hekta mwaka 2016 hadi tani 1.8/hekta mwaka 2021.

Pia Mhe Ndejembi alisema kuwa mahitaji mengine ni pamoja na Kuongeza uzalishaji wa ufuta toka tani 0.5/hekta mwaka 2016 hadi tani 1.2/hekta ifikapo june 2021, pamoja na Kuongeza pato la Mtu/watu toka Tsh 500,000/= Mwaka 2016 hadi Tsh 800,000/= June 2021.

DC Ndejembi ameagiza kufanyika utaratibu wa kuhakikisha kila kaya inalima Heka zisizopungua mbili (2) za Mtama, Mbili za Mahindi, kulingana na eneo husika wakishauriwa na maafisa ugani lakini mtama ni lazima kwa kila kaya hata kama analima mahindi.

Pia amewaagiza vijana wote wasio na kazi Wilayani Kongwa wapewe Hekari mbili kila mmoja ili waache kucheza pool table na kujihusisha na vikundi Ovu vya wizi na matumizi ya Dawa za kulevya.

Saambamba na hayo Mhe Ndejembi aamepiga marufuku kuchezwa mchezo wa Pool Table mpaka ifikapo majira ya saa 10 jioni, hivyo kwa yeyote atakaye kiuka utaratibu huo atakuwa amekiuka amri halali ya serikali.



DC. MUHEZA,HAJAT, MHANDISI, MWANAASHA TUMBO, ATEMBELEA ZAHANATI MPYA YA KIJIJI CHA ZENETI

 Mkuu wa wilaya ya Muheza,Haja Mhandisi,Mwanasha Tumbo katika akiongozwa na Diwani wa Kata ya Potwe,Rashid Mdachi na Mwenyekiti wa Serikali ya  Kijiji cha Zeneti wakitembelea Jengo jipya la Zanahati ya Zeneti iliyojengwa kwa ushirikiana baina ya Halmashauri,Wananchi na Shirika la World Vision na Mbunge wa Jimbo hilo ambalo limegharimu kiasi cha milioni 35.2.
 

Kulia ni Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Muheza,Mathew Mganga akimuongozwa Mkuu wa wilaya ya Muheza, Hajat, Mhandisi Mwanasha Tumbo aliyetembelea zahanati ya Zeneti kuona jinsi inayoendelea na ujenzi wake kushoto ni Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Zeneti
 

Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya ya Muheza,Mathew Mganga kulia akisisistiza jambo kwa Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo wa pili kutoka kushoto kuhusu ujenzi wa zahanati hiyo katikati ni Diwani wa Kata ya Potwe,Rashid Mdachi.
 

Diwani wa Kata ya Potwe,Rashid Mdachi akimuonyesha kitu Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat, Mhandisi Mwanasha Tumbo wa pili kulia
 

Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo katikati akisisitiza jambo kwa Diwani wa Kata ya Potwe,Rashid Mdachi.
 

Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo katikati akiangalia baadhi ya vyoo vya Zahanati hiyo wakati alipoitembelea kuikagua na kuona namna ujenzi wake unavyoendelea.
 

Diwaniwa Kata ya Potwe,Rashid Mdachi akizungumza na wananchi  katika ziara hiyo ya Mkuu wa wilaya katika Zahanati ya Kijiji cha Zeneti