Saturday, August 19, 2023

DR JAFO AZINDUA MIRADI YA MAJI KISARAWE VISIMA 140 HUKU AKITAKA JAMII KUENDELEZA AJENDA YA RAIS SAMIA YA KUTUNZA MAZINGIRA NA VYANZO VYA MAJI

 

MWANDISHI WETU 

Pwani-Kisarawe


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Dkt Selemani Saidi Jafo amezindua mradi Mkubwa wa maji safi na Salama wa visima 140 Kisarawe 19.08.2023.


Akizungumza wakati wa ufunguzi huo Kata ya Mzenga Mhe Dkt Jafo aliwataka Wana Kisarawe kutunza vyanzo vya maji na Mazingira ya visima ili kudumisha uhai wa visima Hivyo katika jamii,


*"Natoa wito Kwa jamii ya Kisarawe na Tanzania Kwa ujumla kuyatunza Mazingira haya tusiyaharibu ili kupata maji safi na Salama Kwa muda mrefu alisisitiza Mhe Dkt Jafo*"


*"Lengo la visima hivi ni kuhakikisha jamii yetu haipati tabu na Inapata maji Kwa urahisi mno hivyo tuyatunze mazingira haya alimalizia Mhe Dkt Jafo*"


Jumla ya visima 140 vinaendelea kuchimbwa katika Kata za Mzenga, Vihingo,Marui na Vikumburu Kwa msaada wa Taasisi na Kwa kushirikiana na Ofisi ya mbunge Jimbo la Kisarawe kwa Mwaka 2023,


Hata Hivyo akizungumza Kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya Kisarawe Bi Khadija Mwinuka alishukuru Taasisi hiyo na Ofisi ya mbunge Kwa kuchimba visima vya maji karibu na Jamii na shule,


*"Kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya Kisarawe tunakupongeza sana mhe Dkt Jafo Kwa kutatulia shida hii kwa Wanafunzi wetu hasa hapa shule ya Vihingo ambapo Wanafunzi wetu wa Sekondari ya Dkt Selemani Jafo wanasoma tunaamini kabisa wataenda kufanya vyema na kuengeza wastani wa ufaulu kutokana na kupata maji alimalizia Bi Khadija*


Nae kwa upande wake meneja wa mamla ya maji Kisarawe Eng Evagalista Kahwili alitoa wito Kwa jamii kutunza Mazingira pamoja na vyanzo vya maji ili jamii iwe salama na kuweza kupata maji zaidi na zaidi Kwa muda mrefu


*"Ndugu zangu wa Kisarawe tunatoa wito kwenu kuungana na Mhe Rais Dkt Samia na Waziri wetu Dkt Jafo katika kusisitiza juu ya kutunza miundombinu ya visima hapa katika Kata zote za Vihingo, Mzenga, Vikumbumburu, Marui na chole ili viweze kuwahudumia Kwa muda mrefu alisisitiza Meneja Eng Kahwili*" 


SERIKALI, BUNGE WAAZIMIA KUTOKOMEZA MALARIA IFIKAPO 2030

 


Na WAF, Dodoma 


Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kushirikiana na kamati ya afya ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imejadili afua za kutokomeza Malaria ifikapo Mwaka 2030 ili kuendelea kuimarisha sekta ya afya nchini. 


Hayo yamebainishwa leo Agosti 19, 2023 na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI Mhe. Stanslaus Nyongo wakati akifungua kikao cha siku Mbili chenye lengo la kujenga uwezo Kwa Wabunge na wajumbe wa Baraza la kutokomeza Malaria.


Aidha Mhe. Nyongo amesema kamati ya bunge itashirikiana na Serikali katika kutokomeza malaria kwa kutoa elimu kwa wananchi pamoja na kutumia dawa za viua wadudu ili kuondoa mabaki na mazalia ya mbu.


“Serikali, Bunge na wadau wanapaswa kuweka nguvu na nia katika kutokomeza Malaria ifikapo mwaka 2030 ili kuboresha zaidi Afya za Watanzania na hivyo kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa Taifa letu”, amesema Mhe. Nyongo


Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya Mhe. Godwin Mollel amesema amesisitiza katika kutumika vyema kwa rasilimali ambazo serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwani jitihada za kutafuta pesa ni kubwa katika kuboresha sekta ya afya nchini.


Aidha, Dkt. Mollel amelitaka Baraza la kutokomeza Malaria nchini kusimamia vizuri rasilimali zilizopo za kutokomeza Malaria ili kufikia malengo ya kuutokemeza ugonjwa huo ifikapo 2030. 


“Serikali chini ya Rais Dkt. Samia inahangaika kutafuta hela na kununua rasilimali ili kusaidia kutokomeza Malaria sasa ni vizuri mkazisimamia rasilimali zilizopo”, ameongeza Dkt. Mollel.


Nae, Mwenyekiti wa Baraza la Kutokomeza Malaria nchini Eng. Leodegar Tenga amesema Tanzania imepiga hatua kubwa katika kupunguza idadi ya wagonjwa na vifo kutokana na malaria licha ya changamoto zilizopo, hii ni kufuatia jitihada za Serikali na Wadau katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malaria nchini. 


“Sisi Kama Baraza tunatambua kwamba Tanzania imepiga hatua kubwa katika kupunguza idadi ya wagonjwa na vifo kutokana na malaria, licha ya changamoto zilizopo ikiwemo za kupata rasilimali.









KIKAO CHA WENYEVITI WA BODI MATUKIO KATIKA PICHA

 






MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI YA TAREHE 19 AGISTI 2023.

 




















RAIS DKT. SAMIA NA WAZIRI MKUU MAJALIWA KUFUNGUA KIKAO KAZI ARUSHA.

 

NI UFUNGUZI WA KWANZA WA KIKAO KAZI CHA WENYEVITI NA WAKURUGENZI WA MASHIRIKA YA UMMA NA SERIKALI.*


Na Lucas Myovela _ Arusha.


Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa Kufungua kikao kazi cha wenyeviti na Wakurugenzi wa Mashirika ya Umma pamoja na Taasisi za kiserikali, Pia anatarajiwa kuhudhuria kwenye kilele cha maadhimisho ya Miaka 60 ya kanisa la KKKT ambapo matukio yote hayo yatafanyika Jijini Arusha.


Akiongea na waandishi wa Habari Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela Mapema Agosti 18, 2023, amesema kuwa Mhe, Rais Samia Suluhu Hassan, Mnanmo tarehe 19/8/2023, atafungua kikao kazi cha Wenyeviti na Wakurugenzi wa mashirika ya umma na Taasisi za Serikali,utakaofanuika Ukumbi wa mikutano ya kimataifa, AICC Jijini Arusha.


Pia Mongela ameeleza kuwa kuwa tarehe 21/8/2023, Mhe, Rais Samia, atakuwa mgeni rasmi kwenye madhimisho ya miaka 60 ya Kanisa la Kiinjili la kiluthe

RAIS SAMIA ATENGUA UTEUZI WA KATIBU MKUU WIZARA YA MAJI.

 



Friday, August 18, 2023

COREFA YATANGAZA SAFU YA UONGOZI MKOA WA PWANI.


 



JAJI NONGWA AWATAKA MAHAKIMU WAKAZI WAPYA KUFANYA KAZI KWA UFANISI.

 


Jaji wa Mahakama Kuu, kanda ya Mbeya, Mhe. Victoria Nongwa amewataka Wahe. Mahakimu wakazi wapya wa Mahakama za mwanzo kufanya kazi kwa uweledi, uadilifu na uwajibikaji bila kujali kuwa wao bado ni wageni katika kazi hiyo mpya.

Mhe. Nongwa ametoa kauli hiyo leo Agosti 18, 2023 wakati akifunga Mafunzo Elekezi ya siku tano kwa Mahakimu wakazi wapya wa Mahakama za mwanzo, yaliyokuwa yanafanyika katika Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) wilayani Lushoto mkoani Tanga.

Mafunzo hayo ambayo yaliandaliwa na Mahakama ya Tanzania na kuendeshwa na IJA, yalifunguliwa Agosti 14, 2023 na Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Wilbert Chuma.

Mhe. Nongwa amewaambia Mahakimu hao:"Huna budi kufanya kazi kwa ufanisi na ubora mara tu unapotoka hapa, maana wewe ni Hakimu halisi sio mwanafunzi tena."

Pia amewakumbusha watambue kwamba majalada ya mashauri wanayokwenda kuyashughulikia ni maisha halisi ya mtu na hivyo wanapaswa kuwa makini na uamuzi wao watakaokuwa wanautoa.

Kwa upande mwingine, Mhe. Nongwa amewashauri Mahakimu hao kuzingatia maadili kwa kujiepusha na rushwa kwa kuwa rushwa ni adui wa haki.

Naye mshiriki wa mafunzo hayo ambaye ni Hakimu Mkazi mpya Mhe. Dina Mgoloka ametoa neno la shukrani kwa niaba ya wenzake akiweka wazi kuwa mafunzo hayo yamewapa uamsho wa kufanya kazi.

"Kwa kweli mafunzo haya yote yameweza kuleta uamsho au morali kwetu sisi ya kufanya kazi, nasi tunaahidi kuyabeba kama nyenzo za kutuwezesha kufanya kazi za uhakimu kwa uadilifu, uweledi na uwajibikaji," amesema Mhe. Mgoloka.

Awali, Mkurugenzi Msaidizi wa Mafunzo ya Mahakama ya Tanzania, Bi. Patricia Ngungulu ameishukuru IJA kwa kuendesha mafunzo hayo kwa ufanisi pamoja na kuwashukuru Mahakimu hao kwa utulivu wao wakati wote wa mafunzo.