Monday, September 19, 2022

DARAJA JIPYA LA WAMI KUANZA KUTUMIKA SEPTEMBA 30 MWAKA HUU 2022,


 No description available.

Katibu Wa Itikadi Na Uenezi CCM Ndg. Shaka Hamdu Shaka ,Wananchi na Baadhi ya Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wakipita katika Njia ya Watembea kwa miguu Kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja jipya la Wami ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 89.02 na zaidi ya Sh. bilioni 75 zimepangwa kutumika.

..............................................

 

DARAJA Jipya la Wami lenye urefu wa mita 513.5 na barabara unganishi ya kilometa 3.8 litaanza kutumika Septemba 30, 2022.

 

Akizungumza katika ziara yake leo Septemba 18, 2022 Katibu, wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Shaka Hamdu Shaka amesema serikali imeridhishwa na ujenzi wa daraja hilo la Wami ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 89

-

"Daraja hili lilianza ujenzi mwaka 2018, hadi Rais Samia Suluhu Hassan anaingia madarakani ujenzi ulikua umefika asilimia 47, lakini ndani ya mwaka mmoja wa Rais Samia, kasi imeongezeka kwa asilimia 42 na sasa wataalamu wanatuambia ujenzi umefikia asilimia 89," amesema Shaka na kuongeza

-

“Pongezi zetu ziwafikie wakandarasi ndani ya kipindi kifupi tuliambiwa daraja hili lingeanza kazi Septemba 20 tukasema haitawezekana lianze kazi kabla ya chama kufika hili jambo ni kubwa, ni utekelezaji wa ilani ya CCM ibara 55 (d) (1)....; "CCM inaridhishwa, na kazi zinazofanywa na serikali” alisema

-

Alisema daraja hilo limebeba maslahi mapana ya Watanzania kwa kuwa linakwenda kuunganisha Mikoa yote ya Kaskazini na nchi jirani ikiwemo Kenya hivyo fursa ambazo zitatokana na daraja hilo ni nyingi hasa kiuchumi.

No description available.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka akiwa na viongozi, wana CCM na wataalamu wakipita juu ya Daraja la Wami mkoani Pwani alipotembelea ujenzi wa daraja hilo.

No description available.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka akizungumza na viongozi, wana CCM na wataalamu wakati alipotembelea ujenzi wa Daraja la Wami mkoani Pwani.


Wednesday, August 10, 2022

DC. BAGAMOYO AFANYA KIKAO NA KAMATI YA SENSA WILAYA.

 May be an image of 2 people, people sitting and indoor

Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe Zainab Abdallah, akizungumza katika kikao alipokutana na Kamati za Sensa za Halmashauri za Bagamoyo na Chalinze.

.................................

 

Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe Zainab Abdallah Amefanya Kikao na kamati ya Sensa ya Wilaya pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama (KUU) ya Wilaya kufuatia maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi inayotarajiwa kufanyika tarehe 23/08/2022.

 

Mkuu huyo wa Wilaya pia ameendelea kuwasisitiza Wananchi wa Bagamoyo, wawe tayari kuhesabiwa Tarehe 23 Mwezi huu itakapofika ili kusaidia serikali iweze kupanga Mipango ya maendeleo kwa Miaka 10 ijayo.

 

Alisema ili serikali iweze kupanga mambo mbalimbali ya maendeleo inahitaji kuwa na idadi ya wananchi wake iliyo sahihi kwaajili ya kufikisha huduma za jamii mahitaji yaliyo sahihi.

 

Kikao cha kamati ya sensa kimefanyika ili kufanya tathmini ya mwenendo mzima wa maandalizi ya zoezi la sensa na hali halisi ya mwenendo wa mafunzo ya wataalam na makarani watakao shiriki zoezi hilo adhimu la serikali siku ya tarehe 23 Agosti mwaka huu.

Wakitoa taarifa ya zoezi hilo waratibu wa sensa ya watu na makazi kwa halmashauri zote mbili ya Chalinze na Bagamoyo, walieleza jumla ya makarani 991 wanaendelea na mafunzo kwa siku 15 katika halmashauri ya Chalinze na makarani 418 wanaendelea na mafunzo kwa hamashauri ya Bagamoyo.

 

Katika kikao hicho wajumbe wamekubaliana kwa pamoja kuhakikisha wananchi wanahamasishwa kushiriki katika zoezi la sensa kupitia michezo mbalimbali pia kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

Aidha katika kikao hicho wajumbe walikubaliana kuwa wenyeviti wa vitongoji wahakikishe wanahamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi la sensa na kutoa ushirikiano wa hali ya juu kwa makarani katika kuwaongoza kuwafikia wananchi.

 

Ikumbukwe kuwa Sensa ya Watu na Makazi hufanyika kila baada ya Miaka 10 ambapo Sensa ya Mwaka huu 2022 ni Sensa ya watu na makazi.

May be an image of 3 people and people sitting

 

May be an image of 7 people, people sitting and indoor

 

RC KUNENGE AMEITAKA NDC KUANDAA MCHORO ENEO LA KONGANI YA UWEKEZAJI KIBAHA KWA AJILI YA KUVUTIA WAWEKEZAJI

No description available.

Na Mwamvua Mwinyi, Pwani

 

MKUU wa Mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge amekutana na uongozi wa Shirika la Maendelo la Taifa – NDC kwa mazungumzo ya kuitangaza Kongani ya Viwanda inayomilikiwa na Shirika hilo, Mjini Kibaha na kuhakikisha inaandaa mchoro wa eneo hilo kwa ajili wawekezaji.

 

Mazungumzo hayo yalifanyika kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa huo ambapo Kunenge amemshauri Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo Nicolaus Shombe  kuhakikisha ofisi yake inaandaa mchoro huo ili kuinua uwekezaji.

 

“Ni wajibu wangu kuzisemea taasisi zote zilizopo mkoani kwangu, hivyo mnapaswa kuandaa mchoro wa eneo hilo, mnipatie ili tuweze kulitangaza kwa wawekezaji wanaotafuta maeneo ya uwekezaji,” alisema Kunenge.

 Akifafanua faida za uwekezaji, Kunenge ameeleza kuwa unasaidia katika kufanikisha malengo ya mkakati mkubwa wa mkoa uliolenga kuongeza vyanzo vya mapato, hivyo eneo hilo la NDC ni muhimu na litasaidia kuongeza mapato.

 

Katika Hatua nyingine, amewapongeza watendaji wote wa Sekretarieti ya Mkoa na wa Halmashauri zote za Mkoa wa Pwani kwa utendaji wa kazi na kupelekea mkoa kushika nafasi ya tatu nchini kwa kigezo cha makusanyo yanayotokana na mapato ya ndani.

 

Nae Mkurugenzi Mtendaji Wa shirika la Maendeleo ya Taifa NDC  Dr. Nicolaus Shombe alifafanua kuwa Kongane la Viwanda TAMCO, Kibaha lina eneo lenye ukubwa wa ekari 201.63 na limeteuliwa kujenga Viwanda katika Makundi matatu aliyoyataja kuwa ni Viwanda vya madawa na vifaa tiba, viwanda vya kuunganisha magari na mitambo pamoja na viwanda vya nguo.

 

Alisema eneo hilo linahitaji miundombinu ya barabara kama kilomita 4.8 na tayari Kilomita 1.6 imeshajengwa.

 

Dr. Shombe  alieleza ,tayari eneo hilo limepelekewa umeme wa Kv 33 na TANESCO huku miundombinu ya maji ikiwa inaendelea kuboreshwa.