Wednesday, August 10, 2022

DC. BAGAMOYO AFANYA KIKAO NA KAMATI YA SENSA WILAYA.

 May be an image of 2 people, people sitting and indoor

Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe Zainab Abdallah, akizungumza katika kikao alipokutana na Kamati za Sensa za Halmashauri za Bagamoyo na Chalinze.

.................................

 

Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe Zainab Abdallah Amefanya Kikao na kamati ya Sensa ya Wilaya pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama (KUU) ya Wilaya kufuatia maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi inayotarajiwa kufanyika tarehe 23/08/2022.

 

Mkuu huyo wa Wilaya pia ameendelea kuwasisitiza Wananchi wa Bagamoyo, wawe tayari kuhesabiwa Tarehe 23 Mwezi huu itakapofika ili kusaidia serikali iweze kupanga Mipango ya maendeleo kwa Miaka 10 ijayo.

 

Alisema ili serikali iweze kupanga mambo mbalimbali ya maendeleo inahitaji kuwa na idadi ya wananchi wake iliyo sahihi kwaajili ya kufikisha huduma za jamii mahitaji yaliyo sahihi.

 

Kikao cha kamati ya sensa kimefanyika ili kufanya tathmini ya mwenendo mzima wa maandalizi ya zoezi la sensa na hali halisi ya mwenendo wa mafunzo ya wataalam na makarani watakao shiriki zoezi hilo adhimu la serikali siku ya tarehe 23 Agosti mwaka huu.

Wakitoa taarifa ya zoezi hilo waratibu wa sensa ya watu na makazi kwa halmashauri zote mbili ya Chalinze na Bagamoyo, walieleza jumla ya makarani 991 wanaendelea na mafunzo kwa siku 15 katika halmashauri ya Chalinze na makarani 418 wanaendelea na mafunzo kwa hamashauri ya Bagamoyo.

 

Katika kikao hicho wajumbe wamekubaliana kwa pamoja kuhakikisha wananchi wanahamasishwa kushiriki katika zoezi la sensa kupitia michezo mbalimbali pia kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

Aidha katika kikao hicho wajumbe walikubaliana kuwa wenyeviti wa vitongoji wahakikishe wanahamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi la sensa na kutoa ushirikiano wa hali ya juu kwa makarani katika kuwaongoza kuwafikia wananchi.

 

Ikumbukwe kuwa Sensa ya Watu na Makazi hufanyika kila baada ya Miaka 10 ambapo Sensa ya Mwaka huu 2022 ni Sensa ya watu na makazi.

May be an image of 3 people and people sitting

 

May be an image of 7 people, people sitting and indoor

 

No comments:

Post a Comment