Wednesday, January 1, 2020

RAIS DK SHEIN AONGOZA WANAVIKUNDI KATIKA TAMASHA LA SITA LA MATEMBEZI NA MAZOEZI ZANZIBAR.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk,Ali Mohamed Shein katikati akiongoza Viongozi na Wananchi mbalimbali katika Tamasha la Sita la matembezi na mazoezi ya viungo lililoanzia Ukumbi wa Sheikh Abdulwakil,Michenzani,Uwanja wa kufurahishia watoto Kariakoo,Matumbaku na kumalizia Uwanja wa Mao Zedong Wilaya ya Mjini Unguja. Ikiwa ni Shamra shamra za miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein akisisitiza jambo alipotoa hotuba katika Tamasha la Sita la Matembezi na  mazoezi ya viungo lililoanzia Ukumbi wa Sheikh Abdulwakil,Michenzani,Uwanja wa kufurahishia watoto Kariakoo,Matumbaku na kumalizia Uwanja wa Mao Zedong Wilaya ya Mjini Unguja. Ikiwa ni Shamra shamra za miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk,Ali Mohamed Shein katikati akiongoza Viongozi na Wananchi mbalimbali katika Tamasha la Sita la matembezi na mazoezi ya viungo lililoanzia Ukumbi wa Sheikh Abdulwakil,Michenzani,Uwanja wa kufurahishia watoto Kariakoo,Matumbaku na kumalizia Uwanja wa Mao Zedong Wilaya ya Mjini Unguja. Ikiwa ni Shamra shamra za miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Vikundi mbalimbali vya mazoezi vikipita eneo la Michenzani kisonge katika Tamasha la Sita la mazoezi ya viungo lililoanzia Ukumbi wa Sheikh Abdulwakil,Michenzani,Uwanja wa kufurahishia watoto Kariakoo,Matumbaku na kumalizia Uwanja wa Mao Zedong Wilaya ya Mjini Unguja. Ikiwa ni Shamra shamra za miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Tuesday, December 24, 2019

WANANCHI MOROGORO WATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI

Na.Farida Saidy,Morogoro

Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Morogoro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, (SACP)  wilbrod mutafungwa, ametoa wito kwa wanachi mkoani humo, kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili taarifa zote zinazohusu viashiria vya uhalifu  vifanyiwe kazi mara moja.


Ametoa rai hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari  amesema hali ya mkoa huo ni shwari na kwamba hakuna matukio makubwa yanayotishia usalama wa raia na mali zao, na kuongeza kuwa bado wanaendelea na jitihada mbalimbali za kukabiliana na matukio ya kiuhalifu na wahalifu.


Mutafungwa amesema katika msimu huu wa sikukuu za krismas na mwaka mpya polisi mkoa wa morogoro wamejipanga vizuri kuhakikisha wananchi wanahudhuria katika nyumba za ibada na kushiriki ibada za kusherehekea siku hizi kwa utulivu na amani.


Hata hivyo, kamanda mutafungwa amesisitiza kuwa kutakuwa na ulinzi wakutosha katika nyumba za ibada, majengo ya serikali, benki, masoko, kumbi za starehe, viwanja vya michezo pamoja na kuimarisha doria katika barabara zote kuu pamoja na barabara za mitaani, kwamba kutakua na doria za masafa marefu, pamoja na doria za miguu na doria zinazoambatana na wanyama wakali (mbwa wa polisi).


Katika hatua nyingine jeshi la polisi limetoa motisha kwa askari wake ambapo walishiriki kuokoa maisha ya baba na motto ambalo limetokea siku chache zilizopita katika maporomoko ya nguzo campsite.


Kwa upande wake diwani wa kihonda khamisi kilongo, ambapo ndio wanapoishi baba huyo na mwanaye amelipongeza jeshi la polisi kwa hatua iliyochukua na kusema ni hatua kubwa katika kuleta hamasa kwa askari katika kufanya vizuri na ameomba hii iwe zoezi endelevu kimkoa na ikiwezekana hata taifa zima.


Onesmo kahemere ni miongoni mwa askari walioshiriki uokoaji ameelezea jinsi hali ilivyokua ambapo amesema kama askari licha ya kuwa alikua akitimiza wajibu wake lakini pia aliguswa kibinaadamu kufanya hivyo.

MLANDIZI QUEEN'S YAVAMIA MKUTANO WA UWT


Pichani Zuhura Mizava mmoja wa wajumbe wa (UWT) Kibaha Vijijini akisaini karatasi ya kuchangia klabu ya soka ya Wanawake ya Mlandizi Queen's inayoshiriki Ligi kuu ya Wanawake, kulia ni Nahodha wa timu hiyo Wema Richard. Picha na Omary Mngindo.

Picha ya kwanza Diwani wa Kata ya Mlandizi Kibaha Vijijini Mkoa wa Pwani Euphrasia Kadala akisaini karatasi ya kuchangia klabu ya soka ya Wanawake ya Mlandizi Queen's inayoshiriki Ligi Juu ya Wanawake, kushoto Nahodha wa timu hiyo Wema Richard. Picha na Omary Mngindo.
........................................

Na Omary Mngindo, Mlandizip

UONGOZI wa klabu ya soka ya Wanawake ya Mlandizi Queen's inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara ya Mlandizi Mkoa wa Pwani, umevamia Mkutano wa Jumuia ya Wanawake (UWT) wilayani hapa wakihitaji ushirikiano wao.

Nahodha wa timu hiyo Wema Richard akiambatana na mchezaji mwandamizi wa timu hiyo, Jamila Hassan, Wema aliwaambia wana-UWT hao wa Kibaha Vijijini kwamba, timu yao ipo kambini kwa muda mrefu na kwamba wanakabiliwa na changamoto mbalimbali.

Alisema kuwa wanashiriki Ligi Kuu ya wanawake inayoshirikisha timu 12 kutoka mikoa mbalimbali, ambapo katika kinyang'anyiro hicho pamoja na kupambana kuuwakilisha Mkoa wa Pwani, wanakabiliwa na changamoto nyingi na kwamba wanahitaji ushirikiano wa hali ya juu.

"Tulivyosikia Mama zetu mpo hapa kwa ajili ya kikao cha kikazi, nasi watoto wenu tukaona tutumie fursa hii kuja kuwataka muungane nasi kwa hali na mali katika ushiriki wetu, kwani tunawawakilisha wanawake wote kuanzia hapa Mlandizi na Mkoa kwa ujumla," alisema Wema.

Kwa upande wake Jamila alisema kuwa ligi hiyo yenye ushindani wa hali ya juu, pamoja na kupambana kwao lakini wanakabiliwa na ukata wa kifedha, hivyo kuwaomba wana-UWT hao na wapenda michezo popote walipo wawaunge mkono katika hilo.

"Ligi ya msimu huu yenye timu 12 inayochezwa nyumbani na ugenini, imekuwa na ushindani wa hali ya juu, na kwamba tumecheza mechi 4, tumeshinda moja, tumepoteza tatu, lakini tunawaahidi tutapambana kuhakikisha tunafanya vizuri zaidi," alisema Jamila.

Mmoja wa wana-UWT hao Salha Adinani amewapongeza kwa ushiriki wao, na kwamba kikubwa wanatakiwa kuendelea kupambana katika ushiriki huo, huku akiwaomba wasichana kujitambua katika mavazi.