Wednesday, September 11, 2019

TANZANIA IPO TAYARI KUTOA USHIRIKIANO KWA WAWEKEZAJI

Waziri wa Mambo ya nje, Ramadhan Mwinyi akizungumza kwa niaba ya waziri wa viwanda na biashara leo wakati wa uzinduzi wa wiki ya biashara ya wamisri hapa nchini inayoendelea kufanyika katika hoteli ya Hyatt (Kilimanjaro) kuanzia leo Septemba 11 hadi 14 jijini Dar es Salaam.
........................


Serikali ya Tanzania kupitia sekta binafsi ipo tayari kutoa ushirikiano kwa wawekezaji hapa nchini.

Hayo yamesemwa na mwakilishi wa waziri wa viwanda na biashara, waziri wa mambo ya nje, Ramadhan Mwinyi alipokuwa akizungumza na wafanyabiashara wa nchini Misri na watanzania wakati wa ufunguzi wa wiki ya maonesho ya kibiashara yanayofanyika katika hoteli ya Hyatt (Kilimanjaro) kuanzia leo Septemba 11 hadi 14 jijini Dar es Salaam.

"Tanzania ipo tayari kutoa ushirikiano kwa wawekezaji hapa nchini katika sekta ya marighafi za ujenzi, nishati ya jua, kemikali pamoja na viwanda vya uhandisi".

Nae Rais wa chemba ya wafanyabiashara hapa nchini, Paul Koyi amesema kuwa jukumu lao ni kufanya jambo la kibiashara lisilowezekana kuwezekana ili biashara ziweze kufanyika bila vikwazo. Pia amesema kuwa katika kufanya biashara kunahitaji matendo zaidi na si maneno.

Amesema hii ni fursa kwa watanzania kuungana na kufanya biashara na wamisri kwaajili ya maendeleo ya nchi pamoja na maendeleo yao wenyewe.

Wiki ya maonesho ya biashara ya wamisri yanaendelea kufanyika katika hoteli ya Hyatt Regency (Kilimanjaro) jijini Dar es Salaam kuanzia leo Septemba 11 hadi 14, 2019.
Mkuu wa taasisi ya sekta binafsi (Tpsf), Zachy Mbenna akizungumza katika uzinduzi wa wiki ya biashara ya Misri na Tanzania inayoendelea kufanyika jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Hyatt Regency (Kilimanjaro) kuanzia leo Septemba 11 hadi 14, 2019. Amesema kuwa wafanyabiashara wachukue Fursa hiyo ambapo wafanyabiashara wa nchini Misri wamekuja nchini kuonesha biashara zao katika mambo ya Dawa, marighafi za ujenzi, nishati ya jua, kemikali pamoja na viwanda vya uhandisi ni fursa wa watanzania hapa nchini kujifunza.
 

Rais wa  chemba ya biashara, viwanda na kilimo, Paul  koyi akizungumza na wadau wa biashara wa tanzania na wamisri katika uzinduzi wa wiki ya maonesho ya kibiashara ya wafanyabiashara wa Misri yanayoendelea kufanyika katika hoteli ya Hyatt (Kilimanjaro) kuanzia leo Septemba 11 hadi 14 jijini Dar es Salaam.

 Balozi wa Misri Nchini Tanzania, Mohamed Abdulwafa akizungumza katika uzinduzi wa wiki ya maonesho ya kibiashara ya nchi ya Misri hapa nchini yanayoendelea kufanyika katika hoteli ya Hyatt Regency (Kilimanjaro) jijini Dar es Salaam 11 hadi 14 Septemba,2019.

Waziri wa Mambo ya nje, Ramadhan Mwinyi, Rais wa  chemba ya biashara, viwanda na kilimo, Paul  koyi, Mkuu wa taasisi ya sekta binafsi (Tpsf), Zachy Mbenna na Balozi wa Misri Nchini Tanzania, Mohamed Abdulwafa wakikata utepe kuzinduz wa wiki ya biashara ya wamisri hapa nchini inayoendelea kufanyika katika hoteli ya Hyatt (Kilimanjaro) kuanzia leo Septemba 11 hadi 14 jijini Dar es Salaam.

Tuesday, September 10, 2019

NG'OMBE ELFU KUMI WAVAMIA DUTUMI

Na Omary Mngindo, Mlandizi

Ng'ombe zaidi ya elfu kumi wanadaiwa kuingia katika Kijiji cha Madege kilichopo Kata ya Dutumi wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani pasipokufuata taratibu.

Hali hiyo inasababisha kuleta migogoro kati ya wenye mifugo hiyo na wakulima, ambao ndio wamiliki wa maeneo hayo kutokana na kutengwa maalumu kwa ajili ya kilimo na si kufugia.

Diwani wa Viti Maalumu Tarafa ya Ruvu Ester Dikoko, ameyaeleza hayo nwishoni mwa wiki kwenye baraza la madiwani chini ya Mwenyekiti Mansour Kisebengo, Makamu Fatma Ngozi aliyemaliza muda wake na Mkurugenzi Mtendaji Butamo Ndalahwa.

"Katika maeneo hayo hali ni mbaya, kuna kundi kubwa la mifugo ipatayo zaidi ya elfu kumi imeingia katika Kijiji cha Madege, hali inayosababisha migogoro isiyokwisha kuhusiana na uingiaji kwenye mashamba na kula vyakula," alisema Dikoko.

Nae diwani wa Kata ya Magindu Issa Mkali yeye ameiomba ofisi ya Mkurugenzi kutenga pesa katika bajeti ijayo, kwaajili ya kuboresha eneo la mnada wa mifugo uliopo Kijiji cha Magindu kwakuwa hauna mazingira mazuri.

"Niiombe ofisi ya Mkurugenzi katika bajeti ijayo itenge fedha kwa ajili ya kuboresha eneo la mnada kijiji cha Magindu, kwani kwa sasa una mazingira mabaya, jamii ya wafugaji na watu wanaopeleka biashara tofauti wanalalamikia mazingira yaliyopo," alisema Mkali.

Baada ya taarifa hiyo Kisebengo alimtaka Mwenyekiti wa Kamati husika Mohamed Samara atolee maelezo suala la mifugo, ambapo Samata alisema kuwa mifugo hiyo imeshaondolewa, imeelekea maeneo ya Kibiti na Rufiji.

"Mheshimiwa Mwenyekiti suala la mifugo ni kweli lilikuwepo lakini Kamati ya Ulinzi na Usalama imeshaipatia ufumbuzi kwa kuondolewa, na kwa taarifa iliyopo ni kwamba imeelekea maeneo ya Kibiti na Rufiji," alisema Samata.

Kuhusiana na suala la uboreshaji wa eneo la mnada wa mifugo, Mwenyekiti Kisebengo ameitaka ofisi ya Mkurugenzi kwenda kulifanyia kazi suala hilo, ili kuipatia ufumbuzi.